Mimi nilijisomea mwenyewe ila sikushauri ufanye kama mimi utatumia energy kubwa,tena kama unafanya kazi mahala ndo kabisaa utakosa muda wa kusoma vizuri, CISA ina mambo mengi ,ni vyema ukatafuta centers zake wapo watu wanafundisha kwa dar nishaona matangazo posta,hata humu jf pia nishaona.
Kitu cha kwanza unatakiwa uwe na kitabu cha Cisa ,ukisome chote mstari kwa mstari na kuelewa
Ufanye maswali ya kutosha kujua concepts za auditing,leadership,governance,project managements and data protection
Uingie kwenye website yao inaitwa
www.isaca.org kuomba membership ujisajili na kulipa gharama ya membership,kama unaweza lipia na mtihani hapo hapo,pia unaeza kununua vitabu vyao humo ndani ,then unasubiri watakutumia ticket ya mtihani ambayo waga ni confidential inakuelekeza mtihani unafanyika wapi lini na saa ngapi
Zamani walikua wanafanya hoteli ya new afrika kule posta ila mimi nilifanyia law school jirani na mawasiliano jijini dar mwezi june mwaka huu
Pia mitihani yao ni paper based,ila nilisoma kwenye website yao,kuanzia mwaka ujao 2017 mitihani itakua online kama CCNA etc,ko nadhani hakutakua na ishu za kusubiri matokeo kwa muda mrefu