Naupenda huu wimbo, enjoy mistari toka kwa Dallarz na Banana
Mtaani kwetu mwanangu kuna mambo mengi,
mtaani kwetu vituko vingi, mtaani kwetu mwanagu wambea wengi.
Mtaani kwetu wachawi wengi.
mtaani kwetu ee bwana wee utakonda, unakula nyama wengine wanakula ng'onda,
Mtaani kwetu hakuna anayekupenda,
Unahaimia leo kesho unakwenda,
Unapigwa chale usiku unaliwa denda.
mtaani kwetu tunapaweza wenyewe,
Akiibiwa mtu wenyewe kwa wenyewe tunaimbizana Hadi kesi zinakwisha.
mtaani kwetu kunanifurahisha,
Mtoto mdogo anakutingisha,
Kashika bisibisi huku anakutisha,
Ukiwa muoga utasema leo nimekwisha,
Mtaani kwetu hatupendi shule,
Ukitagaza ndoa demu unapewa bure,
Mtaani kwetu usifungue duka,
Wataliwangia hadi liwe linanuka,
Mtaani kwetu hata vyumba havipo,
Tarehe 28 ujiandae na malipo,
Ukipitisha siku vitu vyako havipo,
Kachukua nani baba mwenye nyumba
Mtaani kwetu misikule inalishwa pumba,
Mtaani kwetu kwani mbali,
Si unasikia ngoma watu wanamlema mwali,
Mtaani kwetu chakula chetu ugali.
Mtaani kwetu kweli kiboko,
mpaka sikukuu ndio tunafanya mitoko,
Likinyesha mvuatope la ugoko
Mtaani kwetu usiwe mroho wa nyama,
Mjanja mzima wamenilisha panya,
Mtaani kwetu pananichanganya,
Mtu anapengo utazani mwanya,
Mtaani kwetu mimi sina la kufanya,
Nikiimba mziki eti bishoo,
Nifanye kazi gani? Mzibua vyoo
Mtaani kwetu jamani mnanizingua,
Maendeleo sina mnataka kuniua
Mtaani kwetu kondom ya nini,
Karibia wote tunaumwa Ukimw,
Mtaani kwetu heshima hakuna,
Mtoto mdogo anatukana wakubwa,
Na mzazi anamwabia mwanae mbwa,
Kama yeye mbwa na wewe mbwa,
Jibu kamili wote mijibwa🤣🤣