Comoro Island

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
843
VISIWA VYA COMORO,NI ENEO LA VISIWA VILIVYO TOKANA NA MATUMBAWE.

Na.Comred Mbwana Allyamtu
Friday -11/1/2018

Comoro ni muunganiko wa visiwa vitatu, na ni nchi ya jamuhuri ya muungano wa visiwa vya Comoro (Union Republic of Comoro Island), Jina la taifa hilo limetokana na lugha ya Kiarabu inayopatikana kwenye kitabu kitakatifu cha Quran ndani ya Juzur al-Qamar (جزر القمر) ikinamaanisha "visiwa vya mwezi".

Comoro ina visiwa vitatu vikubwa ambavyo ni Grande Comore (Ngazidja), Anjouan (Nzwani) na Moheli (Mwali). Kisiwa cha Mayotte si sehemu ya visiwa vya jamuhuri ya Comoro, lakini kijiografia na kihistoria ilikuwa sehemu ya visiwa vya Comoro, kisiwa cha Mayotte kisiasa ni sehemu ya Ufaransa kwa sababu wakati wa uhuru watu wa Mayotte walipiga kura nyingi karibu 73% ya kusalia chini ya himaya ya Ufaransa, Japo kuwa Comoro inadai kuwa visiwa vya Mayotte ni sehemu ya eneo lake.

Visiwa vya Comoro vilipata uhuru mwaka 1975, baada ya kura ya maoni ya kujitenga na Ufaransa (Referandum of independence) iliyofanyika mwaka 1974, mji wake mkuu ni Moroni, Visiwa vya Comoro vina ukubwa wa karibu 2,034 km2, huku idadi ya raia wake ni 1,000,000 kwa mujibu wa census ya mwaka 2016, Visiwa hivyo hupatikana katika bahari ya Indian, katika eneo la Afrika Mashariki.Visiwa hivi vipo karibu na nchi ya Madagascar, Sarafu ya pesa yao huitwa "Comorian franc" (KMF), na lugha rasmi ni kicomorian, French, kiswahili na kiarabic.

Mliman mrefu katika Visiwa hivyo ni Mlima wa Karthala, ni Mlima wa volcano hai (an active volcano) na una urefu wa mita 2,361. Ni mlima unaofuka kila mara, umekuwa ukifuka volcano zaidi ya mara 20 kwa karne hii ya 19.

Visiwa vya Comoro ni moja ya visiwa vilivyo tengenezwa kwa mabaki mengi ya viumbe wa bahari, yani matumbawe huku Ikiwa moja ya eneo wanapopatikana viumbe wengi wa baharini. (one of the world’s largest coral atolls which parades hundreds of fish species, shells and corals with great chances of seeing large turtles, manta rays, marline and whale sharks)

Mapema mwaka 1974 kura ya maoni iliitishwa juu ya visiwa hivyo kupatiwa uhuru kutoka Ufaransa, katika kura hiyo 95% walipiga kura ya kutaka uhuru,(voted for independence). Kutoa kisiwa cha Mayotte pekee ndio kilipiga kura ya kubakia kuwa eneo la Ufaransa.

Ikumbukwe kuwa kisiwa cha Mayotte kina idadi kubwa ya waumini wa kikiristo ndio maana ilikuwa rahisi kuchagua kubaki kuwa sehemu ya Ufaransa, huku Visiwa vingine vikiwa na waumini wengi wa dini ya uislam, uhuru kamili ulipatikana July 6 1975. Nchini Comoro uislam ndio dini ya nchi huku uislam wa dhehebu la Sunni ukichukua karibu 98%, alafu Roman Catholic 2% tu.

Rais wa kwanza wa Comoro aliitwa Ahmed Abdullah Abderemane, ambae alizaliwa katika eneo la Domoni, kwenye kisiwa cha Anjouan mwaka 1919. Alikuwa rais wa kwanza mara baada ya uhuru wa Comoro mapema mwaka 1975, Lakin baadae alikumbwa na mapinduzi kadhaa Kabla ya yale mapinduzi yaliyo pelekea kuuwawa kwake kwa kupingwa risasi akiwa ikulu mjini Moroni siku ya ijumaa ya tarehe 26th November 1989, ambapo mapinduzi hayo yalitekelezwa na Bob Denard na Said Mohammed Djohar kufatia mgogoro wa kisiasa baina ya Ahmed Abderemane na Bob Denard.

