Clouds FM imeshakuwa Radio ya Kubet, vipindi vyote ni "Tuma Buku, Cheza na Buku, Buku Mchongo,"

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Ni aibu kwa level ya Radio kama Clouds kuwa na matangazo yanayohamasisha watu kubet kila dakika. Ubunifu wa kupata mapato umeisha wamebaki kutegemea Buku Buku za wasikilizaji. Clouds imekua radio ya ajabu sana kwasasa. Kama hali imekuwa ngumu wauze hisa tu ili wapate mwekezaji mwingine.

Mbona akina Rostam wapo tu na hela hazina kazi.
1688704283223.png
 
Nchi yenyewe hii ni ya kubet...

Tunafanya mambo kwa kutegemea wachezeshaji wengine ili tupate faida ambayo hatujui hata kama tutaipata (ingawa kwa past events na tabia zetu ni kwamba tutapigwa); Tunaishi kwa mategemeo ambayo mathematically the odds are not on our side....

Clouds yupo kazini (kwenye betting ukitaka ushinde either uwe mchezeshaji au wafundishe watu jinsi ya kucheza wewe pesa yako inakuwa guaranteed) waulize kwanini hizo buku buku wasiweke wenyewe...
 
Serikali yenyewe ina mgao kila ukishinda kuna percent kama 15 unawaachia (hapo unategemea nini); Badala ya kujenga wao ndio wanasaidia kubomoa

Aliyesema mbomoa nchi ni mwananchi nadhani hakuishi Tanzania
 
Watz tuko M 60+..….....Watu 1,000,000 wakikuchangia 1000 kila mmoja kwa siku unafikiri unapata sh ngapi..?? Ata ungekua wewe ungeacha...?
 
Back
Top Bottom