(---) Onesmo Mushi
Niliwahi kuuliza hili swali huko nyuma kuhusu #SGR na ninaomba kuliuliza tena baada ya kuona taarifa ya TAZARA⬇️.
C&P
NATAMANI KUFAHAMU MIPANGO YA KUENDESHA SGR
Tangu kuanzishwa kwake 1970s, reli ya TAZARA imekuwa ikifanya kazi kwa hasara.
Freight capacity ya TAZARA ni tani milioni tano kwa mwaka. Lakini ni asilimia 4% tu za huu uwezo zimekuwa zikitumika.
Kwa mfano, mwaka 2023 TAZARA ilisafirisha tani 251,264 tu, sawa na asilimia 5.02% ya uwezo.
Kwenye report ya kamati ya bunge miundombinu 2020, kamati ilionesha wasiwasi wa TAZARA kufilisika na kuomba serikali iingilie kati angalau kwa kuipa mtaji wa kujiendesha.
Reli ya Kati, Dar-Kigoma nayo ina ugonjwa huo huo. Ina uwezo wa kubeba tani millioni tano kwa mwaka lakini mzigo ambao imekuwa ikibeba mpaka hivi karibuni haufiki hata asilimia 3% ya capacity yake (rejea taarifa ya Central Corridor Transit).
Reli ya Dar-Arusha ndio kama ilishakufa kabisa, haina hata maana kuzungumzia capacity yake.
Hii miradi inatengenezwa kwa fedha za watanzania maskini na jasho lao.
Kama sikosei TAZARA ni credit ya serikali ya China na juzi tumeiombea mkopo Benki ya Dunia dola million 200, zaidi ya Bilioni 500, kuiboresha.
SGR na yenyewe hivyo hivyo, tumekopa kila kona kuijenga. Juzi tu Benki ya Standard Chartered imetukopesha Trillion tatu za huu mradi. Tunaambiwa mpaka ukamilike utatumia zaidi ya trillion 23 zitakazolipwa kwa kodi za watanzania.
Reli ya Dar-Arusha nayo hivyo hivyo, juzi Rais Magufuli ametumia zaidi ya Bilioni 10 kuifufua na sina hakika kama inafanya kazi hivi sasa.
Swali la msingi tunalotakiwa kujiuliza, ni mipango gani maalum iliyopo itakayohakikisha SGR haigeuki kuwa TAZARA na reli nyingine ambazo ama zimekufa au zinaelekea kufa?
Ni kweli SGR ni “MRADI WA KIMKAKATI” lakini faida yake haipo kwenye uwepo wake tu. Faida ya SGR itakuwa kwenye kutumia uwezo wake.
Kuna mipango gani itakayohakikisha kuna uzalishaji wa kutosha utakaoiwezesha SGR kusafirisha mizigo inayoendana na capacity yake?
Ni mikakati gani iliyopo itakayohakikisha SGR inakuwa competitive kiasi cha kushindana na biashara za malori ya mizigo na mabasi ya abiria?
Mi utaratibu gani umeandaliwa ili kutengeneza co-existence ya SGR na njia nyingine za usafirishaji ili kuhakikisha kuwa sekta zote zinasaidiana kukua kwa maslahi ya watanzania watanzania badala ya sekta moja kuiua nyingine?
Kwa sasa tupo katika euphoric state kwa sababu ya upya wa SGR, lakini baada ya muda mfupi tu SGR itageuka kuwa huduma ya kawaida.
Ni mipango gani itakayotuendesha baada ya hii “ashki” kuisha?