Kimsingi Visiwa vya Comoro vimekaliwa na watu mbalimbali kutoka Afrika na Asia Kusini. Wanaakiolojia walitambua mabaki ya makazi ya watu kutoka karne ya 6 kwenye kisiwa cha Nzwani lakini haijulikani kama watu walitangulia kufika mapema bila kuacha mabaki ya kutambulika. Waswahili wa kwanza walifika kisiwani humo wakiwa ni sehemu ya Wabantu toka tangu karne ya 9 BK. Kipindi cha kwanza kufika kwao waswahili huitwa kipindi cha Dembeni kuanzia karne ya 9 mpaka karne ya 10, ambako Waswahili walianzisha kijiji kimoja katika kila kisiwa.

Wakati wa karne ya 11 hadi ya 15 biashara iliongezeka kwa watu kutoka Madagaska kuwasili kisiwani humo, pia na wafanyabiashara kutoka Uarabuni walianza kuwasili katika visiwa vya Comoro, Vijiji vidogo vikaongezeka na vijiji vya awali vikakua vikawa miji. Kumbukumbu ya wenyeji hutaja mara nyingi majina ya Waarabu kutoka Yemen na maeneo ya Oman kama mababu wa koo asilia lakini hakuna uhakika kama kumbukumbu hizo zinalingana na historia halisi.

Athira ya Kiarabu na ya Kiislamu ikaongezeka kutokana na biashara ya watumwa, dhahabu na pembe za ndovu kati ya Afrika ya Mashariki na nchi za Kiarabu. Waarabu na Waajemi walijenga vituo kwa ajili ya biashara yao pamoja na misikiti na kueneza dini ya Uislamu kwenye visiwa hivyo. Kutanuka kwa tamaduni za kiarabu kuliifanya Comoro kuwa taifa lenye misingi ya kislam kwa muda mrefu. Hata hivyo kufuatana na katiba ya uhuru ya mwaka 1975 Comoro ilitangazwa kuwa jamhuri ya Kiislamu.

Baada ya uhuru serikali za awali zilipinduliwa mara kwa mara, na wanajeshi au na mamluki wa koloni lake la zamani Ufaransa, Katiba mpya ya mwaka 2001 iliondoa kipengere cha kidini ndani ya dola na iliunda utaratibu wa urais kuzunguka kati ya visiwa vitatu vikubwa, nchini humo. Katika muundo huo rais wa jamhuri ya Comoro atateuliwa kila baada ya miaka minne kutoka kisiwa tofauti.

Katika uchaguzi ya mwaka 2002 rais Azali Assoumani alichaguliwa kutoka kisiwa cha Ngazidja (yani Comoro Kuu), pia katika uchaguzi mkuu wa 2006 rais alichaguliwa kutoka katika kisiwa cha Anjouan. Wananchi wa Anjouan walitoa rais wa jamuhuri kwa mara ya kwanza toka uhuru wa visiwa hivyo. Kwa mujibu wa katiba ya Comoro, imewaka mashariti kwamba "Kila kisiwa kitateuwa mgombea mmoja atakae patikana kutoka kwa wagombea wenye kura nyingi, kwenye kila kisiwa kisha wagombea hao watatu kutoka kwenye kila kisiwa ambao wamepata kura nyingi Kutoka kwenye kila kisiwa watagombea urais wa jamuhuri kwa kusimamishwa mbele ya wapiga kura wa visiwa vyote ambao wao watamchagua rais mmoja wa jamhuri".

Rais wa mwaka 2010 alitoka katika kisiwa cha Moheli, baadaye tena rais kutoka kisiwani Ngazidja, Katika uchaguzi wa 2010 ulivunja rekodi kwani bwana Ikililou Dhoinine alipata kura kuliko wagombea wote katika historia ya visiwa hivyo, alipata ushindi wa 100% ya kura zote.

Hii ndio Comoro eneo la visiwa vilivyo undwa kutokana na mabaki ya matumbawe na sehemu ya volcano kulipuka miaka mingi huko nyuma.

Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
FB_IMG_1557210579858.jpeg
FB_IMG_1557210589491.jpeg
 
It is a wonder hawa jamaa wanazungumza Kiswahili safi sana kama cha Zanzibar!

Aisee dunia ni very fun!
 
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.comView attachment 1090193View attachment 1090194
Huu ndio utamu wa Jamiiforums buana, unakula hadi kusaza.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom