Counting Down: Lowassa na Dr. Magufuli, mpambano wa karne

Counting Down: Lowassa na Dr. Magufuli, mpambano wa karne

Serikali ya mseto ya nini?Rais ni Lowassa pekee,naona mmeona mambo magumu mnaanza kubembelezea serikali ya mseto.
 
Kwa sasa Edo yuko Bunda. Watu wanakanyagana walao kumwona tu zile mnvi zake. He's the 5th Tz president for sure!!
 
Serikali ya mseto ya nini?Rais ni Lowassa pekee,naona mmeona mambo magumu mnaanza kubembelezea serikali ya mseto.


Serikali ya mseto kwa nchi za afrika itakuwa ngumu sana.
Ukawa wakichukua bunge na CCM wakichukua serikali kuna hatihati serikali ya magufuli ikapelekeshwa kiasi cha kushindwa kufuata maazimio ya bunge.
Kwa serikali iliyojaa wizi na ufisadi basi bunge linaweza hata kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais.
 
Haya maneno sijuhi mara mpambano wa karne mara sijuhi hapakaliki ..haya maneno mmemezeshwa na nyie mmeyameza bila kuyatafuna ..yatawakwama!
 
Ni uchaguzi wa historia maana haijawahi kutokea wagombea uraisi wenye mvuto mkubwa kwenye kinyang'anyiro hiki walikuwa chama kimoja miezi miwili iliyopita! CCM "A' na CCM"B" hadi mgombea mmoja akijisahau kwamba kahama chama akatoa kibwagizo cha CCM Oyee!..
Wananchi waweke utaifa mbele badala ya chama na kuchagua mtu mwenye uwezo wa kweli kuleta mabadiliko tunayoyataka!
Hasira Hasara.. Tukichagua kwa jazba tutachagua "garasa".. Na itatulazimu tusote kwa miaka mingine mitano..SISI SOTE NI NDUGU.. VYAMA NI NGUO TU TULIZOVAA!!

Mungu Ibariki Tanzania.. Mungu bariki Uchanguzi wetu uwe wa Amani..
 
Tunakaribia. Tunafika mwishoni. Tunafika pa kumaliza utata. Siku ya kupiga kura imegonga hodi. Zimebaki siku 12 za kampeni na moja ya kupiga kura. Mikutano ya kampeni inaendelea. Inazizima kutoka Dodoma hadi Ruvuma; Mbeya hadi Musoma. Mwanza nayo haiko nyuma. Lowassa na Dr. Magufuli. Historia inakwenda kuandikwa na mmoja wao. Anakwenda kuwa Rais wa Tano wa Tanzania.

Mmoja wao anajiunga kwenye daftari la kumbukumbu lenye majina ya Hayati Mwalimu Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na Rais Kikwete. Mmoja wao atapigiwa kura za ushindi hapo Oktoba 25 mwaka huu. Tangu kampeni zianze, Lowassa na Dr. Magufuli wanachuana kwelikweli. Wanapiga kampeni za kusheheni sera, kuomba kura na mwitiko wa vituko. Hakika, ni mpambano wa kukata na shoka.

Kwa mara ya kwanza, CCM haina uhakika wa ushindi. Si Urais, Ubunge wala Udiwani. Kwa mara ya kwanza, CCM inatumia kila mbinu lakini wapinzani wanazing'amua na kushambulia. Ni piga-nikupige; fanya nikuige. Ni mwendo wa kupita nifute; umati wako si kama wangu. Uchaguzi wa maamuzi. Tanzania mpya yaja. Ni kwa mara ya kwanza, wanawake na wazee nao wanatamani kuwapigia kura wapinzani. Wananchi hawatishiki kirahisi.

Kadiri tunavyosogelea na kukaribia Oktoba 25, ndivyo homa ya mabadiliko yao au yetu inavyozidi kupanda. Hata maji yaliyokuwa ya moto sasa yameganda. Aliyekuwa njia nyoofu sasa yuko njia panda. Hapatoshi. Mpira unachezwa Muheza, washangiliaji wako hadi Mwanza. Pwani,Tabora, Ruvuma,Morogoro,Dodoma,Rukwa,Tanga na Mtwara mbioni kuonja Wabunge wa upinzani.

Binafsi, natabiri kuwepo kwa Serikali ya mseto kwakuwa hakuna dalili zozote za chama kimoja hapa Tanzania kupata Urais, wingi wa Ubunge na Udiwani. Tanzania mpya imefika!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

chief, huu uandishi wako unashahibiana sana na wa gwiji Ndimara Tegambwage.

au wewe ndiye?
 
Back
Top Bottom