Condester Sichalwe Apongeza Ongezeko la Bajeti Wizara ya Kilimo

Condester Sichalwe Apongeza Ongezeko la Bajeti Wizara ya Kilimo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,428

CONDESTER SICHALWE APONGEZA ONGEZEKO LA BAJETI WIZARA YA KILIMO

Mbunge wa jimbo la Momba Condester Michael Sichalwe ameitazama bajeti ya wizara ya kilimo kama mkombozi kwa wakulima wa mahindi na mpunga kwa kuwa itasaidia kupata Masoko ya nje ambapo pia imeitaka serikali kuhakikisha inatokomeza kabisa kilimo cha mkono.

Bunge limeidhinisha jumla ya kiasi cha Shilingi 1,242,975,075,000 katika mwaka 2025/2026 ili kuiwezesha Wizara ya Kilimo kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ambayo inalenga kuongeza ukuaji wa Sekta ya Kilimo.

Bajeti itatekeleza vipaumbele ambavyo ni kuongeza tija na uzalishaji; kuchangia kuongeza ajira zenye staha na ushiriki wa vijana na wanawake kwenye kilimo; kuimarisha usalama wa chakula na lishe, kuimarisha upatikanaji wa masoko, mitaji na mauzo ya mazao nje ya nchi; kuimarisha maendeleo ya ushirika pamoja na kuimarisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika uendelezaji wa Sekta ya Kilimo.

#BajetiYaWakulima
#BajetiYaWakulima2025/2026
#TwenzetuShambani
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2025-05-23 at 15.25.49.mp4
    31.7 MB
Back
Top Bottom