Condoleezza Rice: Kim Jong Un is pretty clever

Condoleezza Rice: Kim Jong Un is pretty clever

Mkuu Malcom Lumumba ndiyo maana mimi siku zote nimekuwa nikiamini kwamba South and North Korea ni projects zilizosukwa kimkakati. They agreed/decided to divide in order to advance and contain.
Haya mataifa yenye umri mkubwa (1000+ years) huwa wana akili zilizo beba maono ya mbali sana. Na mikakati yao ni kuvivusha na kuvijenga vizazi vyao siyo class fulani. Hivyo mataifa kama China, Kirea kusini na Kaskazini wanaweza kufanya lolote kwa ajili ya vizazi vyao.
Kuna series niliwahi pata kuiangalia kuna kakipande kadogo mno kwenye moja ya Episode kanaonyesha namna usiri mkuu uliopo baina ya mataifa haya ukikaangalia kwa akili nzuri utaina kuna mikakati ilishatengenezwa kabla hata hawajafarakana ni namna gani watakuja kuungana huko mbele. Na kuna watu wanahakikisha mgogoro unakua mkubwa kwa gharama yoyote ile lakini hii yote ni mbinu tu.
Korea Kaskazini ni mbeba msalaba lakini lastly hawa kuna kitu wanamchota mzungu.
Asante kwa andiko hili. Samahani, naomba nitajie jina la hiyo series. Asante.
 
Nakubaliana na wewe kaka na nategemea iwe kama ulivyosema,
Kuna kitu nimekiongezea hapo juu kiangalie.
Kinachoniegopesha ni kwamba nyakati zimebadilika sana tofauti na miaka ya nyuma.
Dunia imefungamanika sana kipindi hiki kuliko nyakati zozote zile katika historia ya binadamu.
Kitakachotokea Korea kule mbali kabisa kinauwezo mkubwa sana wa kutuathiri mimi na wewe kwa namna moja au nyingine

Upande wa pili,
Haya mataifa makubwa yanapenda kabisa hizi Korea ziungane tokea imepata Uhuru toka kwa Japani,
Lakini mwisho wa siku swali la Msingi linakuja "Hizi Korea zikishaungana ni kwa faida na hasara ya nani ??"
Linapokuja swali gumu kama hili ndiyo mambo mazito ya Balance of Power yanaingia hapa na wanaanza kuvutana tena.

Mfano Mzuri ni kwamba Bara la Ulaya mpaka leo wanapenda sana kuungana na kuwa nchi moja kaa ilivyokuwa kipindi cha Mfalme Justine au Mfalme Charlemagne wa dola Rumi. Wazungu wa Ulaya na akili zao zote walijaribu kufanya kila aina ya mbinu lakini mwisho wa siku ni Urusi na Marekani ndiyo kikwazo kwasababu wanajua Ulaya iliyoungana ni hatari sana kwa ushawishi wa Urusi na Marekani. Hivyo kila mtu anazuia huu muungano na pia anataka Bara la Ulaya liungane likiwa upande wake yeye binafsi.

Kina kipindi UN walipendekeza baadhi ya nchi kama Ujerumani, Brazil, India na AU wapewe kura za VETO kwenye Baraza la Ulinzi la Umoja wa Mataifa lakini taharuki ilikuwa kubwa sana. Swali ni hili: Je, kama Marekani na Urusi wana nia njema na ustawi wa mataifa na amani ya dunia kwanini wapinge kwa kiasi kikubwa wengine kuwa na VETO ??
Jibu ni rahisi tu, Ule mpango utavuruga BALANCE OF POWER Kwasababu mwaka 1972 walifanya jaribio la kumpa Uchina kura ya VETO badala ya nchi ya TAIWAN lakini leo wanajuta. Sasa wampe nchi nyingine kama Ujerumani lazima itakula kwao.

