Hapa tupo pamoja sana....Mi sintosahau siku moja tumeenda Club tupo watatu tukiwa kwenye dance floor tunacheza nikamkanyaga jamaa mmoja bahati mbaya yupo na demu wake na machalii wengine...Tukazinguana pale mabaunsa wakaja tukaachanishwa jamaa akaniambia kama vp twende nje tukafundishane adabu nikamwambia twende boya tu wewe...Duh jamaa kumbe ni bondia bwana tukapiga mkono hapo nje hakuna mtu anaamua...watu wametuzunguka wameeka round, kama dk 10 za kwanza jamaa nikaona nammudu kabisa baada ya dk 10 ile nimeanza kuchoka jamaa akafungulia ngumi alizipiga hadi nikasema hapa ntakufa..nampa 1 ananipa 3 safi..Nikaona isiwe tabu nikamwambia asee jomba wacha ujinga utakuja niua nanii.. watu wakanicheka mno jamaa wakaja wakaamua sababu jamaa ni bondia akanifuata akaniambia hata ivyo umejitahidi twende zetu ndani...Sikuweza rudi Club tena nimeiva mwili mzima.. Toka siku hiyo nilipunguza sana ugomvi ugomvi.