Confessions of an unfaithful husband | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Confessions of an unfaithful husband

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nduka, Jul 25, 2011.

 1. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mke wangu mpendwa!
  Nimekuwa nikiandamwa na msongo wa mawazo siku za karibuni kwa kuwa sasa nadhani nimefikia mwisho sina budi kukueleza aina ya mume uliyekubali kuwa naye hadi mungu atakapo tutenganisha. Najua wewe ni mpole na mvumilivu lakini ninayokwenda kuyasema ni mazito sana kwa moyo wa mwanadamu hivyo usinionee huruma kwa uamuzi utakao uchukua kwani tayari nimeukubali kabla sijaujua. Sijajua kosa ulilolifanya hadi kupewa adhabu ya mume kama mimi ila ninaamini aliyekuadhibu akiyasikia haya basi atakuandalia pepo yako mbinguni kwa kuwa umekwisha onja kiama hapa duniani, mke wangu:-

  1. Yule mtoto wa shangazi yako ninayemsomesha sifanyi hayo kwa mapenzi yangu kwako bali ninaficha ubaya tunaokufanyia, nimekuwa na uhusiano usiofaa na binti huyu tangu alipovunja ungo, miaka nane iliyopita.
  2. Msichana wa kazi uliyemfukuza kwa kuwa na ujauzito tukagombana sana na nilikuita majina yote mabaya ni kwa kuwa nilikuwa najaribu kumlinda kwa kuwa sikuwa na uhakika kama hiyo mimba hainihusu kwa kuwa nimetembea naye miezi ile miwili uliyokwenda mafunzo south africa.
  3. Nyumba unayoisifia sana aliyopanga shoga yako Suzzy wa Sinza, ninalipia mimi kodi na nimekuwa na uhusiano wa siri na rafiki yako Suzzy tangu mkiwa pamoja chuo kikuu.
  4. Ugomvi mara kwa mara ndani ya nyumba yetu mara zote huwa naupanga ili kuficha maovu yangu.
  5. Mke wangu sijawaji kukumbuka birthday yako hata siku moja ila ninaambiwa na rafiki yako Suzzy.
  6. Hata tabia ya kwenda Bar si kwa sababu ya kukutana na marafiki bali ni tabia yangu mbaya ya kupenda kuwashika shika makalio na matiti ma bar maid.
  7. Kinachonipeleka salon kufanya scrub si usafi mke wangu bali ni tamaa ya kushikwa shikwa na kutekenywa na wasichana wadogo wa salon, hii ndio sababu mara zote unaponunu dawa za scrub nyumbani nazipoteza au nasingizia zinanitoa chunusi.
  8. Mke wangu mimi sio shabiki kabisa wa mpira bali huwa nasingizia kupenda ili nilpate uhuru wa kutumia muda mwingi nje ya nyumbani.
  9. Mke wangu yule personal trainer wa gym nilimuajiri pia kukuangalia, kukuchunguza na pia kukujaribu ili nipate visingizio vya kukuacha tangu miaka miwili iliyopita lakini sikufanikiwa na alichoniambia ndicho kimenifikisha kwenye ungamo hili.
  10. Mke wangu pete yangu ya harusi haikupotea bali niliigawa kwa rafiki yako Suzzy siku ya pili baada ya ndoa kama ishara ya kuendela na pembe tatu yetu hii.

  Najua sistahili kusamehewa na kwa hilo sitakupa mzigo tena kwani ninajua umekuwa ni zaidi ya mke kwangu bali ni mlezi, kiongozi na mlinzi wa nyumba yetu.
  Ni mimi
  Mumeo Mkosefu.
   
 2. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu inahitaji roho ya chuma kuungama hivi..lakini k2 kimoja nilichokipenda na mimi nafikiri ntamuambia maiwaifu ni hiki...''2. Msichana wa kazi uliyemfukuza kwa kuwa na ujauzito tukagombana sana na nilikuita majina yote mabaya ni kwa kuwa nilikuwa najaribu kumlinda kwa kuwa sikuwa na uhakika kama hiyo mimba hainihusu kwa kuwa nimetembea naye miezi ile miwili uliyokwenda mafunzo south africa''.
  penye nyekundu weka Arusha.
   
 3. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Je ulimwambia haya uso kwa uso
  Au umeyaandika tu hapa ...??
   
 4. LD

  LD JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sawa baba nimekusikia, pole sana kwa tabia hizi mbaya zinazokuendesha mume wangu mpendwa. Sasa naomba nikuulize kaswali kadogo tu. Je unafikiria nini baada ya kujitambua na kuona hayo ufanyayo ni makosa mbele ya Mungu na wanadamu?
   
 5. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mmmmmmh kazi kwelikweli, na wake wenyewe wa .com haponi mtu hapo.
   
 6. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  LOh huzimiiiiiii?
   
 7. LD

  LD JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wakumwitu wanawake tuna mioyo ya nyama bwana, sio ya jiwe. Tunasamehe sana hata mara sabini.
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,789
  Likes Received: 416,597
  Trophy Points: 280
  nionavyo haya ni mikakati ya kumwacha mkeo na huna nia ya kujirekebisha kama ulivyobaini kwenye namba 9 hapo juu.
   
 9. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Mume wangu na mimi naungama kwa haya:
  1. Gauni la harusi yetu nilinunuliwa na boyfriend wangu Mjapani.
  2. Watoto wetu watatu, wa kwanza nilizaa na baba yako mzazi, wa pili nilizaa na kaka yako mkubwa na watatu nilizaa na shamba boy.
  3. Kile kitanda kilichovunjika siyo bahati mbaya ila siku ile bosi wako alipitia mchana kama kawaida yetu kufanyia mapenzi pale kitandani kwako, hivyo penzi lilivyozidi chaga za kitanda zikakatika vipande vipande.
  4. Lile gari jekundu siyo mkopo kutoka kazini bali nilipewa kama zawadi na mpenzi wangu wa siku nyingi RA.
  5. Niliposafiri kwenda Japan kikazi lile basi la abiria nililorudi nalo ni zawadi nilipewa na yule mpenzi wangu Mjapani.

  Kwa kuwe wewe uliungama dhambi 10 mimi makosa yangu ni machache sana yaani ni 5 tu. Natumaini ndoa yetu itakuwa ya furaha na upendo mwingi.
   
 10. neggirl

  neggirl JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 4,830
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mh... wapi mch/shehe aliyefungisha hii ndoa aongoze sala ya toba ...........lol
   
 11. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  inahuzunisha, inasikitisha na inatia hasira.
  Mungu na akusamehe bure ndugu yangu! Daaah, mkeo ana kazi aisee, manake huu ni zaid ya ubazazi.
   
 12. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu, mkeo alikusamehe kweli? Unaweza kuwa na nia nzuri ya kutubu kumbe ndio unampoteza zaidi mkeo maana anaweza kulipiza kisasi. Naamini ni bora kuzijutia wewe mwenyewe hizo zambi zako nakuacha kabisa uasherati.
   
 13. A

  Aine JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ee Mungu wangu nashindwa la kusema, nipe muda nilie weee hasira zikiisha nitakuwa na jibu!!
   
 14. Mvua Ya Kiangaz

  Mvua Ya Kiangaz JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Duh! huwa nafikiri mimi nina courage ya kuusema na kujua ukweli.......lakini hii ni kiboko.
   
 15. Mvua Ya Kiangaz

  Mvua Ya Kiangaz JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Duh! huwa nafikiri mimi nina courage ya kuusema na kujua ukweli.......lakini hii ni kiboko.

  These are two deadly confessions................hamna mtu yeyote wa karne hii ataweza kuukabili ukweli huu,kwa kuwa tumefanywa,tumeupokea na tunauishi uongo........kwa ukweli huu ni presha juu,kisukari na kifo tu,otherwise mioyo yenu wote ni yaa chuma.
   
 16. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Kama ni yule wa magamba nitakusamehe mke wangu.
   
 17. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Nikipata msamaha huu naahidi nitakuwa muumini mkubwa wa kanisa la kakobe.
   
 18. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  At least he had the guts to confess to his wife. The rest remains with the wife herself...
   
 19. D

  Derimto JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mamndenyi umemaliza kabisa na hapo ndipo utajua kuwa wanaume wana roho ya aina gani maana anaweza hata kukumwagia petrol akuchome moto
   
 20. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Kinachotia hasira kwenye hali kama hii pale mume anapodhani anaungama kwa mkewe mwema kumbe mke pia ni shetani, sasa hapo si bora wote mashetani mngekaa kimya. Mimi nimefanya uchunguzi wa kina na nimejilidhisha kuwa mke ni mwema ndio kilichonifikisha hapa.
   
Loading...