NB: Hoja nayotaka niiseme hapa ni kwamba haya mataifa makubwa hayafurahii ustawi wa hizi nchi nyingine huku yakiona maslahi yao yanaharibika. Marekani, Urusi na Uchina kama yanakubaliana na huu mjadala ni lazima basi yanapata maslahi ya moja kwa moja (Hakuna cha bure): maana tokea mwaka 1945 hadi leo Warusi, Wachina na Wamarekani wametupa mabilioni ya fedha nchi Korea (Kaskazini na Kusini) na wanajeshi wao wamekufa sana kwenye vita za Korea, ni lazima wanategemea kitu cha manufaa ya kiusalama au kibiashara.
Wakimpa mjerumani itakula kwao! Dah....it seems kuna maelezo mengi nyuma ambayo Mimi sijyajui. Ukipata muda naomba unijibu mkuu.
 
Mkuu Consigliere unakumbuka ule uzi wako kuhusu Korea Kaskazini ?
Uchina , Korea Kaskazini na Urusi wanataka wawaweke Korea Kusini na Marekani kwenye kikaango,
Huku akijua kabisa Marekani atafanya kila namna kujaribu kufanyia figisu Korea Kaskazini tena, hapo atapata kisingizio kwamba yeye alikubali mazungumzo na pila alikubali kwenye kwenye michezo ya Olympiki: Ana nia njema kabisa ya kumaliza huu mgogoro lakini Marekani hataki. Hii lazima itazua taharuki kwa wananchi kwa Korea Kusini kwasababu Marekani ataoneka dhahiri kabisa kwamba hataki suluhisho na anahatarisha maisha yao.

Huu mchezo wa Divide et Impera (Iron Wedge Diplomacy) ameitumia sana Urusi Barani Ulaya,
Kawafanyia Vurugu kule Ukraine na kajibebea Crimea lakini kwenye Minsk Agreement akaenda vizuri tu huku akisema yeye Wayukreini ni ndugu (Brethren) hivyo anapenda wakae chini wayamalize. Hapa Marekani alitengwa kabisa wakenda Maraisi wa Ufaransa, Belarus, Ukraine na Ujerumani. Mwisho wa siku Marekani juzi amekubali kuuizia silaha nzito (Lethal Weapons) nchi ya Ukraine kinyume kabisa na makubaliano ya Minsk na leo hii Marekani anaonekana Mkorofi mbela ya Jumuiya ya Kimataifa. (Very Clever Move; Exceptionally Clever)

Leo hii Bunge la Ulaya wanasema Marekani anahatarisha Usalama wa Ulaya kwa kumchokoza Urusi,
Marekani haaminiki sana Ulaya kama ilivyokuwa zamani na anaendelea kutengwa kila siku,
Nigel Farage juzi akasema ndani ya Bunge la Ulaya kwamba "When you poke the Russian Bear expect the reaction"

Sasa Korea Kaskazini kaiga huo mchezo,
Lakini mimi nagopa sana kwasababu tofauti kabisa na nchi ya Ukraine Marekani ana maslahi makubwa sana pale,
Ndiyo maana nikasema hayo mazungumzo yatamalizika vizuri endapo wahusika wakubwa (Uchina, Japan, Urusi na Marekani) Mbali na Korea zote kuhusishwa. Ufaransa, Ujerumani na Belarus walihusishwa kwenye Minsk Accord kwasababu wao wana maslahi ya moja kwa moja nchini Ukraine tofauti na Marekani.

NB: Korea Kusini na Japan ni masoko makubwa sana ya kibiashara ya Marekani pia ni eneo la kimkakati kwa Marekani kulinda The Western Hemisphere: Vivyo hivyo Uchina na Urusi wana maslahi ya moja kwa moja nchini Korea Kaskazini ndiyo maana nasema ili kuwe na amani pale kwenye Korean Peninsula ni lazima kuwe na Bilateral Agreement ambayo itahusisha minimum support or supervision kutoka nchi nyingine husika....

Marekani anapeleka Masilaha kule Ukraine kuwakomesha Ulaya na Urusi kwa kutotaka kumhusisha kwenye Mkataba wa Minsk anatuma ujumbe kwamba huwezi kupata suluhisho la amani bila yeye kuwepo.

