Naomba kujua kama kuna sheria inayoruhusu debt collection ya deni la nje ya nchi kufuatia hukumu ya mahakama ya nje kutibitisha deni na kama ikiwa mdaiwa ni raia wa Tanzania na ana mali Tanzania.
sheria za tanzania zinatambua hukumu zilizotolewa katika mahakama za nchi zingine kwa mujibu wa sheria ya reciprocal enforcement of foreign judgement Act, ili mradi masharti yafuatayo yatimizwe.
1 lazima hukumu hiyo iwe imetolewa katika mahakama kutoka nchi zinazotambuliwa na sheria (schedule yake ina orodha ya nchi hizo)
2 iwe imetolewa na mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.
3 kusiwe na mgongano wakisheria kati ya sheria mbili za nchi husika yaani tanzania na nchi ambako hukumu hiyo imetolewa. kwa mfano mkataba uwe halali kwa mujibu wa sheria za tanzania au dhumuni la mkataba liwe halali kwa sheria za tanzania.
ukishajiridhisha hayo utafungua shauri la kusajili hukumu yako mahakama kuu likishasajiliwa utapewa utaratibu ni namna gani utaweza kukusanya deni lako.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.