Clouds FM wanawaibia Watanzania kwa kutumia Ujumbe mfupi wa simu

Clouds FM wanawaibia Watanzania kwa kutumia Ujumbe mfupi wa simu

NAMKWAKWA

Member
Joined
May 16, 2013
Posts
43
Reaction score
38
Kampuni ya Clouds media kupitia makampuni yake ya clouds f.m na clouds Tv wamebuni mbinu ya kuwaibia watanzania ambao wengi hawana uwelewa mkubwa wa matumizi ya teknolojia ya mawasiliano kwani wanakutumia ujumbe mfupi unaohusu shughuli za burudani wanazozifanya kisha wanakukata hela,pasipo wewe mpokea ujumbe wa simu kujiunga na huduma hizo kiasi wanachokata ni Tsh 150.Hili suala ni very sensitive kwani nimejaribu kuwapigia simu watu wa huduma kwa wateja na kuwalalamikia wao wamesema hawajui kitu zaidi ya kunishauri nitume neno STOP kwenda number 15556 Ili kusitisha ujumbe huo ambao unaiba pesa za watanzania,suala la kujiuliza hapa ni kuwa mimi ni mwelewa wa mabo ya mawasiliano je kwa mjomba wangu aliyepo kule kijijini Lukuredi kama atakuwa anatumiwa ujumbe na hawa watu kila siku na anakatwa hela pasipo ridhaa yake hawa watu watakuwa wanatengeneza mabilioni mangapi ya pesa?.Hata hao watu wa huduma kwa wateja kwenye makampuni ya simu kwa majibu yao wanaonekana wameelekezwa na maboss wao kuwa mtu akihoji hili suala umwambie ulijiunga mwenyewe atume neno ONDOA kWENDA NUMBER 15556,hIvi mtu mzima na akili zako unaweza jiunga kwenye huduma za kitoto za matukio ya fiesta?.
Ufuatao ni copy ya ujumbe mfupi ambao hii kampuni inautuma ovyo kwa watanzania na kuwakata hela bila ridhaa yao


"CLOUDS TV:Angalia mkali wa ngolongolo Diamond Platnumz akiwasha moto Fiesta 2012.Diamond amewakilisha Tabora, Dodoma.SIMU.TV;Bofya; http://db.tt/CXiJhfHZ "

Nakala
i)Joseph Kusaga (Clouds media Group)

ii) Makamba J (Naibu waziri)
 
hawa jamaa wanajiamini sana kwasababu muda wowote uingia ikulu kama sebuleni mwao, na kuhusu uhuni huu ni wa muda sanaa... Cha msingi tungoje mabadiliko watashika adabu tu.
 
duh big papa.ila usishangae ndo tabia ya chama twawala na makada wake!
 
Clouds wamekuja duniani kuwaibia watu hakuna chazaidi na ruge anatumia elimu yake kuwaibia wanamziki
 
huwa wana majidai kuwa ni watoto wa town ila mwisho wao waja.
 
asante kwa taarifa mkuu , waliwahi kumdhulumu sugu tamasha la malaria kwa kushirikiana na january.
 
hawa jamaa wanajiamini sana kwasababu muda wowote uingia ikulu kama sebuleni mwao, na kuhusu uhuni huu ni wa muda sanaa... Cha msingi tungoje mabadiliko watashika adabu tu.
Khaa!! ahadi za visasi zimekuwa nyingi sasa. Siye tunaziandika tu:whistle:
 
dah nathani huu ndo mwisho wao sasa vp ulipotuma neno stop waliacha kukukata au bado mwendo uleule? ubunifu zero cloud
 
Hata ukiomba kutolewa huduma kwa wateja hautolew na daily unakatwa zaid ya 450 wanakutumia sms 3 kila moja 150 kutoka mpaka labda utumie lugha kali kwenye mtandao unao tumia
 
Naijua issue ya malaria walipomuibia Sugu. Siku yaja watalala nao
 
Hawa jamaa huwa pia wanauwezo wa kumrubuni mkuu wa mkoa, wilaya, RPC wa sehemu husika na hata kuwarekodi na kutumia uharamia huo kwenye vyombo vyao habari kuonyesha wizi wao umehalalishwa na vyombo vya dola.

Pia walishawahi mrubuni hata waziri mkuu ahudhurie matamasha yao.
 
Wanadai wanatoa pikipiki na magari kwenye matamasha yao, lakini hakuna aliyebahatika.
 
Kwasiku naweza pokea jumbe tano...Ndo maana huwa nashindwa kuelewa kwann salio langu huwa linakkwisha bila sababu...
 
Tatizo ni TCRA ambao wanabidi kudhibiti sms zinazotumwa kwa mteja hata kama huhitaji. Pili kwa swala la privacy kampuni za simu hazitakiwi kuwapa namba za wateja mtu wa 'tatu'. La sivyo walazimishe watuma ujumbe kuandika wazi jinsi ya kujitoa badala ya mt mpaka utafute huduma kwa wateja.
 
Kinachonistua ni kutumia watumishi wa umma kama Polisi kuhamasisha mahudhurio kwenye matamasha yao.
Jeshi la Polisi pigeni marufuku MaRPC kutumika.Unakuta RPC anahojiwa anasema wananchi hudhurieni kwa wingi tutawawekea ulinzi wa kutosha!!!
watumishi wa umma wajue mipaka yao.
 
Hizo namba wanazipataje???.

Wanawezaje ku intergrate system yao na ya makampuni ya simu bila ridhaa yao???.

Hapo wa kuwalaumu si Clouds ni hayo makampuni ya simu. Wanajua kila.kitu.
 
Back
Top Bottom