Confusion ya Marafiki, Please help!

Confusion ya Marafiki, Please help!

Fixed Point

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2009
Posts
11,304
Reaction score
12,753
Jamani tumesalimika ndugu zangu?
Nina hili jambo huwa naliwaza sana na labda sielewi kwa nini watu wengi wana mtazamo tofauti na ninavyoamini mimi...
Ni hili swala la marafiki wa kuambatana nao (hapa naongelea marafiki wa kawaida tu na siyo wapenzi).
Watu wengi wanasisitiza sana watu wasiambatane na marafiki wenye tabia "mbaya" kwa sababu wanazozijua wao. na hili limenichanganya zaidi baada ya kulisikia jana kwa mtu ambaye sikutegemea angewaza hivi.
Mimi naamini unaweza kuwa na marafiki wenye hizo tabia na wewe usiwe/usiige hizo tabia zao.
Labda mimi sielewi mtu mzima unawezaje kuwa influenced na tabia ya mtu mwingine ambayo unaona siyo nzuri?

NOTE: HII NAONGELEA WATU WAZIMA AMBAO WANAJUA KUTOFAUTISHA JEMA NA BAYA, TUSIHUSISHE WATOTO KATIKA MJADALA HUU

Fuata nyuki..................,ukikaa karibu na waridi...............ukitembeana na mchina lazima utajua katare
 
Ndege waliofanana huruka pamoja, so haiwezekani mkawa marafiki wakati Tabia zinatofautiana, ni lazima kuna tabia zinazofanana. Ni sawa na kukaa na Mwizi lazima nawe iko siku utaiba tu, Au kukaa karibu na Uaridi lazima unukie vile, au kukaa na mtu mwenye Pesa kwa vyovyote nawe utakuja pata pesa, So be care kwa uambiwacho.
 
huu ndo ubinafsi, it is all about nitapata nini toka kwa hawa watu....
kwa nini usiamue wewe kuwa waridi kwa hao wenye tabia zisizofaa? i.e. wao wanukie toka kwako
 
Swala la kuwa "bendera fuata upepo" sio la watoto tu, hata watu wazima wapo wanaofuata mkumbo sana tu. Na watoto wapo wengi tu wenye misimamo wasioiga iga mambo hovyo, niliwahi kuwa mmoja wao.

Binafsi naamini mtu wa kupotoka atapotoka tu hata awe na marafiki wazuri namna gani, maana asiposhawishiwa na marafiki atashawishiwa na wapita njia. Na mtu mwenye msimamo wake hawezi kuwa na tabia za ajabu ajabu kisa tu ndo marafiki zake walivyo. Kama mimi marafiki zangu wengi wanatumia pombe ila mie sijawahi na wala sitarajii japo wapo wanaoshawishi hata nijaribu tu. Ukiwa mtu mwepesi kufuata mkumbo na kutaka kufurahisha (please) kila mtu ndio huo msemo wa "Ndege wafananao huruka pamoja" unakuhusu.
 
hapo kwenye RED nimewahi kuulizwa na watu siku "inawezekanaje fulani ni rafiki yako lakini mna tabia tofauti? mbona wewe hauko kama yeye?"
Mimi naamini ukishakuwa mtu mzima unajua kabisa kuwa hiki kitu siyo kizuri na ukajiepusha nacho, na ni vizuri kama rafiki zako wana tabia ambazo unaona hazifai ukawarudisha kwenye mstari
 
Ndege waliofanana huruka pamoja, so haiwezekani mkawa marafiki wakati Tabia zinatofautiana, ni lazima kuna tabia zinazofanana. Ni sawa na kukaa na Mwizi lazima nawe iko siku utaiba tu, Au kukaa karibu na Uaridi lazima unukie vile, au kukaa na mtu mwenye Pesa kwa vyovyote nawe utakuja pata pesa, So be care kwa uambiwacho.

Hahahahah, kaaazi kweli kweli.
Eti "ukikaa na mtu mwenye pesa kwa vyovyote nawe utakuja pata pesa".
 
Swala la kuwa "bendera fuata upepo" sio la watoto tu, hata watu wazima wapo wanaofuata mkumbo sana tu. Na watoto wapo wengi tu wenye misimamo wasioiga iga mambo hovyo, niliwahi kuwa mmoja wao.

