Counting Down: Lowassa na Dr. Magufuli, mpambano wa karne

Counting Down: Lowassa na Dr. Magufuli, mpambano wa karne

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Tunakaribia. Tunafika mwishoni. Tunafika pa kumaliza utata. Siku ya kupiga kura imegonga hodi. Zimebaki siku 12 za kampeni na moja ya kupiga kura. Mikutano ya kampeni inaendelea. Inazizima kutoka Dodoma hadi Ruvuma; Mbeya hadi Musoma. Mwanza nayo haiko nyuma. Lowassa na Dr. Magufuli. Historia inakwenda kuandikwa na mmoja wao. Anakwenda kuwa Rais wa Tano wa Tanzania.

Mmoja wao anajiunga kwenye daftari la kumbukumbu lenye majina ya Hayati Mwalimu Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na Rais Kikwete. Mmoja wao atapigiwa kura za ushindi hapo Oktoba 25 mwaka huu. Tangu kampeni zianze, Lowassa na Dr. Magufuli wanachuana kwelikweli. Wanapiga kampeni za kusheheni sera, kuomba kura na mwitiko wa vituko. Hakika, ni mpambano wa kukata na shoka.

Kwa mara ya kwanza, CCM haina uhakika wa ushindi. Si Urais, Ubunge wala Udiwani. Kwa mara ya kwanza, CCM inatumia kila mbinu lakini wapinzani wanazing'amua na kushambulia. Ni piga-nikupige; fanya nikuige. Ni mwendo wa kupita nifute; umati wako si kama wangu. Uchaguzi wa maamuzi. Tanzania mpya yaja. Ni kwa mara ya kwanza, wanawake na wazee nao wanatamani kuwapigia kura wapinzani. Wananchi hawatishiki kirahisi.

Kadiri tunavyosogelea na kukaribia Oktoba 25, ndivyo homa ya mabadiliko yao au yetu inavyozidi kupanda. Hata maji yaliyokuwa ya moto sasa yameganda. Aliyekuwa njia nyoofu sasa yuko njia panda. Hapatoshi. Mpira unachezwa Muheza, washangiliaji wako hadi Mwanza. Pwani,Tabora, Ruvuma,Morogoro,Dodoma,Rukwa,Tanga na Mtwara mbioni kuonja Wabunge wa upinzani.

Binafsi, natabiri kuwepo kwa Serikali ya mseto kwakuwa hakuna dalili zozote za chama kimoja hapa Tanzania kupata Urais, wingi wa Ubunge na Udiwani. Tanzania mpya imefika!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
VUTA-NKUVUTE

Lowassa atashinda urais... Wabunge wengi watakuwa wa CCM... Huo ndio ukweli, na kwa namna hiyo serikali ya mpito inawezekana...

Ingawa CCM wasisahau Lowassa bado ana watu wake huko ambao watakuwa wabunge kama Bashe, Kingu, Serukamba, Chegeni nk. Hawa wataungana na Ukawa na kuizika rasmi CCM hasa kwenye kumpitisha waziri mkuu
 
Last edited by a moderator:

Labda urais wa watu wanaojinye na si urais wa nchi. Ikulu hawezi kwenda fisadi
 
Raisi wetu ni Lowassa eeh, nachingwea na rorya kila kona ni lowassa. Tanzania mpya inakuja
 
Haki ikitendeka, Lowassa ataunda serikali. Atapata kura nyingi mno na hata wabunge watapatikana wa kutosha kuunda serikali.
Nani atampa mamlaka hayo? Mnadhani nchi hii watu hawana akili? Subirini kipigo ndani ya ballot box
 
Raisi wetu ni Lowassa eeh, nachingwea na rorya kila kona ni lowassa. Tanzania mpya inakuja
Huko Nachingwea ndo usiseme kabisaaa! Leo Magufuli yupo huko. Hakika mji wa Nachingwea umesimama. Kule hakuna upinzani kabisa
 
Huko Nachingwea ndo usiseme kabisaaa! Leo Magufuli yupo huko. Hakika mji wa Nachingwea umesimama. Kule hakuna upinzani kabisa

Kingunge akipita wala hakuna atakayemkumbuka magufuli
 
Huu mpambano wa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu una msisimko mkubwa na ni mpambano w karne kama lilivyokuwa pambano la ngumi kati ya Mayweather na Manpaciao.
 
Labda urais wa watu wanaojinye na si urais wa nchi. Ikulu hawezi kwenda fisadi
Hizo kauli zenu magamba zenye nia ya kumdhalilisha Lowassa ndiyo zinazidi kufanya wananchi wazidishe marafufu mahaba yao kwake.

Kama tulivyoona jana kule Musoma mjini ambako wananchi walidiriki 'kuideki' barabara aliyokuwa akipita Rais mtarajiwa Edo.
 
Back
Top Bottom