Mfano mwingine hai kabisa,
Hata kule nchini Syria kama unakumbuka kwenye Astana Peace Talks walikaa Uturuki, Urusi na Iran halafu USA na Israel wakapigwa kapuni lakini mwisho wa siku umeona sasa Urusi na Syria wameshinda vita lakini Marekani na Isreal wamekataa kutoka nchini Syria na naskia wana mpango wa kukata kipande cha Syria na kutengeneza Kurdish State (Another USA client state in the middle east). Mpaka leo asubuhi nasikia U.S.A amepanga kutengeneza kikosi cha Wanajeshi 30000 wa Kikurdi ambao wengi wao ni wastaafu wa jeshi la Syria. Juzi wametuma drones zimelipua kambi ya Warusi, leo wanaweka wanajeshi kama 30000 kwenye mpaka wa Uturuki ambapo humo ndani kutakuwa na majamaa ya IDF, SIS, NAVY SEALS na Mercenaries wengine wenye silaha nzito.

Hivyo basi,
Tukiangalia haya mambo in a Realistic Point of view,
Huwezi kupata suluhisho la kisiasa la kudumu hapa duniani bila kuhusisha Urusi,USA na Uchina (Kwenye issue ya Korea) Hawa wawili ndiyo chanzo cha hii migogoro yote na vurugu zinazoendelea hapa duniani. Endapo utaweza kuwaweka hawa Simba Dume wawili kwenye zizi moja basi utaona amani ya kudumu nchini Korea na kwingineko duniani.

Kama CUBA mwaka 1962 na Ujerumani mwaka 1985 iliwezekana kwanini Korea 2018 Ishindikane kama wakiamua ???

CC: izzo , Dotworld , Bukyanagandi, ze kokuyo, Richard , SirChief , britanicca, Dragoon, Nalendwa, Maalim Shewedy
We jamaa ni kwikwi... Salute.
 
Inaitwa Iris, ina series nne. Angalia vizuri na kwa umakini ulio mkuu zile series mbili za mwanzo. Series mbili za mwisho (3 and 4) ni ziada, ni kwa ajili ya kuzubaisha akili za watu na kuwafuta majonzi tu.
Iris imefika serie 3&4!?..kilimo cha bangi kinaniweka bize sana!!..
 
Good to see you bro with this masterpiece. bless up
 
Hilo jina lako tu adabu huna si kila mtu anakaa kuangalia series mda wote jibu kwa adabu.
 
Nadhani wewe bado sana. Hujui hata kiswahili
Badala ya kuandika neno "ivoo" andika "hivyo"
Badala ya kuandika "sio" andika "siyo"
Elimu ya bure hiyo dogo.

I normally get annoyed to see these big mistakes in some of serious tabloids. See below:
1. Ndio instead of Ndiyo
2. Sio instead of siyo
3. Ivo instead of hivyo
4. Kua instead of kuwa
etc etc.
 
Kwahiyo unglyyyyyyyyyyy maana yake ni sura mbaya? Nimetafuta kwenye kamusi ya kingereza sijaona neno kama hilo "ungly" Acha kubisha wewe. Unatuaibisha vijana wa TZ
Kiingereza hicho huongea ndugu wa kabila fulani kutoka nchi jirani. God husema "Ngod" hamna shida ni lafudhi tu. Ukimsikiliza Mshona akiongea Kiingereza utafikiri ni kutoka Mkoa wa Mara, Tanzania. Hakuna shida mradi tu mtu asijifanye kuijua sana hiyo lugha. Hapo watu watamcheka. Umewahi kusikia Muitaliano akiongea Kiingereza ama Mchina ama Mjaluo au Mganda? Kwa mfano mimi hufurahia matamshi ya Kiingereza ya watu wa ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki. Hakuna shida ila usijifanye unaijua sana kama ni lugha yako. Wenyewe huwa hawapendi uongee kana kwamba ni kama wao. Hapana, wanapenda kuiona lafudhi yako ya Ghana, Nigeria, India ama Namibia. Cha msingi ukizungumza na kuandika lugha ya watu zingatia sarufi. Matamshi yako watu huyavumilia na tena huyafurahia.
 
Mkuu Palantir please read Post #19
Mkuu kwa strategy inayotumika USA yupo hali mbaya!. Lakini je NK hawaogopi ikibackfire maana naiona too risky kuharibu site zake na vinu vyake even if anaweza ficha lakini kuruhusu muungano kutapelekea achangamane na SK ambapo hata spies wa USA wataweza kuhusika kuharibu plan zake au kufichua secret millitary sites zake!.
 
Back
Top Bottom