Clouds media wateka shughuli ya kumpokea Samata

Kidamva

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
2,578
1,984
Kama ilivyo kawaida ya Clouds Media kujiweka mbele kwenye issue za watu maarufu, sasa wameshajiweka kwenye mapokezi ya Samata.
Utakumbuka kwenye muziki wa Bongo flavor jinsi Clouds walivyokula kupitia kwenye migongo ya wasanii kama vile Diamond platnumz na wengineo.
Wengine kama vile Lady JD, Mr. Sugu walishtuka wakajiondoa.
Itakumbuka mwaka 2010 jinsi Clouds walivyopora tamasha la Ukimwi lililokuwa linaandaliwa na Mr. Sugu hadi wakagombana na Ruge Mutahaba kupitia vyombo vya habari. Mpaka leo hawapatani.
Ruge ambaye alijiweka karibu sana na utawala wa Rais Kikwete anadaiwa kupora studio ya wanamuziki waliyopewa na serikali na kuifanya kuwa THT.
Sasa wameshaona Samata ni deal, wamemfuatilia kwa muda mrefu. Sitashangaa kusikia Ruge ndio meneja wa Samata. TFF wamezubaa tu.
 
Once a chicken you will always be a chicken

Nchi ya wajinga ni ya wajinga tuuu
 
JAMAA WAMEONA FURSA WANAITUMIA SIO WAKUWALAUMU,,hapo ni Mwenyewe muhusika kujiongeza,,akili kumkichwa
 
Back
Top Bottom