Kwanza, nikupongeze kwa dhati kabisa kwa kuchaguliwa. Civil engineering ni kozi nzuri sana kwa ujumla kwani itakupa ujuzi wa kiuhalisia na sio mambo ya dhahania. Utadesign structure na utaona uhalisia wake ikisimama. Civil engineering inajumuisha sub-courses tatu ambazo ni Irrigation engineering, structural engineering na transportation& geotechnical engineering.
Hivyo basi, mwisho wa mihula minane utakuwa na ujuzi wa kutosha katika nyanja kuu tatu; TRANSPORTATION(highway geometric design, pavement design n maintenance, route location, bridges, "airport, railway n harbour engineering", etc). STRUCTURAL ENG ( Utafahamu vingi kama RC structures, steel structures, timber structures etc). IRRIGATION ENG( Utajifunza kudesign water systems, irrigation systems ktk kilimo, reservoirs n rivers, water quality control, waste water eng, na mazaga meeengi).
Kwa mfumo wa pale UD utafunzwa kwa hatua ya kuanzia chini kabisa mpaka juu na kadri miaka itakavyosonga ndivyo utakavyozidi kuwa nondo. Mtapewa lectures, tutorials na practicals za kutosha kabisa kwani kuna maabara nzuri saaana.
Angalizo ni: KASOME SANA, kozi hii inaongoza kwa kung'atua. Kuna idara ya TGE utaifahamu ukifika pale, kozi zao zina code kama TR334, TR321,TR221,TR112 nk. Hawa watu hawana masihara so jipange. Ukikaza msuli utatoka na GPA nzuri na uelewa wa kutosha( kumbuka civil engineers wako wengi kutoka vyuo vingi na wako vizuri kuliko utakavyofikiria).
Kuhama kozi inawezekana sana na ni rahisi kama ni ndani ya college moja japo sikushauri uhame civil. Cha msingi uwe na sifa stahiki kama ulivosema, min req.
Zaidi karibu sana UDSM.
(Nimeeleza kwa uchache sana, ukiwa na swali waweza uliza ndugu)