Clouds Fm wamshukia Mnyika, wampuuza kwa kuchanganya mambo

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
263
13
Watangazaji wa Clouds Fm, Kibonde na Gadner wamemshukia mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA John Mnyika na kueleza kwamba anachanganya mambo. Wanahabari hao waliyasema hayo katika kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo hicho.

Jambo hilo lilijitokeza wakati wakisoma magazeti katika kipindi hicho ambapo Kibonde aliamua kumpuuza na kupuuza kuisoma habari iliyokuwa ukurasa wa mbele wa gazeti la Dar Leo.

Gazeti hilo lilinukuu kauli ya Mnyika kuhusu ripoti ya Umoja wa Mataifa(UN) inayohusisha Tanzania na tuhuma za uuzaji na silaha.

Kibonde alisema kuwa kitendo cha Mnyika kutaja suala la dhahabu na Kampuni ya Meremeta, na madini na ripoti ya UN inayohusu silaha ni kuchanganya mambo kwa lengo la ubunge wa ubungo mwaka 2010.

Hivyo, Kibonde aliacha kuisoma habari hiyo hewani kwa kauli ambayo iluungwa mkono na Gadner.

Kwa tukio hilo Clouds Fm imeweza kumuumbua vizuri Mnyika kwa kuwa redio hiyo ni kipenzi cha vijana kote Dar es salaam ikiwemo katika jimbo la Ubungo.

Tukio hilo ni dalili ya wanahabari kuwa makini katika kuchambua mambo na hivyo kuepuka propaganda chafu za wanasiasa dhidi ya CCM na serikali yake

........ndiyohiyo
 
Usihangaike na hawa ma-brainwashers wa Clouds. Kazi yao kubwa ni brain'washing ya vijana wetu kwa ajili ya kupata pesa ya harakaharaka kupitia matamasha.
 
yaani unafikia kuwafagilia clouds?.......kwa lipi mbona akina kibonde na gardener ni wauza sura tu......au wamekutuma uwaoshe zaidi kwenye jf....HATUDANGANYIKI!!!!!
eti mnyijka anaipiga vita ccm kwani we ccm ndio babako.....cjui mwandishi wa hii mada ana umri gani maana wenzako tangu uhuru chini ya ccm bado tupo hoi bin taabani........mafisadi jamani wana kampeni kali ona sasa wanamtumia vibaya kijana wa watu....
 
We can't waste our time kumjadili Kibonde, huwa anaropoka tu! Size yake ni kujadili tamasha la Fiesta yeye na watangazaji wenzake wa clouds (isipokuwa wa power breakfast) ambao wanajua kuwa duniani kuna fiesta tu na bongo flavour!
 
Ukifuatilia kipindi cha jahazi jioni cha Kibonde na Gadner na hata kipindi cha hasubuhi cha kusoma magazeti wanasoma vichwa vya habari vya magazeti mengine yote wanayatoa vichwani mwao na pia wanachagua habari ipi waisome na ipi waiache! inahudhi na inakera sana! hawa watu kuna mahali wanaegemea au wametumwa!!! fatilia Radio One na hawa uone tofauti.

Clauds Fm wakianza kusoma magazeti utafikiri ni kijiwe cha umbea na uzushi!!! hawaelewi kuwa watu wako vijijini/mikoa mbalimbali wanafuatilia habari za magazeti, inakuwa kuwasikiliza wao.
 
Hili ni tatizo kubwa sana la wanahabari wetu hasa wa redio! Kuna wakati nabadili station haraka mtu asikute nawasikiliza! Hawasomi, hawapitii habari zao wenyewe kabla ya kuzitangaza! It is pathetic! Mtangazaji anaweza kusema jambo unajiuliza, hivi kwanini analisema kama hajui? Au huwa hawajui kuwa hawajui?

Ngoja sasa atamke majina ya nchi, miji au watu! Loh! Wenzao kabla ya kwenda hewani huuliza majina yanatamkwaje na kufanya mazoezi!
 
of course yes.............wanauza sura tu
Huyu Kibonde hana lolote ni mganga njaa tuu, kuna vitu vingi tu huwa anaongea pumba, kama ukipata nafasi ukiwa Dar sikiliza kipindi cha Jahazi cha Clouds jamaa huwa anaongea pumba sana, kuanzina maswala ya siasa na hata michezo yeye alichofanya ni kuona kuna ishu ya Deep Green na Kagoda akaanza kuponda eti hivi vitu vimeingiaje humu....he cant connect them dots na jamaa nina wasiwasi hasomi na ni kilaza wa kutupwa.

The same day aliulizwa na mtangazi mwenzake kuwa mbona Blatter huko FIFA mda mrefu akaja na Pumba kwamba Rais wa FIFA ni wakudumu mpaka atakapo achia ngazi mwenyewe na ni kama TFF, what a rubbish..

At the sametime anatangaza kwamba kabla ya kwenda kwenye kipindi alipitia ANGAZA kupima kwa mara ya TATU na mambo yako shwari..ana akili huyu..

Ngoja nikamfungulie thread

T.I
 
Ukifuatilia kipindi cha jahazi jioni cha Kibonde na Gadner na hata kipindi cha hasubuhi cha kusoma magazeti wanasoma vichwa vya habari vya magazeti mengine yote wanayatoa vichwani mwao na pia wanachagua habari ipi waisome na ipi waiache! inahudhi na inakera sana! hawa watu kuna mahali wanaegemea au wametumwa!!! fatilia Radio One na hawa uone tofauti.

Clauds Fm wakianza kusoma magazeti utafikiri ni kijiwe cha umbea na uzushi!!! hawaelewi kuwa watu wako vijijini/mikoa mbalimbali wanafuatilia habari za magazeti, inakuwa kuwasikiliza wao.
Ni redio ya UDAKU kama yalivyo magazeti ya Shigongo. Na inasikilizwa sana hasa asubuhi na hicho kipindi cha jahazi. Watanzania mbongo zetu zilishasafishwa sana.
 
Tukio hilo ni dalili ya wanahabari kuwa makini katika kuchambua mambo na hivyo kuepuka propaganda chafu za wanasiasa dhidi ya CCM na serikali yake

........ndiyohiyo
Ni vyema vyombo vya habari vikajiepusha na propaganda za kisiasa, pia nivyema chombo huru cha habari kikajitenga na propaganda za kuegema upande, najua upo ukaribu Kina Kibonde na Masha, ni lazima watazichukia habari hizo nz kuziponda.
Kibonde na Gadner, sina hakika kama wanalielewa vyema sakata zima la Meremeta na biashara haramu ya silaha, ninamashaka kama wanasoma kwa ukaribu taarifa kuhusu mambo haya, kweli inashangaza.
EPHRAIM hana ubavu wa kukosoa uelewa wa mnyika John, huyu ni aina ya watu ambao huanza kukosoa habari kwakusoma vichwa vya habari, ni aibu kwao.
HAWAPENDI VIJANA WENYE AKILI ZINAZOKATA KAMA VISU, WANAPENDA vijana wenye mind za bongo flavour. wamechelewa.
 
yaani unafikia kuwafagilia clouds?.......kwa lipi mbona akina kibonde na gardener ni wauza sura tu......au wamekutuma uwaoshe zaidi kwenye jf....HATUDANGANYIKI!!!!!
eti mnyijka anaipiga vita ccm kwani we ccm ndio babako.....cjui mwandishi wa hii mada ana umri gani maana wenzako tangu uhuru chini ya ccm bado tupo hoi bin taabani........mafisadi jamani wana kampeni kali ona sasa wanamtumia vibaya kijana wa watu....

Wakati mwingine tuwe serious, hivi kweli waweza kusikiliza habari kutoka kwa "WAFUGWAJI" hawa (KI-BONDE & GARDENER) ukaamini?....they are not source of credible information, wanachojua ni kufugwa.

Sometimes ukisikiliza kipindi cha Jahazi jioni huwezi kuamini kama hiyo radio mawingu kama ina wasimamizi wa vipindi, ni utumbo mtupu wanaongea...wakurupukaji, wasio na hoja, wanaoleta ubinafsi kwenye chombo cha habari, wenye dharau, wanaotukana hovyo redioni, wafitini,,,,huenda ikiwa ni wachawi pia.

