Clouds FM na website yenu!!

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Hivi watu wa Clouds FM
Naamini huwa mnatembelea humu jamvini

Mnashindwa kweli ku-update website yenu hata walau mara moja kwa wiki kama kwa kila siku haiwezekani?? hadi leo habari yenu kuu iliyopo ni matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa mwezi mzima sasa!!! Shame on You!1

Bado katika TOP 20 yenu nyimbo zilizopo mliziweka tangu mwaka jana na zipo vile vile hadi sasa. Kweli hii ndio Top 20 yenu kwa sasa hadi Prakatatumba ipo???? Haibadiliki??

Hebu jaribuni kuwa updated kidogo maana ni aibu leo kusoma habari za miezi kadhaa zikiwa ndio habari zenu kuu.

JIREKEBISHENI
 
Acha kupoteza romuda na mitandao isiyo na tija. Hujui ni chombo cha propaganda? CCM hawana jipya
 
Achana na hao watoto wa magamba.kama ulivyoshauriwa wajulishe kupitia Facebook huku huwa hawaji.
Sioni kama kuna haja ya kuwashauri hawa VINEGA..........
 
Achana na hao watoto wa magamba.kama ulivyoshauriwa wajulishe kupitia Facebook huku huwa hawaji.
Sioni kama kuna haja ya kuwashauri hawa VINEGA..........

Hahahaha, wamebadilika kuwa vinega siku hizi???
 
Watu wa Clouds wote ni feki tu...ubishoo mwingi kazi yao kuongea broken English tu basi. Bora ujisomee blogs za watu lakini si clouds media, hawana jipya na ndiyo maana nina karibia ya mwaka sasa sisikilizi redio yao.
 
Back
Top Bottom