Kwa heshima na taadhima naomba kuwafikishia ujumbe huu Wamiliki wa Clouds FM juu ya wimbo wa Taifa ambao umekuwa ukipigwa sana kwa sasa kwenye radio hii.
Wimbo huu unaopigwa siyo wimbo halisi wa Taifa letu, umeongezwa vionjo vya aina ya akapela hivi na midundo lakini mapungufu makubwa zaidi ya huu wimbo ni kwamba umeimbwa ubeti mmoja tu wa mwisho. Hii kwa imani yangu kwa taifa hili naiona kuwa siyo sawasawa na ni vizuri kuikemea ili usiendelee kupigwa.
Naomba uongozi, Kaka yangu Joseph uliangalie hili kwa makini zaidi, nakubaliana na ubunifu ambao umekuwa ukifanyika na timu yenu kwenye mambo mengi lakini hapa kwenye wimbo wa Taifa nashauri tuuache ubaki vile vile. Tayari mtaani kwetu watoto wanaimba wimbo huo mpaya kama vile ndiyo wimbo wa taifa.
Kwa uelewa wangu na kwa kutembea kwangu, wimbo wa taifa unaweza kuimbwa tofauti lakini kwenye majukwaa ya live consert na hairuhusiwi kurecord. kwa sababu kuna madhara mengi sana ya kuupiga wimbo wa taifa kwa utofauti. Mojawapo ya madhara ni kwamba watoto wanaokua hawataelewa waushike wimbo upo tayari umebadilisha nembo mojawapo ya utaifa wetu.
Kwa kuwa hata watu wazima hawawezi kuuimba wimbo wetu wa Taifa ni vizuri mtusaidie basi kuwa mnaupiga wimbo halisi ili wengine waweze kuendelea kujifunza kutokea kwenu.
Naomba kuwasilisha