Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,829
- 43,276
Wana Jf kama mtakumbuka hivi karibuni serikali kupitia wizara ya afya ilipiga marufuku urushwaji wa matangazo yote yanayo husu tiba za asili kwenye runinga,radio na mitandao ya kijamii mpaka hapo itakapo amuliwa tena..!
Baada ya tangazo lile nilitegemea vyombo vya habari vingekuwa vya kwanza kuheshima na kutekeleza agizo la serikali lakini imekuwa vinginevyo!
Nimewaandika Clouds TV moja kwa moja maana leo saa 3 nimeona kipindi cha tabibu Fadhili(Fadhageti) kikiitwa Matunda leo kama sijakosea ambacho maudhui yake ni yale yale kuhusu tiba asilia!
Serikali aliamua kuyapiga marufuku haya matangazo na vipindi vyake ili kuwakagua upya lakini cha kushangaza vyombo vya habari vinaweka biashara mbele na kushindwa kuheshimu serikali!
Nawaomba TCRA na serikali wawarudishe kwenye mstari na ni vyema wakajua wanafanya kosa serikali itakapo chukua hatua wasiwe wa kwanza kulalama!
Karibuni wana jamvi

Last edited by a moderator: