CIA: Nyerere Under Fire. An Intelligence Assessment.

Yericko Nyerere

Verified Member
Dec 22, 2010
16,782
2,000
Weekend hii nimejipa jukumu la kusoma nyaraka na ripoti mbalimbali za kijasusi duniani, nimeona kwamba Mashirika ya ujasusi duniani kote hufanyiana ujasusi kwa kila nchi, hujasusi mambo mengi kama vile siasa, uchumi, ulinzi na usalama, mambo ya kijeshi, nk..

Ripoti ya Shirika la Ujasusi la Marekani CIA ya miaka ya 1980 na iliyoachiwa 19/01/2012 inaeleza kwa kirefu muundo wa Idara ya Usalama Tanzania TISS, udhaifu na uimara wake.

Sehemu ya ripoti hii inamuelezea mkuu wa Ujasusi wa Tanzania enzi hizo ikiitwa Tawi Maalumu (SB), Meja Jenerali Kombe kwakuangazia wasifu wake na mapito yake. Ripoti hiyo yenye kurasa 385 inabeba kichwa cha Tanzania: Nyerere Under Fire. An Intelligence Assessment.

Utangulizi wa Ripoti hiyo unamuelezea Nyerere ukiangazia hofu yake ua kupinduliwa na jeshi hasa 1964 na kwamba aliamua kulifanya jeshi kuwa la kisiasa, kwamba ili uingie jeshi ilikuwa ni lazima utoke UVCCM. Kwa maoni ya CIA ni kwamba mfumo huo wa vyombo vya ulinzi ni mfumo hatarishi katika ulimwengu mpya wa siasa za vyama vingi.

Utangulizi huo wenye jina la "Key Judgements", unakazia kwakusema kwa nadharia Tanzania inaonekana ni ya vyama vingi kimaandishi, lakini kivitendo ni ya chama kimoja na siasa imekuwa kubwa ndani ya Jeshi, Polisi na TISS ambako vyombo hivyo vimepewa mamlaka makubwa na chama tawala kuhakikisha kinabaki madarakani hali inayotafsiri dhahiri udhaifu wa idara ya usalama nchini humo.

Ukurasa wa 4 wa Ripoti hii unamuelezea kwa undani Dr Salim A. Salim kama waziri mkuu 1984 baada ya kifo cha Waziri Mkuu Sokoine. Unamueleza kama kiongozi mweledi aliyeaminiwa sana na Nyerere na mtu thabiti wa kijamaa mwenye kuheshimiwa na wajamaa duniani.

Ukurasa wa 6 wa ripoti hii wenye kichwa cha "Major Economic Activity" CIA wanaeleza kwamba kotosho ndio shughuli kuu ya kiuchumi yenye kuingiza pato kuu la kigeni katika uwanda wa Kilimo, na Katika viwanda wameitaja Cement kwamba ndio biashara kuu kwa uwanda huo. Na katika uwanda wa madini wanataja coalified kwamba ndio biashara muhimu kwa nchi. Ripoti inamambo mengi sana yenye kutuelekeza tujisahihishe kama taifa.

Ili kujua haya na mengine mengi, Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

Kwa hisani ya #MeyaBonifaceUbungo, vitabu 100 tu, utanunua kwa 56,000/= tu

0715865544 au 0755865544
IMG_20181027_090155_429.jpg
 

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
2,914
2,000
Umeongea fact mkuu kwa sasa ile mtu aingie TISS lazima awe UVCCM/CCM na huwa ninajiulizaga kuwa hivi ile dhamira ya kuwa usalama wa taifa itakuwa kwa taifa tena au itakuwa ni usalama wa CCM na viongozi wao?
 

The MaskmaN

Senior Member
Sep 28, 2017
139
250
Vitu vya moto hivi.....kuna some informations hapo kwenye bandiko hatari,kuhusu zenji..mie napita tu
 

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
6,325
2,000
Not always need a degree to operate in the field ..... but practice on safety, freedom of action and technical knowledge ..... and then the rest is a black site.
 

Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
3,569
2,000
Duh mbwembwe zoote ni pro ya kitabu. Sijui humu jf kama kuna sheria ya kulipia matangazo ya biashara
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom