Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 471
Habari zinasema kwamba PJ, Abel Onesmo na Gerald Hando watapigwa chini kuanzia mwezi April mwaka huu.
Kwa kawaida, Clouds wana utaratibu wa kutoa mikataba mipya kila ifikapo April 1. Katika zoezi hilo kuna wafanyakazi wapya wanaopewa mikataba na wale wa zamani ambao kituo kinawahitaji "hurenew" mikataba yao.
Imefahamika kwamba PJ , Abel Onesmo na Gerald Hando ambao wote wanatoka kipindi cha Power Breakfast (PB) watapigwa chini mwezi huu au kwa kauli ya mjini ni kwamba "Watatumbuliwa".
Sababu kubwa inayotajwa ya wakongwe hao kupigwa chini ni kushindwa kuendana na taratibu za kampuni hiyo kongwe na kinara katika sekta ya Burudani nchini kwani wanajiona wao wako juu ya watu wote.
Pia inasemekana suala la Rais Magufuli kupiga simu kwenye kipindi cha Clouds 360 limewauma sana kwani walikuwa wanaamini wao ndio kipindi bora zaidi cha asubuhi hivyo Suala la Magufuli kupiga simu 360 limeprove "otherwise".
Inadaiwa kuwa msuguano mkubwa ulianza wakati wa kipindi cha uchaguzi kutokana na kutumika kisiasa na kulipwa na baadhi ya wanasiasa ili watumie Power Breakfast kama jukwaa la kuwasafisha kinyume na maadili ya kazi yao yanayosisitiza "neutrality" katika kutoa habari.
Vilevile habari za kuaminika kutoka ndani ya Clouds zinasema kwamba tayari Clouds Media Group imeajiri vichwa vipya ambavyo kuanzia tarehe 1 vitaanza kupiga kazi.
==============
Mwingine
=============

Katika pita pita zangu leo kuachana na habari ya Marekani kutunyima msaada pale maskani kwetu, nikapata taarifa kwamba Mkurugenzi wa vipindi Clouds Fm Bwana Ruge Mutahaba amewatimua kazi watangazaji wake Gerad Hando na Paul James (PJ) na sababu ni kuwa watovu wa nidhamu.
Kufanya maamuzi magumu na sahihi, uamuzi ambao utagharimu vingi lakini mwisho wa siku mambo yatanyooka.
Hongera Ruge Mutahaba. Naamini sasa ni wakati wa maamuzi magumu na sahihi. Tumbua jipu Kwa yeyote atakayeshindwa kufuata kanuni na taratibu zake. Mwajiriwa aje kazini amelewa, afanye anavyotaka huko hatutafika. Natumaini umefanya hili baada ya kutoridhishwa na mwenendo wao licha ya kuwakanya mara nyingi.
Mwaka huu nchi itarudi kwenye mstari kama kila mmoja ataamua kusimamia maamuzi magumu na sahihi. Na hii iwe fundisho kwa wafanyakazi wa kampuni nyingine, waige mfano wako Ruge. Hata uwe na mfanyakazi bora kiasi gani, bila nidhamu ni sawa na Yai viza, likipasuka litakukera tu.