Clouds FM: Tundu Lissu kuhamia ACT- Wazalendo

Clouds FM: Tundu Lissu kuhamia ACT- Wazalendo

GRAMAA

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2014
Posts
1,322
Reaction score
4,211
Leo kwenye PERUZI NA KUDADISI ya clouds FM alisikika Masudi Kipanya akisema kwamba Tundu Lisu yupo tayari kuhamia ACT- Wazalendo muda wowote kuanzia sasa. Kinachosubiriwa ni muda tu ufike.

SOURCE: Clouds FM.

MAJIBU YA ZITTO:

Ni vema tueleweke vizuri. Chama cha ACT kitashirikiana na vyama vingine vya upinzani katika kuunganisha nguvu kukabiliana na CCM. Vikao vya Chama vimetoa maamuzi kwa Viongozi kuwasiliana na Viongozi wa Vyama vingine ili kujenga mshikamano. Sheria ya vyama imeweka utaratibu wa namna ya Vyama kushirikiana. Tutafuata Sheria.

Ndugu Tundu Lissu ndio alama ya harakati za haki nchini kwetu kwa sasa. Tundu sio tena Mali ya chama fulani au kundi fulani la jamii. Tundu ni wa Watanzania wote. Ndio maana alipoumizwa katika jaribio la kumwua Watanzania wote bila kujali vyama wala wanakotoka walilia. Wote walishiriki kuhakikisha anapata matibabu baada ya Serikali dhalimu ya CCM kukataa kumpa stahiki zake za matibabu. Ni watu wasio na busara tu ndio wanaweza kumkumbatia Lissu kuwa ni wao peke yao. Lissu ni alama ya mapambano dhidi ya UKATILI. Ni kama vile ANC wangewaambia vyama vingine vya ukombozi kama PAC kutomtumia Mandela. Ridiculously childish!

Katika miaka 4 ya utawala wa kikatili alama inayoishi ni Tundu Lissu. Wengine hatunao, wamepotezwa. Tundu tunaye maana Mungu alifanya miujiza yake. Mungu ana sababu ya kumfanya Tundu kuwa hai. Siasa za kitoto na kibinafsi zisituondoe katika vita kubwa dhidi ya ukatili.

Sisi kama ACT tunatambua nafasi ya TL katika harakati za kuleta haki nchini kwetu. Tunatambua Lissu ni mwanachama wa CHADEMA na tutaheshimu maamuzi ya chama hicho kuhusu nafasi ambayo TL atacheza katika mtanange wa 2020. Wakimpanga kuwa mshambuliaji, Mimi nikiwa kiungo nitampa mipira atingishe nyavu. Wakiamua awe kiungo tutakuwa tayari kutingisha nyavu. Wakiamua kuwa awe Beki pia tutaheshimu.

Nawasihi Watanzania kuwa tusikubali kugawanywa. Hakuna jambo Magufuli anaogopa kama umoja wa vyama vya Upinzani. Tutazame mbele, Daima mbele nyuma mwiko ( mashabiki wa Yanga wanajua hili ).

Nkrumah: Forward Ever. Backwards Never
 
Zitto kima video anawaambia wafuasi wake kwamba ana salamu kutoka kwa Lisu kwamba yuko tayari kiungana nao kupigania haki za kidemocrasia ktika nchii hii.

Kwa ule uspecial aliopewa Lisu kwenye mkutano wa ACT mwenye akili anajua nini kinafuata.

Inawezekana Lisu hafurahishwi na jinsi Mbowe anavyo kanyaga katiba ya chadema.
 
Safi sana upinzani unachokitaka ni kumg'oa mkoloni mweusi ccm
Leo kwenye PERUZI NA KUDADISI ya clouds FM alisikika Masudi Kipanya akisema kwamba Tundu Lisu yupo tayari kuhamia ACT- Wazalendo muda wowote kuanzia sasa. Kinachosubiriwa ni muda tu ufike.

SOURCE: Clouds FM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom