Clinton: Trump hawezi kutatua matatizo Marekani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
160729032547_hillary_clinton_624x351_reuters.jpg

Bi Clinton amesema Wamarekani wenyewe ndio wanaoweza kusuluhisha matatizo yao
Hillary Clinton amekubali rasmi kuwa mgombezi wa Urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic, huku akisema wakati wa kupambana na mpinzani wake sasa umeanza rasmi.

Alitoa wito kwa wanachama wote wa Democratic kuungana naye huku akimkebehi mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump, katika madai yake kuwa ni yeye pekee anayeweza kuyasuluhisha matatizo ya Marekani.

Alisema kuwa Wamarekani hufanya kazi kwa pamoja kyatatua yote yanayonufaisha taifa. Awali, bintiye Chelsea Clinton alikuwa ametoa hotuba na kumsifu sana mamake. Alisema ni mwanamke ambaye huwa hasahau anawapigania akina nani.

"Watu huniuliza kila wakati, huwa anawezaje kufanya haya? ... ni kwa sababu huwa hawasahau watu anaowatetea," amesema.

"Najua kwa moyo wangu wote kwamba mamangu atatufanya tujionee fahari.

Chanzo: BBC
 
Hizo ni kauli za kilevi kabisa
Anaeweza kutatua matatizo ya wamarekani angeyazuia kabla hayajaitwa matatizo
 
mama kampikie mumeo, mambo ya ikulu mwachie trump.


A classic misogynist, sad thing is you don't know you're the opposite at heart.
You can't survive and be a misogynist, without being a philogynist. Toidi.
 
Teh!, can't wait to see madame President, uone watu watavo fura. :)
 
Back
Top Bottom