warumi kwa maelezo yako hapo juu yatosha kusema wewe ni mdau na mfuatiliaji mzuri wa Tasnia ya filamu hapa nchini.
Yawezekana nawe ni mmoja wa wasanii/watayarishaji wa filamu ambao mpo hapa JF lakini hamjaamua kutumia majina yenu.
Cloud 112 amefanya kitu kizuri kujiunga na JF, na nina thubutu kusema ni ujasiri mkubwa na pia maamuzi yake ni sahihi kwani hii itamfanya kuwa karibu na wadau wa tasnia ya filamy ambao wangependa kuchat nae na kumuuliza maswali kama hivi alivyofanya
warumi na wengine kwa lengo la kuleta mapinduzi ya kweli ya Bongo Movie.
Mwisho niwathibitishie kua
Cloud 112 ndio yeye halisi kwa maana ya actor na mtayarishaji wa Bongo movie, tunafahamiana sana na Cloud na nimewasiliana nae kuthibitisha hili. Na yeye atakuja kujibu maswali yenu hapa!