Colonel Dr. Hassy Kitine afichua siri yake na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere

Dah mzee yupo deep, pamoja na nafasi zote alizozishika lkn maisha yake ya kawaida, sasa watafute watu wanaoshika vyeo kama alivyowahi kuvishika yy uone walivyokuwa na utajiri wa kutisha. Kuna haja ya hawa wazee ya kuandika vitabu juu za kazi zao naona zitachochea uzalendo na kama ikiwezekana viingizwe ktk mitaala ya shule, ili vijana watambue wapi tulipotoka na wapi tunaenda naona itachochea uzalendo.
 
Mzee kitine kuna sehemu kateleza...yeye wakati anakuja kugombea Iringa kikao cha kwanza alifanya na wazee wa kikinga..hapo akajiweka sehemu mbaya...udini haukuwepo wakati ule...pia alikuwa anatudanganya sana wakati wa kampeni..mara kwa mara alikuwa akisema yeye amesoma mpaka sehemu imeandikwa mwisho..wakati darasani tuliambiwa haina mwisho..pia alifikiri pesa itatununua watu wa iringa mjini..alimwaga pesa nyingi sana..
Matokeo yake akadondoshwa na mwalimu wa secondary
Nakumbuka alikuja kufanya kampeni Mkwawa high school,kwenye uwanja wa mpira.Maswali aliyo ulizwa alishindwa kuyajibu,aliapa ikiwa atapita shule yetu ingekuwa ya kwanza kuishughulikia lakini akiukosa ubunge tutamkuta UD.
 
Nilimfahamu vizuri sana huyu kachero mwaka 1995 alipogombea ubunge Iringa mjini, mimi wakati huo nilikua nasoma A-level Mkwawa High school; CV yake ilitisha na baadhi ya vitu alivyo visema hapa alivisiema pia kwenye karatasi yake ya kugombea na hata alipokuja Mkwawa pia alitwambia but kwa vuguvugu la uchaguzi wa wakati huo Augostine Lyatonga Mrema akiwa kaishika sana Tanzania huyu bwana tulimpiga chini UBUNGE na tukampa aliyekua heard master wa Mwembetogwa Secondary school, shule iliokua ikimilikwa na ccm but yeye aligombea kwa njia ya NCCR-Mageuzi. Baada ya uchaguzi ule nakumbuka tulipata shida sana wanafunzi wa Mkwawa na Iringa Girls kwenye mitaa ya Iringa, wazee walitulaumu kwa kuwachagulia mbunge ambaye sio. Bado nikikumbukaga uchaguzi ule still bado hua naona niliitendea haki nafsi yangu. Kwa ufupi huyu bwana kwenye issues za RUSHWA nae ni muhusika, wanafunzi tulikula sana pesa zake wakati ule.
Mkuu kumbe tulikuwa wote kwenye uwanja wa mpira.
 
uzi mkali ila hautembei kabisa wakati ule wa "comment chochote upate like" upo page ya elfu 30 sijui. ndo maana hata kwenye lugha ngeni wabongo tunaanzaga kujua matusi kwanza
 
Kule.wapi ambako yeye hakuwepo? Unafiki mnao nyinyi mnaopigania udini. Tanzania ni ya watanzania. Siyo ya dini fulani maalumu. Hata uarabuni yanawashinda. Wanagawana vipisi vipisi sembuse hapa???

Sent using Jamii Forums mobile app
Aliyesema "kule" kuna udini ni aliepata kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa. Kwanini suala la udini hakulisema "alipopigwa jungu la kununua Benz" na alizungumzie kwenye uchaguzi wa Iringa Mjini; hususani tuhuma dhidi ya wasimamizi wa uchaguzi? Yaani kwa akili yako ndo ushaona yeye ndie mdini na mpigania dini!! Angekuwa ni mdini au mpigania dini angekuwa na wakurugenzi wanne ambao kwa majina wanaonekana karibu wote ni Wakristo?! Angekuwa ni mdini au mpigania dini Mwalimu angekuwa anachukua maoni kwake alipokuwa anafanya teuzi? Angekuwa mdini na mpigania angeweza kufikia nafasi ya juu kama hiyo wakati wa Mwalimu?

