watakua hawajawaonea,wamezidi kuingilia hasa mambo ya siasa,tena kwa kuegemea chama fulani,kwani ni nani asiyewafahamu kazi yao kusifia tu viongoz wa ccm,kwa nini wasitafute mada za msingi za kuongelea mpaka wazungumzie watu binafsi,au wanahongwa ili kufanya hivyo.nadhani TCRA ikemee tabia hizi kwa sababu ni kero kubwa kwa jamii.
mkuu punguza jazba, inachofanya clouds ni sawa na magazeti ya uhuru, tanzania daima nk,
na humu jf wengi mnatatizwa na kipindi kimoja tu ambacho ni jahazi
kama unasikiliza asubuhi wana power break fast, humo nikukosoa serikali kwa kwenda mbele.
Kuna leo tena, karibu 80% ya wanawake hapa dar wanasikiliza.
Kisha kuna xxl, vijana karibu wote town hii ndio kipindi yao,
sasa kuna jahazi, hapa ndipo jf wanapochefuka simple kwasababu ya mtu mmoja tu, kibonde.
Kisha vipindi vinavyofuata ni miziki na michezo.
Jf kama great thinker sioni mantiki ya kila siku kupost mambo ya clouds na kuyapa kipaumbele utadhani issue ya maana, hii ni radio ya burudani siasa ni by the way.
Hakuna ubaya wowote kwa wao kuegemea ccm kama ilivyo sahihi kwa tanzania daima kuegemea chadema,
naomba niwe mkweli napenda kusikiliza clauds kama kituo cha burudani na nina hakika wengi wetu humu ndani niwasikilizaji wazuri wa clouds thats why chochote kitakacho jiri clouds utakikuta humu jf.
Na kama unajidanganya kuwa haipendwi jaribu kufanya jautafiti kadogo, pita uswahilini, panda madaladala utapata majibu