Condoleezza Rice: Kim Jong Un is pretty clever

Condoleezza Rice: Kim Jong Un is pretty clever

Mkuu Consigliere unakumbuka ule uzi wako kuhusu Korea Kaskazini ?
Uchina , Korea Kaskazini na Urusi wanataka wawaweke Korea Kusini na Marekani kwenye kikaango,
Huku akijua kabisa Marekani atafanya kila namna kujaribu kufanyia figisu Korea Kaskazini tena, hapo atapata kisingizio kwamba yeye alikubali mazungumzo na pila alikubali kwenye kwenye michezo ya Olympiki: Ana nia njema kabisa ya kumaliza huu mgogoro lakini Marekani hataki. Hii lazima itazua taharuki kwa wananchi kwa Korea Kusini kwasababu Marekani ataoneka dhahiri kabisa kwamba hataki suluhisho na anahatarisha maisha yao.

Huu mchezo wa Divide et Impera (Iron Wedge Diplomacy) ameitumia sana Urusi Barani Ulaya,
Kawafanyia Vurugu kule Ukraine na kajibebea Crimea lakini kwenye Minsk Agreement akaenda vizuri tu huku akisema yeye Wayukreini ni ndugu (Brethren) hivyo anapenda wakae chini wayamalize. Hapa Marekani alitengwa kabisa wakenda Maraisi wa Ufaransa, Belarus, Ukraine na Ujerumani. Mwisho wa siku Marekani juzi amekubali kuuizia silaha nzito (Lethal Weapons) nchi ya Ukraine kinyume kabisa na makubaliano ya Minsk na leo hii Marekani anaonekana Mkorofi mbela ya Jumuiya ya Kimataifa. (Very Clever Move; Exceptionally Clever)

Leo hii Bunge la Ulaya wanasema Marekani anahatarisha Usalama wa Ulaya kwa kumchokoza Urusi,
Marekani haaminiki sana Ulaya kama ilivyokuwa zamani na anaendelea kutengwa kila siku,
Nigel Farage juzi akasema ndani ya Bunge la Ulaya kwamba "When you poke the Russian Bear expect the reaction"

Sasa Korea Kaskazini kaiga huo mchezo,
Lakini mimi nagopa sana kwasababu tofauti kabisa na nchi ya Ukraine Marekani ana maslahi makubwa sana pale,
Ndiyo maana nikasema hayo mazungumzo yatamalizika vizuri endapo wahusika wakubwa (Uchina, Japan, Urusi na Marekani) Mbali na Korea zote kuhusishwa. Ufaransa, Ujerumani na Belarus walihusishwa kwenye Minsk Accord kwasababu wao wana maslahi ya moja kwa moja nchini Ukraine tofauti na Marekani.

NB: Korea Kusini na Japan ni masoko makubwa sana ya kibiashara ya Marekani pia ni eneo la kimkakati kwa Marekani kulinda The Western Hemisphere: Vivyo hivyo Uchina na Urusi wana maslahi ya moja kwa moja nchini Korea Kaskazini ndiyo maana nasema ili kuwe na amani pale kwenye Korean Peninsula ni lazima kuwe na Bilateral Agreement ambayo itahusisha minimum support or supervision kutoka nchi nyingine husika....

Marekani anapeleka Masilaha kule Ukraine kuwakomesha Ulaya na Urusi kwa kutotaka kumhusisha kwenye Mkataba wa Minsk anatuma ujumbe kwamba huwezi kupata suluhisho la amani bila yeye kuwepo.

Mfano mwingine hai kabisa,
Hata kule nchini Syria kama unakumbuka kwenye Astana Peace Talks walikaa Uturuki, Urusi na Iran halafu USA na Israel wakapigwa kapuni lakini mwisho wa siku umeona sasa Urusi na Syria wameshinda vita lakini Marekani na Isreal wamekataa kutoka nchini Syria na naskia wana mpango wa kukata kipande cha Syria na kutengeneza Kurdish State (Another USA client state in the middle east). Mpaka leo asubuhi nasikia U.S.A amepanga kutengeneza kikosi cha Wanajeshi 30000 wa Kikurdi ambao wengi wao ni wastaafu wa jeshi la Syria. Juzi wametuma drones zimelipua kambi ya Warusi, leo wanaweka wanajeshi kama 30000 kwenye mpaka wa Uturuki ambapo humo ndani kutakuwa na majamaa ya IDF, SIS, NAVY SEALS na Mercenaries wengine wenye silaha nzito.

Hivyo basi,
Tukiangalia haya mambo in a Realistic Point of view,
Huwezi kupata suluhisho la kisiasa la kudumu hapa duniani bila kuhusisha Urusi,USA na Uchina (Kwenye issue ya Korea) Hawa wawili ndiyo chanzo cha hii migogoro yote na vurugu zinazoendelea hapa duniani. Endapo utaweza kuwaweka hawa Simba Dume wawili kwenye zizi moja basi utaona amani ya kudumu nchini Korea na kwingineko duniani.

