Clouds FM: Tundu Lissu kuhamia ACT- Wazalendo

Clouds FM: Tundu Lissu kuhamia ACT- Wazalendo

Umesahau tu au kujisahaulisha. Tulipoanzisha ACT tuliambiwa kuwa ni chama cha Lowasa. Ikavuma kuwa Lowasa anakuja ACT tena kwa matusi makali makali dhidi ya ACT kutoka kwa hao hao ambao walimpokea Lowasa.

Wakati mwengine ukiwa na hekima unatazama tu mambo na kukaa kimya. Siasa za Tanzania ni moja ya Siasa za hovyo sana. Jambo ni baya akilifanya mwengine. Ukifanya wewe au aliye karibu nawe sio baya hata kidogo. Siasa za watu wasio na maarifa, wasioijua dunia, wasio na ajenda isipokuwa madaraka ya dola tu sio Siasa. Tufanye Siasa ya kukomboa watu. Tuwe na uwezo wa kuweka tofauti pembeni kwa ajili ya faida kubwa ya nchi. Mission kubwa hapa ni KUIONDOA CCM ili kuboresha maisha ya wananchi. Tu focus hapo
Umeandika kwa uchungu.
 
Leo kwenye PERUZI NA KUDADISI ya clouds FM alisikika Masudi Kipanya akisema kwamba Tundu Lisu yupo tayari kuhamia ACT- Wazalendo muda wowote kuanzia sasa. Kinachosubiriwa ni muda tu ufike.

SOURCE: Clouds FM.

MAJIBU YA ZITTO:
Siamini hadi kauli itoke kinywani mwa TL mwenyewe.
 
ni hisia za kisisiemu kutoka kwenye midomo ya wanccm kupitia chombo cha kisisiemu
 
Mambo mengine ni kukubali tu, ACT ndio inaenda kuwa main opposition party. Tukubali tukate, Chadema uwezo wao umefika mwisho. Waliharibu wakagoma kujivua gamba na kuanza kuvisha wengine gunia la umamluki.

Kwavile waligoma kutubu na kujivua gamba, huyo mdudu atawatafuna tu. Huwezi kubadili wengine kama mwenyewe hutaki kubadilika.

..kama ACT wanaweza kutupatia 40% ++ ya wabunge then wacha TL, Mdee, Sugu, Msigwa, etc etc wahamie ktk chama hicho.

..watu sasa hivi hawaangalii tena vyama wanachotaka ni DEMOKRASIA na HAKI iwepo ktk nchi yetu.
 
.niliwambiaga lowasa atahamia ccm watu walinitukana sana humu... leo narudia kusema mbowe atahamia ccm muda cio mrefu
 
Wapinzani walishapotezana 2015, there is no way watakuja kurecover kutoka ule upumbavu waliofanya any time soon...

Ona sasa hivi hadi mikutano ya ndani wanawekewa polisi, wamebanwa kila kona...
 
H
.niliwambiaga lowasa atahamia ccm watu walinitukana sana humu... leo narudia kusema mbowe atahamia ccm muda cio mrefu
Hizo habari mmewalisha matango pori wanachama wenu. Ndoto huotwa kwa u sawa kwa sisi wote.
 
Anayoyakosoa mengi ni uzushi wa kutengeneza.
Mbowe akipinga kitu huwa nashtuka kwakuwa lazima ki make a lot of sense.

Zitto noooo
Sio kwamba ni muhuni kwasababu anaisema serikali au JPM. Kigezo kikiwa hicho Mimi sikubaliani. JPM lazima asemwe anatuharobia nchi sana tu.
 
Ni vema tueleweke vizuri. Chama cha ACT kitashirikiana na vyama vingine vya upinzani katika kuunganisha nguvu kukabiliana na CCM. Vikao vya Chama vimetoa maamuzi kwa Viongozi kuwasiliana na Viongozi wa Vyama vingine ili kujenga mshikamano. Sheria ya vyama imeweka utaratibu wa namna ya Vyama kushirikiana. Tutafuata Sheria.

Ndugu Tundu Lissu ndio alama ya harakati za haki nchini kwetu kwa sasa. Tundu sio tena Mali ya chama fulani au kundi fulani la jamii. Tundu ni wa Watanzania wote. Ndio maana alipoumizwa katika jaribio la kumwua Watanzania wote bila kujali vyama wala wanakotoka walilia. Wote walishiriki kuhakikisha anapata matibabu baada ya Serikali dhalimu ya CCM kukataa kumpa stahiki zake za matibabu. Ni watu wasio na busara tu ndio wanaweza kumkumbatia Lissu kuwa ni wao peke yao. Lissu ni alama ya mapambano dhidi ya UKATILI. Ni kama vile ANC wangewaambia vyama vingine vya ukombozi kama PAC kutomtumia Mandela. Ridiculously childish!

Katika miaka 4 ya utawala wa kikatili alama inayoishi ni Tundu Lissu. Wengine hatunao, wamepotezwa. Tundu tunaye maana Mungu alifanya miujiza yake. Mungu ana sababu ya kumfanya Tundu kuwa hai. Siasa za kitoto na kibinafsi zisituondoe katika vita kubwa dhidi ya ukatili.