Binafsi naamini mtu wa kupotoka atapotoka tu hata awe na marafiki wazuri namna gani, maana asiposhawishiwa na marafiki atashawishiwa na wapita njia. Na mtu mwenye msimamo wake hawezi kuwa na tabia za ajabu ajabu kisa tu ndo marafiki zake walivyo. Kama mimi marafiki zangu wengi wanatumia pombe ila mie sijawahi na wala sitarajii japo wapo wanaoshawishi hata nijaribu tu. Ukiwa mtu mwepesi kufuata mkumbo na kutaka kufurahisha (please) kila mtu ndio huo msemo wa "Ndege wafananao huruka pamoja" unakuhusu.
asante sana kwa mchango mzuri.....
hapo kwenye RED labda ndo haswa panahusika..... urahisi wako wa kuiga mambo mabaya, haihusiani kama marafiki zako wana tabia mbaya au la.
Asante sana
 
Hahahahah, kaaazi kweli kweli.
Eti "ukikaa na mtu mwenye pesa kwa vyovyote nawe utakuja pata pesa".
Umeona eeeh!
watu wapo about kupata kupata.... mbona hawasemei kutoa? huu ubinafsi utaisha kweli jamani?
 
huu ndo ubinafsi, it is all about nitapata nini toka kwa hawa watu....
kwa nini usiamue wewe kuwa waridi kwa hao wenye tabia zisizofaa? i.e. wao wanukie toka kwako

Chances are 50/50 to influence or to be influenced with.But its more likely if u hang up with bad company in one way or another,direct or idirect u will be affected by it.
 
Hahahahah, kaaazi kweli kweli.
Eti "ukikaa na mtu mwenye pesa kwa vyovyote nawe utakuja pata pesa".
Nilichokuwa namaanisha ni kwamba utajua njia zooote afanyazo kupata pesa zile so nawe utazifuata na kupata pesa.
 
Chances are 50/50 to influence or to be influenced with.But its more likely if u hang up with bad company in one way or another,direct or idirect u will be affected by it.
Nikiwa darasa la 5 tulihama mji na kuhamia sehemu nyingine. Mama alinitambulisha kwa mtoto wa rafiki yake (binti) ambaye tulikuwa tunasoma darasa moja.
Yule binti alikuwa anapenda sana wakaka, kila mtu alikuwa ananiambia nisicheze naye sababu atanifundisha tabia mbaya. Yule dada mpaka leo ni rafiki yangu sana na sikuwahi kuwa na hiyo tabia yake, ingawa wakati huo nilikuwa mdogo, sembuse huku ukubwani?
 
Nilichokuwa namaanisha ni kwamba utajua njia zooote afanyazo kupata pesa zile so nawe utazifuata na kupata pesa.
kuna wengine marafiki lakini wachoyo kwenye michongo ya hela!
 
binafsi huwa siamini dhana hii kwa mtu ambaye ni mzima na anautashi wake, ila tu hili linaweza kwa watoto ama wanafunzi.
mfano sio kwamba marafiki zangu wote nilionao wanatabia njema ila wapo ambao nawajua kabisa tabia zao ni mbaya na kuwa rafiki yao mimi natumika sana kuwarudisha kwenye mstari kila iitwapo leo.

mara nyingi sana ni vyema kumrekebisha mtu mwenye tabia mbaya kwa kuwa rafiki yake na kila siku akajifunza jambo toka kwako ama kwa kukusudia ama wakutokukusudia.

mf, ninaye wifi yangu ni MD sasa anapoishi kuna kijana mmoja mzazi wake alikuwa mkuu wa wilaya na sasa ni marhem huyu kijana kwa kukosa mtu wa kumwongoza amekuwa ni mlevi wa kupindukia hadi anajikojolea. sasa wifi yangu huyu kawa rafiki wa huyu kijana kiasi kwamba hata kwake anakuja wanaongea na wanatoka nae kwenda kunywa nia ya wifi ni kumbadilisha so anapokunywa nae yeye wifi anakunywa malta kijana anakunywa bia ila ana muhesabia zikifika 3 anamwambia haya sasa tuondoke uende nyumban ukalalale, kweli kijana kwa kuheshimu urafiki wake kwa wifi ananyanyuka na kurudi home kabla hajalewa. mumewe wifi imebidi amchukue huyu kijana awe anaenda nae kwenye kazi zake as a friend ili tu abadilike na kuacha pombe kabisa. kwangu mm niliwapongeza sana nikamwambia wifi yangu atakuwa na baraka sana manake anabadili wale ambao jamii inawadharau na kuwatenga.
 
Unazungumzia pia kuwa na marafiki toka jinsia nyingine............Wale vipanga ambao sketi haikatizi kwao.!
 
Thank you rafiki na mwalimu.....
tuna mawazo sawa kabisa rafiki yangu....
Umeweza kuelezea vizuri kabisa, siyo sababu napenda watu wawaze kwa upande huu, hapana.
Kuna siku dada mmoja akamwambia rafiki yetu "wewe unakubalije mumeo awe na rafiki kama yule? yule kaka hafai, atamfundisha mumeo tabia mbaya....."
Nikamwambia yule dada; kama mume wa huyu atafanya hayo unayoyasema, ni kwa sababu yeye kataka. unadhani huyo rafiki yake anaweza kumtafutia huyu mwanamke.... akamtafutia sehemu ya kukutana.... akamvua nguo.... na kumlazimisha kufanya hayo mambo? si atakuwa aliamua mwenyewe?
 
