Content kwa tovuti za habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Content kwa tovuti za habari

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Aug 16, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Aug 16, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Katika blogu yangu mmoja nimekuwa napokea matangazo ya nchi jirani ambayo yanataka content developers ,wataalamu wa kuendeleza tovuti na vitu ndani ya tovuti hiyo ili ivutie na pamoja na kuweka habari mbali mbali , lakini hii imekuwa ni kwa nchi jirani .
  Hapa nchini kwetu sijawahi kuona matangazo kama hayo , mengi utasikia website developer , ingawa hivi ni vitu viwili tofauti , hao ni watu ambao wanatakiwa kushirikiana katika kuendeleza vitu vilivyomo ndani ya tovuti husika .
  Umewahi kutembelea tovuti mbali mbali haswa za kiswahili , ukakuta matangazo katika tovuti hizo yanayokutaka wewe utangaze bidhaa zako au kitu chako katika tovuti hiyo jibu lako litakuwa ni ndio je umewahi kutembelea tovuti hiyo hiyo kwa miaka 2 iliyopita tangazo ukalikuta pale pale na hakuna kampuni au mtu aliyevutiwa na kuweka tangazo lake pale ?
  Kama umewahi kuona vitu kama hivyo lazima utakuwa umejiuliza pia kwanini basi watu au kampuni hazivutiwi na kutangaza katika tovuti au forum husika ingawa imekuwepo kwa muda mwingi inawatembeleaji wengi na inajulikana lakini watangazaji hawataki kupeleka bidhaa zao huko kutangazwa .
  Moja ya matatizo ya tovuti na majukwaa hayo ni kitu kinachoitwa content , yaani content ya tovuti au jukwaa husika ndio inayochangia sana katika kufanya watu washindwe kutangaza bidhaa zao au kitu humo , au kampuni zingine pia zishindwe kutangaza na tovuti au jukwaa husika .
  Pia umewahi kutembelea tovuti mfano www.globalpublisherstz.com hii ni tovuti ya habari ambayo ilikuja kupitwa mbali na blogu ndogo kama www.bongocelebrity.com , tembelea mfano bongo celebrity na global halafu uone tofauti yake ni contents hiyo hiyo .
  Tovuti nyingi sana na forums mbali mbali za kitanzania zimekosa content na watu wa kuendeleza content zilizokwepo ili ziweze kuvutia watangazaji katika tovuti hizo kama kampuni za simu , kampuni za vinywaji , vijarida vya habari vingine na mambo mengine mengi mengi sana .
  Mwaka jana nchini kenya kulikuwa na mkutano ambao ulikutanisha Wadau wa masuala ya Content , moja ya malengo yao katika mkutano huo kwanza ilikuwa ni kudumisha mila na desturi katika tovuti zote zinazohusu masuala yao ya ndani na pia kuwa na aina yao ya content kama standard kwa ajili yao wakenya .
  Pamoja na mkutano huo mwaka huu pia kumekuwa na tamasha lingine ambalo lilitoa zawadi mbali mbali kwa wadau mbali mbali wa contents na mambo mengine yanayohusu ICT katika nchi hiyo haswa vijana .
  Naamini hata nchini Tanzania kuna watu wenye uwezo wa kufanya kazi hizi za kuboresha tovuti na majukwaa mengine mbali mbali ili tufike hatua nzuri za kibiashara huko mbeleni .
  Kazi ya content development imekuwa profesional sasa hivi , tovuti mbali mbali haswa za nchi zingine wanakuwa wanataka content developers kwa ajili ya kuendeleza na kuandika tovuti zao haswa zinazohusu habari na mambo mengine ya mawasiliano .
  Mwisho ni kwa wamiliki wa tovuti za habari na burudani kaeni na content developers wataweza kuwasaidia sana katika kuendeleza majukwaa na tovuti zetu za habari na mtapata matangazo mengi sana yatakayoweza kuwaletea pesa na kuendeleza hizo kampuni zetu kwa njia moja au nyingine .
   
Loading...