Sisi kama ACT tunatambua nafasi ya TL katika harakati za kuleta haki nchini kwetu. Tunatambua Lissu ni mwanachama wa CHADEMA na tutaheshimu maamuzi ya chama hicho kuhusu nafasi ambayo TL atacheza katika mtanange wa 2020. Wakimpanga kuwa mshambuliaji, Mimi nikiwa kiungo nitampa mipira atingishe nyavu. Wakiamua awe kiungo tutakuwa tayari kutingisha nyavu. Wakiamua kuwa awe Beki pia tutaheshimu.

Nawasihi Watanzania kuwa tusikubali kugawanywa. Hakuna jambo Magufuli anaogopa kama umoja wa vyama vya Upinzani. Tutazame mbele, Daima mbele nyuma mwiko ( mashabiki wa Yanga wanajua hili ).

Nkrumah: Forward Ever. Backwards Never
Binafsi ningeridhika na kuamini kama haya unayozungumza wangekuwa wanazungumza na viongozi wa vyama vingine.. Mh tatizo/ mapungufu yako ni kwamba wananchi wengi ni kama walisha declease value yako tangu enzi ukiwa CDM kwa kuaminishwa ya kwamba u msaliti ( na TL akiwemo) swali ni je lini Cledibility yako imekuwa maintained? Pia ni kwa nini ktk mawazo yako unaonyesha kutaka kumtenganisha TL na chama chake? kama umebaini kuna weakness lukuki ndani ya vyama vingine why msikae pamoja kisha mtoke kwa pamoja? Huu uchomozaji wa mmoja mmoja kila kukicha ndo kunafanya wananchi wakose imani as all na mbaya zaidi si cha kina Mbowe wala TL mwenyewe anaegusia hili
 
Ni vema tueleweke vizuri. Chama cha ACT kitashirikiana na vyama vingine vya upinzani katika kuunganisha nguvu kukabiliana na CCM. Vikao vya Chama vimetoa maamuzi kwa Viongozi kuwasiliana na Viongozi wa Vyama vingine ili kujenga mshikamano. Sheria ya vyama imeweka utaratibu wa namna ya Vyama kushirikiana. Tutafuata Sheria.

Ndugu Tundu Lissu ndio alama ya harakati za haki nchini kwetu kwa sasa. Tundu sio tena Mali ya chama fulani au kundi fulani la jamii. Tundu ni wa Watanzania wote. Ndio maana alipoumizwa katika jaribio la kumwua Watanzania wote bila kujali vyama wala wanakotoka walilia. Wote walishiriki kuhakikisha anapata matibabu baada ya Serikali dhalimu ya CCM kukataa kumpa stahiki zake za matibabu. Ni watu wasio na busara tu ndio wanaweza kumkumbatia Lissu kuwa ni wao peke yao. Lissu ni alama ya mapambano dhidi ya UKATILI. Ni kama vile ANC wangewaambia vyama vingine vya ukombozi kama PAC kutomtumia Mandela. Ridiculously childish!

Katika miaka 4 ya utawala wa kikatili alama inayoishi ni Tundu Lissu. Wengine hatunao, wamepotezwa. Tundu tunaye maana Mungu alifanya miujiza yake. Mungu ana sababu ya kumfanya Tundu kuwa hai. Siasa za kitoto na kibinafsi zisituondoe katika vita kubwa dhidi ya ukatili.

Sisi kama ACT tunatambua nafasi ya TL katika harakati za kuleta haki nchini kwetu. Tunatambua Lissu ni mwanachama wa CHADEMA na tutaheshimu maamuzi ya chama hicho kuhusu nafasi ambayo TL atacheza katika mtanange wa 2020. Wakimpanga kuwa mshambuliaji, Mimi nikiwa kiungo nitampa mipira atingishe nyavu. Wakiamua awe kiungo tutakuwa tayari kutingisha nyavu. Wakiamua kuwa awe Beki pia tutaheshimu.

Nawasihi Watanzania kuwa tusikubali kugawanywa. Hakuna jambo Magufuli anaogopa kama umoja wa vyama vya Upinzani. Tutazame mbele, Daima mbele nyuma mwiko ( mashabiki wa Yanga wanajua hili ).

Nkrumah: Forward Ever. Backwards Never

PLO alishawaambia chama pekee cha siasa Afrika ni CCM vingine ni vinapigania kuwa vyama vya siasa bado havijawa sasa unatuletea mfano wa ANC? wewe kweli hamnazo
 
Acha Uongo!!! Huyo alikuwa ni Sam Sasali hiyo jana alisema yeye kaona kwenye mitandao kuna Tetesi za Mbelgiji kuhamia ACT.



Tetesi!!! Tena mitandaoni
 
Clouds na Tbccm wanatofauti gani,sio mahali pa kuamini hata kidogo
 
Back
Top Bottom