Combination ya Kassim Majaliwa, Jakaya Kikwete na Benard Membe Uchaguzi Mkuu 2025

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Siasa ni mchezo mchafu sana, na wanasiasa hawaaminiki wala hawaaminiani kamwe... Kwenye siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu..

Ikumbukwe Mwaka 2015 Benard Membe alikatwa kwenye kinyang'anyiro cha Urais kupitia CCM..Baadae akahamia ACT Wazalendo japo hakutoboa.

Leo October 2021 nimeona Majaliwa yupo Rondo kwa Kijijini kwa Membe. Ikumbukwe hawa wanatoka Mkoa mmoja. Ikumbukwe pia, JK na Membe ni ndugu wa damu.

Mwakani 2022 ni Uchaguzi wa ndani ya CCM, ni muda muhimu wa kupanga safu ya 2025.

Leo Membe ametamka kabisa atarudi CCM. Akirudi maana yake...!?

Muda utaongea
 
Just choose the best side

Kila mtu anaangalia tumbo lake

Maendeleo Tanzania hasa ya teknolojia na fikra yatachukua muda kidogo lakini kuna kizazi watafika lengo

Hata sasa walioanzisha vyama vingi ilichukua muda watu kuamini kuwa kuna maisha nje ya CCM, Lakini upinzani umekuwa tishio kuliko watu wanavyofikiria

kura za haki mikoa kama Dar, Mbeya na Arusha kwa Tume huru ya uchaguzi ccm inaangukia pua kwa Kipigo kikubwa

Shule za kata hata kama vijana walipata Sifuri lakini wamebadilishwa kifikra na wanaamini hawapaswi kuishi maisha walioishi, Wanahitaji maisha bora kama ya viongozi wao


Chagua upande sahihi
 
Mama Samia ndio Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano na Amiri Jeshi mkuu.

Kumtoa hapo labda wamshawishi au aamue kwa hiyari, Kinyume na hapo mnajilisha matango pori.
 
Ukiona wanasiasa wamekuwa maadui jua hiyo ni movie, ikiisha wanaendelea na life lingine.
 
Membe ni spea tyre.. anaweza kupata nafasi ya kugombea uraisi mwaka 2030 after president Samia kumaliza muda wake. Lkn kwa 2025 wewe na Membe wako msahau.
 
Mimi bado naamini litatokea la kutokea ambalo litasababisha mizani ya makundi ya siasa na wapambe wao kubadilika tena kama ilivyotokea. Nchi bado haijatulia na si ajabu kina Kikwete na Membe wakijikuta tena wamerudi back to square one kama walivyokuwa kabla ya kifo cha Magufuli.
 
Ukiangalia haya mambo kwa undani utaona vile watanzania tunachezewa akili na kikundi kidogo cha watu, nasi tunawaangalia tu, hii nchi sasa kuna kundi la watawala na watawaliwa.
 
Back
Top Bottom