Unazungumzia pia kuwa na marafiki toka jinsia nyingine............Wale vipanga ambao sketi haikatizi kwao.!
rafiki ni rafiki mtani..... hata wale wa jinsia nyingine......
ukipanga wake unakuwa influenced na huyo rafiki, au ni tabia yake tu?
 
Jamani tumesalimika ndugu zangu?
Nina hili jambo huwa naliwaza sana na labda sielewi kwa nini watu wengi wana mtazamo tofauti na ninavyoamini mimi...
Ni hili swala la marafiki wa kuambatana nao (hapa naongelea marafiki wa kawaida tu na siyo wapenzi).
Watu wengi wanasisitiza sana watu wasiambatane na marafiki wenye tabia "mbaya" kwa sababu wanazozijua wao. na hili limenichanganya zaidi baada ya kulisikia jana kwa mtu ambaye sikutegemea angewaza hivi.
Mimi naamini unaweza kuwa na marafiki wenye hizo tabia na wewe usiwe/usiige hizo tabia zao.
Labda mimi sielewi mtu mzima unawezaje kuwa influenced na tabia ya mtu mwingine ambayo unaona siyo nzuri?

NOTE: HII NAONGELEA WATU WAZIMA AMBAO WANAJUA KUTOFAUTISHA JEMA NA BAYA, TUSIHUSISHE WATOTO KATIKA MJADALA HUU

Labda kabla ya kuchangia tujiulize urafiki ni nini hasa? Na unajengwa na nini? Na kigezo cha kuwa na rafiki ni kipi? Na yapi yanawaunganisha ktk urafiki?

Nikianza na hili swali la mwisho, urafiki mara nyingi hujengwa kwa njia mbali mbali ikiwepo kuunganishwa na watu au ndugu au marafiki wengine, kukutana kazini au shuleni au vyuoni nk, kwenye shughuli za biashara, kwenye vyombo vya usafiri, kwenye maeneo ya starehe, nyumba za ibada nk.

Lakini mvuto wa urafiki huletwa na vitu fulani common kati ya mtu na huyo rafiki. Inaweza kuwa wote ni wapenzi wa kitu fulani, washabiki wa mpira, majirani manosaidiana nk nk. Ktk hali hiyo ya urafiki hujikuta wakitoka pamoja, kuenjoy pamoja, kutembeleana, kuongelea mambo fulani yenye mtazamo unaofanana nk

Hali hii hulazimisha jamii kuona kuwa marafiki wanatabia zinazofanana, Na hata kama ikitokea kuwa wanatabia ambazo hazifanani, basi kuna uwezekano mkubwa wa mmoja wapo kuiga tabia za mwenzake pasipo yeye kujijua na kujikuta wakidumisha urafiki wao. Ni vigumu ingawa inawezekana sana kuwa na urafiki na mtu ambaye mmepishana sana kitabia au interest. Ktk hali hii pia ni wachache sana wenye uwezo wa kuwa ndani ya urafiki lakini wakaweza kudumisha imani, tamaduni na taratibu zake za kawaida za maisha bila kuwa influenced na tabia za marafiki wengine kwenye kundi lao na ndiyo maana kuna usemi wa ndege wenye rangi moja huruka pamoja!!!

Lakini hata hivyo naunga mkono hoja yako kwamba si vyema sana kuhukumu tabia ya mtu kwa sababu ya urafiki wake na mtu mwingine au kukatazwa kuwa rafiki na mtu kwa sababu za tabia za huyo kama kweli wewe ni mtu mzima na unajua nini unachofanya. Tahadhari ni kuwa mob psychology ni kitu hatari na hutokea pasipo kujua, so ni muhimu kuwa makini sana kwenye mahusiano haya.
 
rafiki ni rafiki mtani..... hata wale wa jinsia nyingine......
ukipanga wake unakuwa influenced na huyo rafiki, au ni tabia yake tu?

Kwangu mimi si tatizo. Miaka iliyopita nilishawishiwa sana na marafiki niwe napiga kilaji lakini sikushawishika mpaka nilipoamua mwenyewe tena baada ya kuhama mji.

Mtaa niliyozaliwa kulikuwa na vijana wa shoka (panga na bangi njenje) lakini mpaka leo sijatumia. So kwangu si tatizo.
Lakini pia maisha ni perception ...jinsi jamii inavyokutazama. Kwa mfano Wewe ni mwanamke na una urafiki na malaya wa kupindukia...kwake yeye noti kwanza, na anachokipata mnashea wote huko kwenye lunch na dinner za out........Na mara nyingine anakubeba kwenye gari alilohongwaa na mume wa mtu, Unajisikiaje? Maana kama ni kubadilika unaye mwaka wa kumi yupo vilevile!!
 
Back
Top Bottom