YALIYOJIRI JANA KUHUSU KOREA KASKAZINI NA KUSINI:
Mkuu
Consigliere Salaam Kwako,
Kama nilivyosema hapo mwanzoni kwenye bandiko langu
#19 haya mazungumzo bila Marekani hayawezi kufika pazuri.
Jana tarehe 16 January 2017 Mawaziri wa mambo ya nje wa Mataifa 20 (Nchi zilizokuwa upande wa Korea Kusini kwenye vita ya Korea ya mwaka 1950-1953) wamekutana nchini Vancouver nchini Canada kwa ajili ya Majadiliano kuhusu kuiwekea vikwazo nchi ya Korea Kaskazini. Mazungumzo haya yameongozwa na serikali ya Marekani na Canada ambapo wamesema "Wanakubaliana na kuiongezea vikwazo Korea Kaskazini kwa ajili ya miradi yake ya silaha za Kinyuklia na mashambulizi ya kimtandao"
Juzi Korea Kaskazini aliwastua sana Mataifa ya Magharibi kwa kutaka makubaliano na Korea Kusini,
Hii ilipelekea hadi Raisi wa Marekani kusema kwamba anakubaliana na uamuzi huo lakini ni ubabe wake ndiyo umefanya Kim Jong-Un aogope. Walijibu vile kwasababu hawakutegemea huo uamuzi hivyo ilibidi waseme hivyo ili wasionekane ni wakorofi na hawataki suluhu. Lakini cha kushangaza ni kwamba jana tarehe 16 Waziri Lex Tillerson kasema kwamba Marekani inaamini kwamba haya mazungumzo ya amani baina ya Korea mbili hayawezi kufika popote mpaka kuwepo na msuluhishi anayeaminika. (A credible Mediator or Negotiator)
Hivyo basi,
Kuiongezea vikwazo Korea Kaskazini ndiyo njia pekee ya kuzorotesha mradi wao wa silaha za kinyuklia.
Ikumbukwe tayari Umoja wa Mataifa umeiwekea tayari vikwazo Korea Kaskazini na Uchina na Urusi walikubaliana navyo.
Kuongeza hivi vikwazo (Uni-lateral Sanctions)nje ya mkakati wa Umoja wa Kimataifa hakutaleta suluhu kabisa kwenye Korean Peninsula. Korea Kaskazini atazidi kuwa na vurugu na mwishowe atapewa silaha nzito zaidi kama ambavyo alipewa makombora haya ya masafa Marefu.
NB 1: Hiki kikao kina lengo moja kuu, "Kuvuruga mazungumzo yanayoendelea baina ya Korea mbili"
Hii inakuja kwasababu Marekani na Japan wanahisi hawajahusishwa wakati wao nao wana maslahi mazito nchini Korea kusini. Marekani kaona haya mazungumzo yakifanikiwa basi itamfanya yeye aonekane mkorofi pia jumuiya ya kimataifa italazimika kuiondolea vikwazo Korea Kaskazini ili kuchochea amani. Mwisho wa siku Korea Kaskazini itakutwa tayari imeshakuwa ni Nchi ya Kinyuklia na imefanikiwa sana kujijenga kijeshi kwasababu vikwazo vitakuwa havipo. Mfano Mzuri ni kinachoendelea nchini Iran, ambapo Raisi Rouhan alikubali mazungumzo ya amani na Marekani na mwishowe akaondolewa vikwazo huku akiahidi kutengeneza Mradi wa Nyuklia wa amani.
Kwa namna moja au nyingine,
Kama Iran imeondolewa vikwazo na imeruhusiwa kuwa na mpango wa Nyuklia wa amani basi ni dhahiri kwamba nchi ile bado itakuwa na wanasayansi wengi sana wa Kinyuklia: ambapo kama siku kunatoea uhitaji wa kutengeneza silaha za Kinyuklia watafanya kwa urahisi na haraka sana kutokana na uwepo wa rasilimali watu na rasilimali nyingine. Mpaka sasa Marekani na Israel wanajaribu kuvuruga huu Mkakati lakini inakuwa ngumu kwasababu Mataifa yote makubwa ya dunia yalihusishwa. European Union, United Nation Security Council na baadhi ya nchi za Kiarabu walikuwepo hivyo wakafikia mkataba ambao wa amani ambao ni ngumu kuuvunja bwana Donald Trump na Benjamin Netanyahu.
NB 2: Upande wa pili wa hoja,
Hiki kikao hakiwezi kuzaa matunda kwasababu Urusi na Uchina hawakuwepo.
Shirika la habari CNBC linasema hivi :
"
But the meeting will likely accomplish little, it said in an editorial. Diplomats say China's absence will limit what can be achieved, while North Korean leader Kim Jong Un has shown no sign of being willing to bow to pressure to give up weapons he sees as vital to his survival"
Hivyo bado tunarudi pale pale,
Hawa wazungu wasitegemee kabisa kumkomoa Korea-Kaskazini wakati uchina Urusi hawajahusishwa.
Wakiongeza vikwazo basi utawala wa Kim Jong-Un utaendelea kupewa masilaha mazito na kuingiziwa mafuta kutoka kwa nchi rafiki zake. Wakifanya Pacific Blockade ambapo wakaingia kwenye maji ya Bahari ya Korea Kaskazini au Territorial Waters kwa Manowari za Kivita, itakuwa ni kitendo cha kutafuta vita " An Act of War".
Au kama kweli wana nia ya kumuumiza Korea basi waziwekee vikwazo nchi zinazoifanya Korea-Kaskazini iendelee kudunda (Warusi na Wachina). Maana mtu mwenye akili timamu ni lazima atang'amua kwamba kwa jinsi ambavyo Korea-Kaskazini imetengwa ni lazima utawala wa
Kim Jong-Un ungekuwa umeshaanguka ndani ya miezi michache tu.
HITIMISHO:
Mwisho wa siku tunarudi pale pale,
Marekani, Urusi na Uchina wataendelea kuvutana na haya mazungumzo yanayoendelea hayatazaa matunda yoyote.
Lazima ifike mahali kila taifa litambue maslahi ya mwenzake ya Kiuchumi na Kiulinzi, ili kuweza kuwa na mazungumzo ya kudumu kwenye ule Ukanda. Mpaka sasa hivi Korea mbili haziwezi kuungana kirahisi lakini kinachotakiwa ni
The New Detante; kwamba haya mataifa yaache kutishiana vita na yashirikiane kwenye baadhi ya mambo ya msingi yatayogusa maisha ya Wakorea.
Marekani naye ni lazima akubali ukweli kwamba dunia imebadilika,
Ile dunia yake ya
UNI-POLARITY ya miaka ya 1991 hadi 2008 haiwezi kurudi tena.
Ili mambo yaende vizuri ni lazima kuwe na
Reciprocity,
Consensus ,
Consent and
Good Faith katika kiwango kikubwa. Hatuweza kupata amani ghafla, tunachohitaji ni Strategic Balance na Detante ili mambo yaende.
Tutaendelea kujuzana,
Young Malcom........
SOURCES:
1.
'Pressure campaign will continue,' Tillerson warns at North Korea summit in Vancouver | CBC News
2.
North Korea in the spotlight as Canada hosts summit on sanctions
3.
US & Canada-led summit wants more sanctions on N. Korea beyond the UN’s
4.
Iran Deal
CC:
mng'ato ,
Toyota escudo ,
Annael ,
zyogo ,
Nalendwa ,
ze kokuyo ,
SirChief,
Baazigar ,
gemmanuel265 ,
travis 1