Commission for mediation and arbitration (CMA), taasisi nyeti inayodharauliwa

MYAO WA KASKAZINI

Senior Member
Aug 10, 2015
133
59
Ndugu wana Jamvi,

Kwanza nisikitike kwamba kuna baadhi ya watu wana mambo mazuri sana vichwani mwao wangetaka kuyazungumza kwa ajili ya maendeleo ya Taifa lao, lakni kwa sababu moja ama nyingine, wanakosa forum sahihi za kusemea mambo muhimu. Ndiyo sababu kwa Wakili Mgeni kama mimi, nimeamua kukimbilia JF ili kusudi nipate kusema machache kuhusu Mahakama yetu ya Kazi, yaani CMA.

CMA ilianzishwa kwa nia na madhumuni ya kutatua migogoro mbalimbali ya kazi ambayo inatokea baina ya Mwajiri na Mwajiriwa. Ina Makao yake Makuu pale jengo la Idara ya Kazi Mkoa wa Dar es Salaam na ina ofisi karibu kila mkoa wa Tanzania.

Kazi kubwa ya chombo hiki ni kusuluhisha na kuamua migogoro yote ya kazi ambayo inapelekwa pale.

Cha kushangaza, ni kwamba ofisi za CMA zina hali mbaya kuliko pengine ofisi nyingine za serikali ambazo zinajulikana hapa Tanzania.

Ubaya wa ofisi za CMA unatokana na mapungufu yafuatayo:

(1) Ni ukosefu wa vitendea kazi. Ni aibu kubwa sana kufika kwenye ofisi ya CMA Makao Makuu na kuambiwa kwamba hakuna majalada ya kufungulia kesi. Hali hiyo nimeikuta Geita, Shinyanga, Njombe na Mtwara. Pale Shinyanga kwa mfano, walimwambia Mlalamikaji ambae n mteja wangu kununua jalada la kuja nalo ili documents zake zisiwe uchi, ziwe kwenye cover. Hii ni aibu kwa taasisi kubwa na ya Muhimu kama hii.

(2) Mara nyingi sana, ofisi za CMA karibu zote, kuanzia Makao Makuu mpaka mikoani, wanakosa wino kwa ajili ya ku print Tuzo za Mahakama. Hili linasababisha kesi kuchelewa kwa sababu hakuna wino wa printer.

(3) OFISI NYINGI ZA CMA HAZINA KARATASI NA STATIONERIES KWA UJUMLA WAKE.
Ndugu wanajamvi, hivi kweli ofisi kubwa na nyeti kama CMA ikose karatasi kwa ajili ya kutolea maamuzi, hivi inajiendeshaje. Nilibahatika kwenda Bukoba Mwaka huu, nikakutana na kijana mmoja pale, anaonekana kuchoooka vibaya sana, akaniambia kwa bahati mbaya ofisi yangu haina karatasi za kukutolea Uamuzi wako. Yaani nilimwonea huruma ikabidi niende kununua ream moja nimpe. Sina uhakika kama zikiisha atapata msamaria mwema wa kununua ama la.

(4) Maafisa wa CMA hasa Makao Makuu wanajisikia sana. Kuna baadhi ya mahakimu wa pale wana dharau sana na kauli zao siyo nzuri. Hii ni kwa sababu wamekaa sana pale Makao Makuu kiasi kwamba wanapaona kama ndiyo nyumbani kwao na hakuna wa kuwafanya kitu. Ahsante kwa Kaimu Mkurugenzi ameanza kuwabadilisha tabia na wanaanza kunyooka sasa. Ila tunamshauri Mkurugenzi awahamishe baadhi ya watumishi hapo makao Makuu na kuwasogeza hata Kibaha kwani wanafanya mambo ndiyo siyo.

(5) Ofisi ya CMA imeshindwa kuwa Huru kama ambavyo Standing Orders imetamka. Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ni idara huru ya serikali. lakini hata hivyo, inaonekana wazi kwamba siyo huru kama ambavyo inasemekana. Inaonekana baadhi ya viongozi wanaiingilia sana.

