Computer eng. V/S Telecom eng.

Naona Dogo wanamchanganya sana watu hapa, masikini weee. Imebidi nirudi nimsaidie.

Kijana, kwenye haya madudu, mie si mtaalam sana ila nafahamu mgawanyiko wake ulivyo.

Kwenye Computer kuna Hardware na Software.

Hardware: Hii hujumlisha wale watu wanaunda Computer (Assemble) na ku-design vitu hizo Integrated parts za Computer kama CPU, RAM, Graphic cards etc. Hizi wala usipoteze muda kuzisoma maana milele hutakuja ukae uwe mtengenezaji. Wamezishika sana watu kama akina Intel, AMD, ASSUS, nk. Sanasana wee utabaki kuwa MUUNDAJI tu. Kwa nchi duniani, ni USA, Taiwan, Malaysia, Thailand, Hong Kong na wengine kadhaa ila mama lao ni Thaiwan.

Software: Hizi nazo zimegawanyika kwenye sehemu kama TATU hivi ingawa kuna kitengo zinakuwa kama mbili-
1. Watengeneza Programing na baadaye kuziuza program zao. Hawa ndiyo watu kama akina Oracle, Microsoft, Norton nk.
2. Wanaosomea hizo program zilizonunuliwa hapo juu na kufundisha watu wengine. Wakati mwingine wanatumia utundu wao wa kuzaliwa na kuleta matumizi fulani ya hizo program ambayo hata wale jamaa wa juu hawakufikiria.
3. Watumiaji wa kawaida ambao inabidi wafundishwe na watu wa pili au wa kwanza kwa ajili ya kazi zao.

Mtu wa pili na wa kwanza wanaweza wote kuwa wamesomea IT. Anaweza kuwa mtu yuleyule kaandika program na kuwafundisha watu jinsi inavyofanya kazi. Katika hizo program, zinapishana sana na kuna zile rahisi ambayo hata wewe leo hii unatakiwa kuwa unaweza kuifanya. Kwa mfano unatengeneza kiprogram cha ku-solve quadratic equation.

Umuhimu wa watu waliosomea IT ni kuwa wanakuwa wameshaweka Msahafu wa Computer kichwani na hii inawasaidia kuwa flexible kwenye field tofauti. Kwa mfano, wanakuja watu wa Muhimbili wanataka kutengeneza kifaa cha kipimo fulani na jamaa wanakaa na Madaktari, kusikia jinsi utaratibu ulivyo na wanatoka na kifaa kilichokuwa na program ya kufanya hivyo. Kesho watakuja watu wa madini wanataka kifaa cha kupimia udongo wenye dhahabu/almasi nk. Wanakaa nao na kujadili jinsi utaratibu wao ulivyo na jamaa wanakuja na kifaa/program ya kupima.

Nilishashuhudia Prof. mmoja aliyekuwa amebobea kwenye somo la Theory of Elasticity and Plasticity alienda USA na kufanya kazi hospital pamja na Madktari na wakali wa IT. Wali-design taya la binadamu bandia. Hapa, Madaktari walianza kwa kuweka jinsi taya linavyofanya kazi. Prof. huyo juu alikuja na kuweka Model nzima ya taya na kutafuta kila sehemu ya taya iwe na Strength kubwa kiasi gani. Watu wa IT ndipo wakaingia sasa na kuchanganya walivyosema Madaktari na huyu Prof. mhandisi. Mwisho wakaja na taya zima lililotengenezwa kwa ushirikiano wao wote.

Ukisomea IT unakuwa kama Mpishi mzuri sana anayejua kupika karibu vyakula vyote duniani. Utaweza kupika chakula kizuri popote pale duniani hata kama huna baadhi ya viungo au vyakula.

Baadhi ya vyuo wanadanganya kuwa wanafundisha hiki au kile ila ukweli wanafundisha kitu kilekile na wengi wao kwa ufupi wanafundisha ELECTRONICS ambayo inahusisha hivi vitu vyote.
Ndiyo maana nikasema hakuna kitu kama Computer Engineering. Wewe kama wataka kuwa Mchezea pote, basi soma Electronics Engineer maana utakuwa na uelewa kila sehemu kidogo. Ukitaka kuwa mtengeneza program basi nenda kwenye IT ila huko, unaweza kujifunza kuunda Computer kwa muda wako maana hakuna mtu atakufundisha. Ila kuna baadhi ya shule sasa wanafundisha baadhi ya field moja kwa moja na IT yake. Kwa mfano unaweza ukasomea kitu kinaitwa Computerised Economics ambapo unasoma Uchumi na IT. Nafikiri pia kuwa ujenzi na IT, Uganga na IT, nk na hawa wanakuwa wakali wa IT ila wamebobea kwenye field zao moja kwa moja yaani anakuwa Mhandisi na mtu mwenye ujuzi wa IT au Mganga na ujuzi wa IT.

Telecominication ni somo lenye future nzuri sana maana kila siku vifaa vinakuwa vingi sana na sidhani itafika sehemu watu wakose kazi. Hili halihitaji sana maelezo.

Jambo la muhimu ni kukumbuka kuwa ukiwa CHUO KIKUU, baadhi ya mambo jisomee mwenyewe na usisubiri mtu akufundishe. Usisome ili upass mitihani bali soma ili yakusaidie huko mbele ya safari au kwa faida yako mwenyewe. Kuandika ukurasa wa WWW, hakuna atakayefundisha ila kama umesoma IT, basi utajisomea wewe mwenyewe na maadam una msingi mzuri, utaelewa na kuwa na uwezowa kutengeneza WWW yako mwenyewe. Computer ikiharibika, kubadili RAM, HDD, sijui CPU, utajifunza mwenyewe na mwisho unakuja kuweka data sawa kwenye BIOS na mtambo unafana kazi.

KILA LA KHERI.
Mkuu umeua hapa
 
duu so TCU inatuma vilaza St. Joseph?
matokeo yangu ya 6 yanawazd baadh ya wana COET.

St Joseph mpo chini ya NACTE na si TCU na bado hamjafika kamba ndefu. Nyinyi ni chuo cha tech sio chuo kikuu. Kuhusu coet sijui lakini nina uhakika hukua na pass za kwenda Coict kusoma telecom au comp eng. that is.. ungekuwa nazo lazima ungeenda kusoma COIct kwenye vipanga wa elimu nchini.. Hii haimaanishi ukifeli basi kila kitu kitakoma.Hapana. Wapo waliofanikiwa hapo DIT au St Jose. Kifupi ni Juhudi zako kila Ngazi ndio zitakuweka mjini. Aksante Pax
 
kama unataka kuja kuwa na pesa kijana na uwanja mkubwa wa kujiajiri soma CIVIL. kama unafikiria usharobaro na utozi nenda huko........
 
Computer scientist anatengeza software package kama ile ya CRDB Bank. Information Technology specialist anaitumia ile package kufanya kaz na ICT inamsaidia consumer kupata huduma katika ile package.

i.e
database admin -computer science
data admin -IT specialist
Consumer au end user ndo ICT Knowleged.

Hamna cha computer science,IT na ICT utofauti wake jina tu nakwambia tena umespma computer science ila bado ni mburula hata window yenyewe ku install shida hiyo configuration ya switch itakuwaje.Watu waliosoma hyo computer science wengi halafu some of them hamna kitu.Mi nakushauri dogo kama unataka kusoma kozi ambayo unaona ni nzuri kasome BE.Engneering in computer engineering and Information Technology hapo utakuwa umeula wangu utakuwa different from sisi tuliyo soma Computer science,ICT, na IT reall nna experice ya hyo computer science ambayo wengi wao ni wakawaida sana tena wali waliosoma kule songea duh hii noma mara mbili nimekutana nao maeneo makubwa kwnye project nkiwa na diploma yangu ya ICT-BUSINESS wao second year halafu computer science dah aibu kwelikweli.So unaposoma kitu soma uwe na ujuzi wake sio yaishie kwenye daftari kama na computer science yako unashindwa ku configure hyo switch na router cabinet unategemea nininn
comms_cabinet.jpg
 
Nakushauri anza na computer science kama utaendelea na masters ndo uje uende kwenye comp eng...
Mie nasoma computer science nategemea kuhtimu mwakan then km ntafanikiwa ndoto yangu ya kwenda MIT(massachussets institute of Technology) ntasoma comp eng.

Raha ipo ktk comptr science unaweza kuwa:-
1. Hadware expert
2. Software engineer/expert
3. Database administrator
4. Network administrator
5. Communication

Unaposema compyuta sayansi lazima uyasome hayo mambo matano na utakuwa na idea nayo yote ila utaamua lipi kati ya hayo liwe ndo utaalamu wako.
Karibu St. Joseph Inst of Info Tech.

Ulifanikiwa kwenda MIT kaka
 
Nakushauri anza na computer science kama utaendelea na masters ndo uje uende kwenye comp eng...
Mie nasoma computer science nategemea kuhtimu mwakan then km ntafanikiwa ndoto yangu ya kwenda MIT(massachussets institute of Technology) ntasoma comp eng.

Raha ipo ktk comptr science unaweza kuwa:-
1. Hadware expert
2. Software engineer/expert
3. Database administrator
4. Network administrator
5. Communication

Unaposema compyuta sayansi lazima uyasome hayo mambo matano na utakuwa na idea nayo yote ila utaamua lipi kati ya hayo liwe ndo utaalamu wako.
Karibu St. Joseph Inst of Info Tech.

Dan, namie najuta kwanini sikusoma Computer Science ya miaka mitatu.
Sasa hivi ningelikua mbali kuliko hapa nilipo.
 
Hahaha nami ningependa atupe mrejesho


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom