Colonel Dr. Hassy Kitine afichua siri yake na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere

pamoja na masimulizi mazuri ya huyu kachero. nina mashaka naye juu ya kifo cha tuntemeke

pia maelezo yake baada kutofautiana na mwalimu hayako clear.

si hivyo tu hata baada ya kufukuzwa ukachero. akiwa waziri alionyesha tabia yake ya uroho wa vitu. ikapelekea kufukuzwa uwaziri
 
Kachero huyu hakuulizwa kashfa ya kugushi matumizi ya sh 60 million kama matumizi ya matibabu ya Mke wake nchini Marekani
 
Unchanganya mambo ndugu! Anakosema kulikuwa na udini ni Iringa Mjini ambako alishinda Chiku Abwao wa NCCR Mageuzi na si kwamba alishindwa dhidi ya Tutemenke Sanga kule Makete!!!
Du; kwenye hili tuachieni tuliopiga KURA Iringa mjini that time; Chiku alikua viti maalumu but aliyeshinda ni heard master wa shule moja ya wazazi ccm inaitwa Mwembe togwa. Kwa wasio fahamu Iringa mjini imejaa sana Waislamu na kila baada ya km chache unakutana na msikiti tena msikiti kweli, yaani mkubwa so kusema eti Hassy alishindwa kwasababu ya dini yake, huo ni uongo. Mageuzi yalipamba moto sana mwaka ule, kwa mbaaali nafananisha uchaguzi ule wa 95 na wa mwaka 2015, upinzani uliishika sana nchi mwaka huo tena ukichukulia Zambia alikua ameshinda mpinzani bwan Chiluba (nafikiri ilikua mwaka 92) na Malawi pia halafu ccm wakawa wamemfukuza Mrema aliyekua kawashika sana wapiga KURA wa Enzi hizo, yaani acha tu, nimekumbuka mbali.
 
kama kawaida yenu na utetezi,mficha maradhi mauti humuumbua,haya yalimkuta kitwana kondo na ubunge kigamboni
Pamoja na Udini unaotajwa kuwepo lakini ieleweke wazi kuwa Joto la Mageunzi na upinzani chini ya Lyatonga lilikuwa kubwa mno kwenye siasa za ukanda ule nyakati hizo hiyo yaweza kuwa miongoni mwa sababu kubwa zaidi.
 
Kachero huyu hakuulizwa kashfa ya kugushi matumizi ya sh 60 million kama matumizi ya matibabu ya Mke wake nchini Marekani
Mahojiano mengine ni ya kupanga haya, anapewa muandishi rafiki, anatoa softball na hagiography mwanzo mpaka mwisho.

Katika maisha ya Kitine, hilo swali linakuwa kubwa kabisa. Haitakiwi muandishi wa habari yeyote, hata kama ni rafiki yake, asiulize hilo japo kizushi tu.

Ni kama unaandika maisha ya Bill Clinton halafu usiandike kashfa ya Monica Lewinsky au unaandika maisha ya Nixon halafu usiandike kashfa ya Watergate.

Inaonyesha hii interview ni ya kirafiki sana, haina standards za uandishi wa habari.
 
Du; kwenye hili tuachieni tuliopiga KURA Iringa mjini that time; Chiku alikua viti maalumu but aliyeshinda ni heard master wa shule moja ya wazazi ccm inaitwa Mwembe togwa. Kwa wasio fahamu Iringa mjini imejaa sana Waislamu na kila baada ya km chache unakutana na msikiti tena msikiti kweli, yaani mkubwa so kusema eti Hassy alishindwa kwasababu ya dini yake, huo ni uongo. Mageuzi yalipamba moto sana mwaka ule, kwa mbaaali nafananisha uchaguzi ule wa 95 na wa mwaka 2015, upinzani uliishika sana nchi mwaka huo tena ukichukulia Zambia alikua ameshinda mpinzani bwan Chiluba (nafikiri ilikua mwaka 92) na Malawi pia halafu ccm wakawa wamemfukuza Mrema aliyekua kawashika sana wapiga KURA wa Enzi hizo, yaani acha tu, nimekumbuka mbali.
Idadi kubwa ya wanafunzi ndio lilikuwa anguko lake.
Mwembetogwa, Mkwawa, Highlands na Iringa girls waliungana kwa ajili ya kumpitisha mwalimu Mwakibasa, ajabu hata chuo cha Klerruu walimuunga mkono mwalimu.Ingekuwa ni udini Hassy angepita kirahisi sana kwa population ya waislam kwa mji wa Iringa. Na ikumbukwe hotuba ya Mwalim Nyerere 1,May,1995 iliwafungua watu wengi sana akili zao
 
Dr Kitine amefanya vizuri sana kunyoosha mambo mengi yanayomhusu pia kutuwekea historia ya Tanzania kwa kiasi anachotaka yeye.
Dr Kitine kwa umri ananizidi miaka mitano na mimi natoka Iringa pia. Ningependa kushauri yafuatayo:
1. Msomi ye yote wa kweli huwa hatambi kuwa ni msomi. Kwa hakika ukiwa msomi ndipo uanaelewa kiasi gani ambacho ni mjinga!
2. Mambo yote yawe ya usalama, ulinzi, au kiasi gani unamjua Nyerere hayakupi ukiritimba wa kukufanya kuwa unajua mambo hayo au mengine kuliko mtu mwingine ye yote.
3. Ukiandika kitabu kuhusu jambo lo lote inafaa ufikirie kitaleta tofauti gani chanya katika fikra au ujuzi kwenye jamaa husika.
4. Masuala yaliyomwangusha Dr Kitine wakati wa kugombea Ubunge Iringa ni mengi lakini moja wapo ni kama ni lile lile lililomwangusha marehemu Daudi Mwakawago hapo hapo Iringa; ni ushiriki wa Mwalimu Nyerere kwenye jukwaa la kampeni pale Iringa.
5. Sifa kubwa ya Dr. Kitine ni kweli hakujilimbikizia mali. Hili halina ubishi na nampa hongera za dhati.
6. Ningekuwa namwuliza maswali ningemwuliza swali moja tu kwamba je yeye anajihisi ana mapungufu yapi pamoja na sifa zote anazoona anazo: Hili swali huwa siku hizi linaulizwa kwenye usaili wa ajira, hasa ajira za uongozi au ningemwuliza kama alimfahamu muasisi wa hiyo Tume ya Usalama, marehemu Mzee Mzena na kama alimfahamu alijifunza nini kwake.
Kama Dr Kitine akiweza kutafakari mambo haya hata kitabu chake kitakuwa kizuri sana. Namshukuru tena Dr Kitine na mwandishi wa stori hii.
 
Idadi kubwa ya wanafunzi ndio lilikuwa anguko lake.
Mwembetogwa, Mkwawa, Highlands na Iringa girls waliungana kwa ajili ya kumpitisha mwalimu Mwakibasa, ajabu hata chuo cha Klerruu walimuunga mkono mwalimu.Ingekuwa ni udini Hassy angepita kirahisi sana kwa population ya waislam kwa mji wa Iringa. Na ikumbukwe hotuba ya Mwalim Nyerere 1,May,1995 iliwafungua watu wengi sana akili zao
Upo sawa kabisa mkuu, Hassy hakushindwa uchaguzi ule kwasababu ya dini yake, alishindwa kwasababu ya hao wasomi watarajiwa. Mimi nilikua hapo kwenye bold.
 
Makongoro east ya chini 1994/96 PCM
Khaaa, we ni met wangu kabisa kaka. Itabidi tukutane somewhere tupige mastory yetu ya town, mi pia ni mwaka huo huo yaani 1994/1996 the same combination na mwalimu wangu wa darasa pamoja na bweni ni yule yule sir Ngui. Haa ha ha ha, nimekumbuka mbali sana mkuu
 
Mahojiano mengine ni ya kupanga haya, anapewa muandishi rafiki, anatoa softball na hagiography mwanzo mpaka mwisho.

Katika maisha ya Kitine, hilo swali linakuwa kubwa kabisa. Haitakiwi muandishi wa habari yeyote, hata kama ni rafiki yake, asiulize hilo japo kizushi tu.

Ni kama unaandika maisha ya Bill Clinton halafu usiandike kashfa ya Monica Lewinsky au unaandika maisha ya Nixon halafu usiandike kashfa ya Watergate.

Inaonyesha hii interview ni ya kirafiki sana, haina standards za uandishi wa habari.
Mkuu, labda nikukumbushe, kabla gazeti hili la raiamwema halijaanzishwa, wamiliki wa hili gazeti ndio waanzilishi wa kampuni ya Habari cooperation Ltd ya pale Sinza na ni kampuni hiyo hiyo ndio ilio chunguza na kutoka na kashfa iliomwondoa mzee Hassy kwenye uwazi if not ukuu wa mkoa wa Tanga, so msimlaumu mwandishi kwa kuto muuliza hilo swali, baada ya story hiyo kutoka ndipo mzee Jenerali Ulimwengu alipoaanza kuishi kwa kulipia Uraia wake hapa BONGO. Tuulizeni wahenga tutawaambia. This is why kwenye issues za rushwa na ufisadi jamaa simkubalii kiiivile.
 
yes ni uzi mzuri mno .name ningependa aandike kitabu na ajitahidi to tell as is,ningependa kujua ni jinsi gani rais wetu wa awamu ya kwanza alivyowachukulia watu ambao walitofautiana nae kiitikadi,vile vile je aliplay any part kuhusu kuugua na kupelekea kifo cha T.M.N.Sanga(Tuntemeke) aliyekuwa mbunge machachari wa Makete.
 
Khaaa, we ni met wangu kabisa kaka. Itabidi tukutane somewhere tupige mastory yetu ya town, mi pia ni mwaka huo huo yaani 1994/1996 the same combination na mwalimu wangu wa darasa pamoja na bweni ni yule yule sir Ngui. Haa ha ha ha, nimekumbuka mbali sana mkuu
Hahahaa Ngui mzee wa ku panic. Nilikuwa PCM 2.Karibu sana mkuu
 
Back
Top Bottom