Isitoshe nimelkuuliza ina maana huo ukurugenzi alipewa na wana-Iringa Mjini hususani wasimaizi wa uchaguzi wa Iringa Mjini?! Jibu hilo swali. Habari za Watanzania ni ya Watanzania zinatoka wapi sasa?! Kwani kuna mahala alipolalamikia Watanzania?! Au kuna maahala aliposema au niliposema kwamba Tanzania ni ya watu wa aina fulani?! Suala la Uarabuni linatoka wapi?
 
waandishi wetu matatizo sana mbona hakumwuliza kuhusu ile kashifa ya mke wake ya fedha za matibabu canada iliyomfanya atoke kwenye uwaziri, halafu huyo jamaa mwongo sana nimesoma Iringa o level na A level iringa mjini wamejaa waislamu hivyo sio sababu ya yeye kushindwa ubunge
Nami nilisoma hadi nukta ya mwisho nikitarajia kukuta hilo swali! Ni unafiki wa waandishi manake wanafahamu ni kweli Kitine alipiga ule mpunga kwahiyo waliogopa kumu-embarrass. Nilitamani angeulizwa ili nione uwezo wake wa kukataa manake kwa vyovyote vile, angekataa tu!
 
Akili mbovu kabisa hizi! Aliyesema "kule" kuna udini ni aliepata kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa. Kwanini suala la udini hakulisema "alipopigwa jungu la kununua Benz" na alizungumzie kwenye uchaguzi wa Iringa Mjini; hususani tuhuma dhidi ya wasimamizi wa uchaguzi? Yaani kwa akili yako ndo ushaona yeye ndie mdini na mpigania dini!! Angekuwa ni mdini au mpigania dini angekuwa na wakurugenzi wanne ambao kwa majina wanaonekana karibu wote ni Wakristo?! Angekuwa ni mdini au mpigania dini Mwalimu angekuwa anachukua maoni kwake alipokuwa anafanya teuzi? Angekuwa mdini na mpigania angeweza kufikia nafasi ya juu kama hiyo wakati wa Mwalimu? Acha akili mbovu wewe.

Isitoshe nimelkuuliza ina maana huo ukurugenzi alipewa na wana-Iringa Mjini hususani wasimaizi wa uchaguzi wa Iringa Mjini?! Jibu hilo swali. Habari za Watanzania ni ya Watanzania zinatoka wapi sasa?! Kwani kuna mahala alipolalamikia Watanzania?! Au kuna maahala aliposema au niliposema kwamba Tanzania ni ya watu wa aina fulani?! Suala la Uarabuni linatoka wapi?

Hongera sana wewe mwenye akili safi na dini inayoonewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana wewe mwenye akili safi na dini inayoonewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Jibu maswali kama huwezi; nyamaza! Hakuna popote niliposema mimi ni dini ipi isipokuwa nimeelezea suala la udini kwa ujumla wake lakini kutokana na mawazo yako ya hovyo tayari umesha-conclude! Endelea kubaki na unafiki wako wakati suala la udini nchi hii wala sio geni!
 
Jibu maswali kama huwezi; nyamaza! Hakuna popote niliposema mimi ni dini ipi isipokuwa nimeelezea suala la udini kwa ujumla wake lakini kutokana na mawazo yako ya hovyo tayari umesha-conclude! Endelea kubaki na unafiki wako wakati suala la udini nchi hii wala sio geni!
Kwanini wewe usinyamaze mwenye dini safi inayoonewa kuliko nyingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini wewe usinyamaze mwenye dini safi inayoonewa kuliko nyingine?

Sent using Jamii Forums mobile app

Muendelezo wa akili mbovu!!! Dini safi ipi?! Kuna mahali niliposema suala la dini safi na dini chafu?! We jamaa vipi wewe?!

Wakuu samahani sana mnaharibu lengo la huu uzi, sasa hivi utakuwa uzi wa udini. Kuna mengi ya muhimu zaidi ya kujifunza kwahiyo hili tuliache mwenye kuelewa kaelewa.

Natumaini sijawakwaza
 
Wakuu samahani sana mnaharibu lengo la huu uzi, sasa hivi utakuwa uzi wa udini. Kuna mengi ya muhimu zaidi ya kujifunza kwahiyo hili tuliache mwenye kuelewa kaelewa.

Natumaini sijawakwaza
Shukrani. Sitaki kabisa kujibizana ila naona mwenzangu anataka ligi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua, ngoja nikwambie, Baba wa Taifa wamemwambia watu wa ndani kwamba Kitine naye ameagiza gari. Baba wa Taifa akachukia sana akaniita …. akaniuliza nikamweleza.

Hatari kweli kweli ,"socialism " ya Nyerere ilikuwa hatari sana,yaani nashangaa huyu Kitine kaitumikia nchi ya Tanzania kwa uwezo wake wote,lakini kaletewa gari tu Nyerere kakasirika..,roho mbaya,roho ya kichawi,bado Tanzania wako watu wana roho kama ya Nyerere...
 
Back
Top Bottom