Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,709
- 1,735
Kweli mgema ukimsifia tembo hulitia maji, yaonekana sasa mheshimiwa Shafi Dauda anaitumia radio kupata nafasi TFF kwa kufanya uzabizabina kuhusu StarTV kuonesha 'live' mechi (za ligi) zinazoihusu timu ya Azam FC pekee. Kinachotukera ni kumsikia akitaka kufahamu uhalali wake kana kwamba hilo ni kosa kubwa sana (la jinai!) kwa mechi za ligi yetu kuoneshwa 'live' na vituo vyetu vya TV hivo sisi wananchi (masikini na wale wote waishio nje ya Mzizima) hatuna haki kabisa ya kuona mechi hizo kupitia TV.
Tafadharini Clouds FM tunapenda kusikia habari (porojo) zenu za michezo, wakati fulani mnazungumza ukweli mtupu lakini kwa hili KERO ZAKE HAZIELEZEKI. Acheni wananchi tuone timu zetu.
Tafadharini Clouds FM tunapenda kusikia habari (porojo) zenu za michezo, wakati fulani mnazungumza ukweli mtupu lakini kwa hili KERO ZAKE HAZIELEZEKI. Acheni wananchi tuone timu zetu.