Idara nyingine huru za serikali zina scheme of service zake, salary scale zake, zina majengo yake, zina vitendea kazi vyake, na wafanyakazi wake ambao ni huru. hata hivyo, CMA inaonekana kutokuwa huru kwa sababu bado ipo chini ya Idara ya Kazi (hata kama wadau watakuja na kusema hapana, lakini uhalisia ndio huo), pale ilipo Idara ya Kazi basi na CMA ipo hapo hapo kiasi kwamba wadau wanashindwa kutofautisha kati ya Idara ya kazi na CMA, wanasema tunaenda leba, peleka malalamiko yako leba; wakifika pale kama akitangulia kuingia Leba basi, ujue hiyo kesi mpaka ifike CMA itakuwa nje ya muda, labda kama Afisa wa kazi ni mwadilifu, lakini kama la, basi ujue kwamba itafanyiwa kazi huko huko na kama ikifika CMA jua ipo nje ya muda; katibu Mkuu wa Wizara anaonekana kuwa na chuki na baadhi ya watu ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu aliyestaafu.....hili lilisababisha CMA kukosa mambo mengi sana.

Uhuru huo imefika pahala nasikia mpaka RPC anaingilia kesi kwa kumwamrisha Muamuzi aamue kesi fulani ndani ya muda fulani (Nasikia hilo limetokea Arusha). Mkuu wa Mkoa anatoa amri, CMA fanyeni hivi, hatuendi wala hatufiki kwa mtindo huo.

Umefika wakati sasa CMA kuwa na majengo yake, kuwa na ofisi zake, kuwa na vitendea kazi zake na pia magari yake kama zilivyo mahakama kwa ajili ya kurahishisha utendaji kazi.

(6) Ofisi za CMA hazina wafanyakazi wa kutosha. Utakuta ofisi kama Njombe, kuna maafisa wawili, wao ndo wafagizi, wachapaji, wasuluhishi na waamuzi. Ni vema kazi za hawa wajamaa zikaheshimiwa. Ofisa anatoka alikotoka na suti yake, lakini akifika kwa ofisi anakutana na vumbi hivyo inambidi afagie kwanza, hata ile hamu ya kuvaa suti baada ya hapo inatoweka. CMA waajiri wafanyakazi wa kada za makarani na wasaidizi wa ofisi ili kurahisisha kazi hizo.

(7) Nilishangaa sana nilipopewa Uamuzi na baada ya muda nikarudi kukazia hukumu, nikaambiwa kwamba CMA haina mamlaka ya kukazia hukumu. Hukumu inakaziwa Mahakama Kuu. Nikaanza kujihoji, hivi ni kwanini Mahakama iliyotoa uamuzi wake isikazie hukumu yenyewe mpaka eti Msajili wa Mahakama ya kazi ndiye aje kukazia? Na kwa bahati mbaya sana, kesi moja niliimaliza Kigoma na kushinda mwaka 2013, lakini mpaka sasa haijakaziwa hukumu. Sasa kama wanaokazia hukumu ni Wasajili, basi wawe wanatembelea mikoani na wakifika wafanye Ukazaji kweli na si kufika na kula per diem na kuahirisha kesi bila kutazama haki za walioshinda. Vinginevyo, CMA inatakiwa ipewe mamlaka ya Kukazia Hukumu zake yenyewe na wapewe ili haki za wadau zisicheleweshwe. Mbona Mahakama ya Ardhi na Nyumba wao wanakazia wenyewe?

(8) Hivi wadau, mkienda kule CMA mnakutana na Ulinzi wa polisi kama Mahakama nyingine? Hawa Mahakimu wa CMA wanapata shida sana pale wanapopata wadau wabishi na wakorofi. Wengine wanapigwa na yupo jamaa kule Musoma alikimbia ofisi baada ya kina Mura kumchukulia masimu yake ya bei ghali. Ana bahati hakupigwa. Lakini Serikali, mlishawahi kulitazama hili, ni kwanini hawa wafanyakazi wa CMA wasipewe Ulinzi wakati wanaendesha kesi, walau wakiwa ndani ya Mahakama zao ili kujiepusha na madhara ambayo yanaweza kuwapata wakiwa wanaendesha kesi za wadaawa wakorofi. Wapeni ulinzi vijana wasije wakadhuriwa ikawa tabu hapo.

(9) Viofisi vingine vya CMA ni vidogo sana kiasi kwamba wadau wanabanana mpaka basi, serikali na kwa vile sasa ipo chini ya Waziri Mkuu, ichukue hatua za makusudi kabisa kuhakikisha kwamba CMA inakuwa na ofisi zake binafsi ili kuwa huru zaidi.

(10) Nimekuwa najiuliza swali moja, ni kwanini Mahakama ya Tanzania (Judiciary) isiichukue hii taasisi na kuiweka chini yake? Kwa sababu kwa mtazamo wangu naona taasisi hii ipo chini ya wrong ministry, na kwa sababu hiyo hata huduma zake zinaonekana kusua sua kwa sababu haipati budget ya kutosha. Inaonekana inabanwa. Sasa Judiciary wangeichukua, naamini kwamba hata utendaji wao wa kazi ungekuwa safi sana.

Hapo walipo CMA, hawana motisha, hawapati professional attires allowances, hawapati House Rent Allowance, Hwana hata extra duties allowance.....................ni shida sana kwa watumishi wa CMA kutoa haki kwa wadau ukizingatia kwamba na vimishahara vyao ni viduchu, kama unavyojua mishahara ya serikali.

MWISHO, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CMA anaonekana yupo vizuri. naona anaanza kufanya mabadiliko kidogo kidogo. Ajitahidi aendane na kasi ya Mzee wa Hapa Kazi tu.

Waziri Mkuu, tembelea ofisi hii, ipo chini ya Ofisi yako; Mwakyembe waziri wa Sheria, tazama endapo bado Taasisi hii inastahili kuwa chini ya Wizara ya Kazi (Kwa sababu kazi zake ni za Kimahakama kabisa, ni kwanini usibadilishe sheria ukaichukua na kuiweka chini ya Wizara yako tena kwenye Mhimili wa Mahakama)

Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, wewe ni Mwanasheria, itazame hii taasisi, inaweza kufa kifo cha mende kama hatua zisipochukuliwa. Shirikiana na Mheshimiwa Mwakyembe kuona namna ya kuinusuru taasisi hii inayokaribia kufa.

Mkurugenzi, tembelea ofisi zako Mkoa wa Dodoma, kunanuka rushwa (rejea jalada lililoenda Mahakama Kuu bila vielelezo).

CMA ofisi nyeti sana, Isaidieni iendelee kuwa nyeti kwa sababu ina deal na haki za wafanyakazi na waajiri, kama mkiiacha ikafa, nchi yetu itapata aibu kubwa sana kwa sababu mpaka nchi za Ulaya na Asia wanakuja kuiga utendaji kazi wa CMA.
 
Mabaraza ya ardhi ni hovyo kabisa kuwahi kutokea.....ofisi za mabaraza ya ardhi ni kama mashimo ya panya,hovyo kabisa anzia dar mpaka mtwara,musoma ndio ujinga kabisa
 
Jamani kweli hii Commission inadharauliwa. Kuna watu wanajiita Wawakilishi binafsi ndani ya Tume ambao wanafanya kazi ya kuwakilisha wateja km mawakili. Kuna wengine ni wajinga wasiokuwa na mfano.
Kuna mtu mmoja anajiita Peter Mnyanyi, kwa historia alikuwa anafanya kazi SBC LTD, akaachishwa kazi. Sasa anavyosumbua..... Anaweka mapingamizi yasiyokuwa ya msingi kwenye makesi yake anayosimamia mpk anakera
 
Na nawashangaa sana hao CMA, hivi hawaoni kwamba kuwaruhusu watu wasiokuwa na taaluma ya sheria kuwakilisha wateja ni ukiukwaji wa sheria. Ni lini watatuondolea hawa wasumbufu? Sheria hawazijui basi ukikutana nao hasa huyo Mnyani ni shida na ma PO yasiyoisha. Sisi mawakili tunapata shida sana ku deal na lay men type za kina Mnyani
 
Na nawashangaa sana hao CMA, hivi hawaoni kwamba kuwaruhusu watu wasiokuwa na taaluma ya sheria kuwakilisha wateja ni ukiukwaji wa sheria. Ni lini watatuondolea hawa wasumbufu? Sheria hawazijui basi ukikutana nao hasa huyo Mnyani ni shida na ma PO yasiyoisha. Sisi mawakili tunapata shida sana ku deal na lay men type za kina Mnyani
Mbali na hii, wako shalo sana! Kichwani hawana vitu, na sheria zenyewe hawazijui...
 
Mungu yupo. Mwenyewe niliacha kupeleka shauri langu huko baada ya kutonywa na mtu wangu kwamba .walikuwa wamepewa maelekezo ya kutonitendea haki. Nilimwachia Mungu.
 
Mimi nilishinda vizuri kesi yangu pale CMA headquarters Dsm/Kinondoni. Sikuona hata dalili ya rushwa na mwajiri alinikoma.

Hongera sana CMA siwezi kuacha kuwatetea ntakuwa siwatendei haki.
 
Mungu yupo. Mwenyewe niliacha kupeleka shauri langu huko baada ya kutonywa na mtu wangu kwamba .walikuwa wamepewa maelekezo ya kutonitendea haki. Nilimwachia Mungu.
Hasira za mkizi furaha ya Mvuvi. Usiwe hivyo Ndugu, rudi Mahakamani kadai haki yako.
 
Tatizo CMA imesuswa katibu mkuu anapendelea sana idara ya kazi , jamaa yangu alipata kazi hapo akakacha maana hawaeleweki wanatia huruma ,wamepauka balaa hiyo rushwa ya kula itatoka wapi wakati wateja wao wenyewe ni walinzi wa makampuni na wafanyakazi choka mbaya wa viwanda?
 
Tatizo CMA imesuswa katibu mkuu anapendelea sana idara ya kazi , jamaa yangu alipata kazi hapo akakacha maana hawaeleweki wanatia huruma ,wamepauka balaa hiyo rushwa ya kula itatoka wapi wakati wateja wao wenyewe ni walinzi wa makampuni na wafanyakazi choka mbaya wa viwanda?
Acha ujinga. Inawezekana ulishindwa kujieleza au hukuwa na strong evidence.

Halafu unaposema wateja ni walinzi ambao ni choka mbaya labda akili yako ndiyo choka mbaya.

Hivi hujui aliyekuwa expert manager kutoka India wa Serengeti breweries (SBL) alifukuzwa kazi na alipoenda CMA akawashinda na CMA ikaamua alipwe more than TZS 1 billion. Ikabidi SBL waombe revision High Court na huko wakamkuta Jaji Mipawa akawatwanga tena vilevile.

Mwaka jana Juma Kaseja alikuwa na kesi yake pale nadhani aliwashitaki Simba. Mwaka huu Charles Boniface wa Yanga anarandaranda pale High court baada ya kushitakiwa na baadhi.

Sikupi mifano zaidi. Hii inatosha kukuonyesha kwamba huijui CMA.
 
Acha ujinga. Inawezekana ulishindwa kujieleza au hukuwa na strong evidence.

Halafu unaposema wateja ni walinzi ambao ni choka mbaya labda akili yako ndiyo choka mbaya.

Hivi hujui aliyekuwa expert manager kutoka India wa Serengeti breweries (SBL) alifukuzwa kazi na alipoenda CMA akawashinda na CMA ikaamua alipwe more than TZS 1 billion. Ikabidi SBL waombe revision High Court na huko wakamkuta Jaji Mipawa akawatwanga tena vilevile.

Mwaka jana Juma Kaseja alikuwa na kesi yake pale nadhani aliwashitaki Simba. Mwaka huu Charles Boniface wa Yanga anarandaranda pale High court baada ya kushitakiwa na baadhi.

Sikupi mifano zaidi. Hii inatosha kukuonyesha kwamba huijui CMA.


Mkuu tupo pamoja nawatetea hao CMA kwamba wanafanya kazi mazingira magumu na hata kama wanakura rushwa basi kiwango kidogo sana maana wateja wao wengi ni wa hali ya chini wasioweza toa rushwa ,hao wa Serengeti au maarufu huwa wachache sana
 
Haka kajamaa kanako weka mapingamizi yasiyo na kichwa wala miguu nadhani kanitwa Christopher Mumanyi...hopeless kabsa. Huwa kana wakilisha waajiri.
Kuna Christopher Mumanyi lakini huyo mwingine Bogus kabisa anaitwa Peter Mnyani.. Yaani kichwa chake utafikiri kina funza!! Yaani ni empty box!! Huyu alikuwaga mfanyakazi wa Pepsi..... Sasa akawa na kesi pale Cma akapata uzoefu lakini much know but empty
box!!
 
Kuna Christopher Mumanyi lakini huyo mwingine Bogus kabisa anaitwa Peter Mnyani.. Yaani kichwa chake utafikiri kina funza!! Yaani ni empty box!! Huyu alikuwaga mfanyakazi wa Pepsi..... Sasa akawa na kesi pale Cma akapata uzoefu lakini much know but empty
box!!

Niliwahi kuwa na kesi pale Arusha cma wanapenda rushwa kweli ila bahati yao hawakuingia kwenye mtego maana niliwaripoti pccb ila wataingia tu 18 za pccb maana hawana hata aibu wanakula rushwa waziwazi
 
Wanae mkurugenzi somebody Mwidunda kama sijakosea
Yupo Mkurugenzi Mkuu pale anaitwa somebody NUNGU!!

Ajitahidi hata kuwafungia wale vijana AC, wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana.

Chumba kimoja kina waamuzi wawili hadi wanne. Sasa hiyo Mahakama sijui ni ya wapi. Nijuavyo Mimi, Chamber moja ya Mahakama inakuwa na Hakimu mmoja na Karani wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom