Comrade Mugabe Arejea Zimbabwe Akiwa Na Afya

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
ImageUploadedByJamiiForums1453551373.634147.jpg

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alirudi nyumbani Ijumaa usiku kutoka likizo yake ya kila mwaka akiwa katika hali nzuri ya afya,na akamaliza uvumi kuwa yeye alikuwa amepata ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Gazeti la Herald siku ya Jumamosi (Leo) walichapisha picha za Mugabe akiwasili katika uwanja wa ndege wa Harare International Airport ambapo alikuwa ameandamana na mkewe Grace, binti Bona na mume wake na viongozi waandamizi wa serikali.
 
Kwenye dunia hii kuna watu ni exceptional ,huyu jamaa hata afanye nini bado wananchi wake wanampenda
Long live Comrade
 
Hivi huyu mzee mbona asiamue kuishi maisha mengine nje ya siasa hasa kutokana na umri wake?
 
Nafikiri yeye mwenyewe alishawahi kulitolea ufafanuzi Hilo Swali lako. Alisema wanaomuhoji wote juu ya umri wake madarakani Mbona hawamuulizi Hilo Swali Malkia Elizabeth II !?
 
Nakumbuka ni kweli kuwa aliwajibu vile waandishi wa uingereza lakini kuna vitu vya kuangalia, Malkia Elizabeth ni ceremonial leader tofauti na Mugabe, pia tofauti akumbuke katika Zimbabwe hakuna mfumo wa kifalme tofauti na Uingereza. Ukiyakubali hayo majibu hayo ya Mugabe yanapoteza mantiki
 
Well, Wananchi wake wanamuona Kama Mfalme then who are we (outsiders) to judge mkuu!!?? Tata Mugabe kwa Wazim huwaambii kitu.
 
Sikatai ils bila kujalisha kuwa ni kweli huwa anashinda au at times wizi pia unatumika, ni kwa nini kwa umri huu asimue tu akae pembeni ili wengine pia wafanye kazi?
 
Umeshawahi kuonja madaraka mkuu!? Hata kuwa Class Prefect !! Madaraka yana utamu wake haswa kwenye level Kama ya Tata Mugabe. Almost maisha yake yote ametumia akiwa madarakani. Kuna ving'ora na perks kibao katika nafasi yake. Kwa hiyo inafikia muda hata yeye Mugabe anaingiwa na Uwoga ( fear of the unknown) kwamba maisha yanakuwaje hapo mbeleni endapo nitaachia haya madaraka na huu "utamu" wote.
 
Huyu mzee yupo na miaka zaidi ya tisini lakini bado yupo gado,sijui anakula chakula gani huyu,live long Mugabe
 
View attachment 318753
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alirudi nyumbani Ijumaa usiku kutoka likizo yake ya kila mwaka akiwa katika hali nzuri ya afya,na akamaliza uvumi kuwa yeye alikuwa amepata ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Gazeti la Herald siku ya Jumamosi (Leo) walichapisha picha za Mugabe akiwasili katika uwanja wa ndege wa Harare International Airport ambapo alikuwa ameandamana na mkewe Grace, binti Bona na mume wake na viongozi waandamizi wa serikali.
Fazaaaaaa
 
Back
Top Bottom