Kama CUBA mwaka 1962 na Ujerumani mwaka 1985 iliwezekana kwanini Korea 2018 Ishindikane kama wakiamua ???
Mkuu heshima kwako aisee
 
Nakubaliana na wewe kaka na nategemea iwe kama ulivyosema,
Kuna kitu nimekiongezea hapo juu kiangalie.
Kinachoniegopesha ni kwamba nyakati zimebadilika sana tofauti na miaka ya nyuma.
Dunia imefungamanika sana kipindi hiki kuliko nyakati zozote zile katika historia ya binadamu.
Kitakachotokea Korea kule mbali kabisa kinauwezo mkubwa sana wa kutuathiri mimi na wewe kwa namna moja au nyingine

Upande wa pili,
Haya mataifa makubwa yanapenda kabisa hizi Korea ziungane tokea imepata Uhuru toka kwa Japani,
Lakini mwisho wa siku swali la Msingi linakuja "Hizi Korea zikishaungana ni kwa faida na hasara ya nani ??"
Linapokuja swali gumu kama hili ndiyo mambo mazito ya Balance of Power yanaingia hapa na wanaanza kuvuta tena.

Mfano Mzuri ni kwamba Bara la Ulaya mpaka leo wanapenda sana kuungana na kuwa nchi moja kaa ilivyokuwa kipindi cha Mfalme Justine au Mfalme Charlemagne wa dola Rumi. Wazungu wa Ulaya na akili zao zote walijaribu kufanya kila aina ya mbinu lakini mwisho wa siku ni Urusi na Marekani ndiyo kikwazo kwasababu wanajua Ulaya iliyoungana ni hatari sana kwa ushawishi wa Urusi na Marekani. Hivyo kila mtu anazuia huu muungano na pia anataka Bara la Ulaya liungane likiwa upande wake yeye binafsi.

Kina kipindi UN walipendekeza baadhi ya nchi kama Ujerumani, Brazil, India na AU wapewe kura za VETO kwenye Baraza la Ulinzi la Umoja wa Mataifa lakini taharuki ilikuwa kubwa sana. Swali ni hili: Je, kama Marekani na Urusi wana nia njema na ustawi wa mataifa na amani ya dunia kwanini wapinge kwa kiasi kikubwa wengine kuwa na VETO ??
Jibu ni rahisi tu, Ule mpango utavuruga BALANCE OF POWER Kwasababu mwaka 1972 walifanya jaribio la kumpa Uchina kura ya VETO badala ya nchi ya TAIWAN lakini leo wanajuta. Sasa wampe nchi nyingine kama Ujerumani lazima itakula kwao.

NB: Hoja nayotaka niiseme hapa ni kwamba haya mataifa makubwa hayafurahii ustawi wa hizi nchi nyingine huku yakiona maslahi yao yanaharibika. Marekani, Urusi na Uchina kama yanakubaliana na huu mjadala ni lazima basi yanapata maslahi ya moja kwa moja (Hakuna cha bure): maana tokea mwaka 1945 hadi leo Warusi, Wachina na Wamarekani wametupa mabilioni ya fedha nchi Korea (Kaskazini na Kusini) na wanajeshi wao wamekufa sana kwenye vita za Korea, ni lazima wanategemea kitu cha manufaa ya kiusalama au kibiashara.
Duh, Kweli dunia yabadilika sana. Inaonekana Japani alikuwa mbabe mno zamani, alizitawala Korea zote 2 na China yao, lakini leo amekuwa wa kupitishiwa makombora juu ya kichwa chake na Kim!
 
Duh, Kweli dunia yabadilika sana. Inaonekana Japani alikuwa mbabe mno zamani, alizitawala Korea zote 2 na China yao, lakini leo amekuwa wa kupitishiwa makombora juu ya kichwa chake na Kim!
Japani walikuwa makatili vilevile na waliipiga urusi 1905 lkn si unajua makubaliano waliingia baada ya WWII kwenye mambo ya kijeshi?
 
Duh, Kweli dunia yabadilika sana. Inaonekana Japani alikuwa mbabe mno zamani, alizitawala Korea zote 2 na China yao, lakini leo amekuwa wa kupitishiwa makombora juu ya kichwa chake na Kim!
Nikikumbuka KAMIKAZE STYLE hua nawakubali sana waJapan.
 
Yule mama mrembo ndio kachoka hivyo. Kweli kuna vitu vichache huwezi kushindana navyo wakati ni mojawapo. Samahani kwa kuwa nje ya mada.


Kama kweli ulikuwa unamuona Condoleezza mrembo siku za nyuma basi unahitaji miwani.
 
Duh, Kweli dunia yabadilika sana. Inaonekana Japani alikuwa mbabe mno zamani, alizitawala Korea zote 2 na China yao, lakini leo amekuwa wa kupitishiwa makombora juu ya kichwa chake na Kim!
Mambo yanabadilika sana mkuu.
 
Siku akiolewa ndo atarudi kwenye form mkuu!

Mimi msimamo wangu ni sawa na ule wa "BOB Marley" kwamba hakunaga mwanamke mbaya.
Tena hawa weusi ndiyo wazuri wacha kabisa; mbali na sura mwanamke ana vitu hatari ambavyo mimi huwa naangalia.
 
lakini ujumbe umefika si ndio. Kwanza unauwakika gani mm mtanzania au laa? As long as message sent and delivered thats what matters, grammatical errors potezea
wewe nae kaa kimya bana umekosea kuandika ngeli unaanza leta ngonjera za sio mbongo!..
Hebu rudi kwenye mada kama huna point tulia tusome watu wenye mantiki!.
 
Back
Top Bottom