Hoja ya Mnyika iko sawa, tatizo ni Certificate zao hawawezi ku-connect hoja....nime-attach hiyo report ya UN, tatizo je wataweza japo hata kuisoma kama sio kuielewa?kwani imeandikwa kiingereza
 
Attachments

  • Group_of_Experts_Report_DRC_november_2009[1].pdf
    530.4 KB · Views: 92
No the guy is completely gabbage/trash...inaonekana hasomi wala hafuatilii mambo yanavyokwenda siyo saisa tuu hata michezo, jamaa ni wa ovyo ovyo

Sio siri kuwa Jakaya anawatumia sana clouds katika kuhamasisha vijana na ndio maana yuko karibu sana na Joseph!! Huyu mtangazaji Kibonde hana upeo mkubwa wa kujua mambo kwani elimu yake ni basic tu kwahiyo hana tools za kuweza kuona uhusiano kati ya Meremeta na hii report ya U.N. kuhusu usafirishaji wa silaha kwenda DRC kupitia Lake Tanganyika. Sintashangaa iwapo hata hiyo issue ya Meremeta pengine haijui!! Hawa ndio sampuli ya vijana Mkulu anaotaka waongoze nchi!! Kumbukeni hawa clouds ndio lilikuwa kimbilio la kwanza kwa Masha kutaka kujisafisha alipokumbana na sakata la Mengi!
 
clouds ina mpango wa kudaka tenda kwenye uchaguzi ujao kwa kuandaa majukwa na kwa kuazimisha vyombo vya muziki kwa ccm,
kwa hiyo waacheni watoto wa kusaga wajipendekeze ili wale mchongo

Tulianza na kofia, Tshirt na kanga, halafu ikaja pilau na maisha bora, usiniambie 2010 tutakula muziki na majukwaa. Hivi sisi ni mazoba kiasi hicho????? Sidhani, hatudanganyiki na muziki, viuno na majukwaa. Nadhani sasa ni ulifanya nini na unataka kufanya nini ambacho hukufanya miaka 5 iliyopita.
 
JAHAZI is absolutely trashy idiotic news ...no analysis at all, it is all about gossiping! These poorly educated guys should look for something else to do.
 
Sio siri kuwa Jakaya anawatumia sana clouds katika kuhamasisha vijana na ndio maana yuko karibu sana na Joseph!! Huyu mtangazaji Kibonde hana upeo mkubwa wa kujua mambo kwani elimu yake ni basic tu kwahiyo hana tools za kuweza kuona uhusiano kati ya Meremeta na hii report ya U.N. kuhusu usafirishaji wa silaha kwenda DRC kupitia Lake Tanganyika. Sintashangaa iwapo hata hiyo issue ya Meremeta pengine haijui!! Hawa ndio sampuli ya vijana Mkulu anaotaka waongoze nchi!! Kumbukeni hawa clouds ndio lilikuwa kimbilio la kwanza kwa Masha kutaka kujisafisha alipokumbana na sakata la Mengi!

basi ndo maana vijana hawajui wanachokifanya
 
Mwenye CV ya Ephraim Kibonde (kama anayo) naomba atuwekee hapa, inawezekana siyo tatizo lake ni vyeti.

Larry King Amesoma wapi, Yule founder wa Dell aliacha chuo, hata p diddy alikimbia shule lakini mbona hawaongei utumbo? Hebu tuache ushamba wa kila mtu akifanya kitu basi sababu ni kusoma.

Hata hivyo hawa jamaa wa jahazi wana akili zao ndiyo maana watu wanawasikiliza tatizo linalojionesha kwa hawa jamaa ni kuwa wameamua kwa makusudi kutumika na kujikomba. Ukisikiliza kipindi chao utaona kabisa mawazo yao yakisema mafisadi njooni mtutumie kuendeleza ufisadi wenu. huwezi ona mawazo ya watu walio huru. Hawa ni tatizo kwa taifa
 
Back
Top Bottom