CIA Director David Petraeus Resigns due to Extramarital Affair

CIA Director David Petraeus Resigns due to Extramarital Affair

Huko ni nchi za wenzetu wanaojua maana ya utumishi wa umma na uwajibikaji. Hapa kwetu ungesikia "sijiuzulu ng'o" halafu majuha mengine yangemtetea kwa visababu uchwara kama "aliyemteua bado anamwona anafaa", "mwanamme wa kiafrika kuwa rijali ni kawaida", na upuuzi mwingine kama huo.

By the way, hivi kashfa ya uzinzi (nje ya ndoa) na kuficha mabilioni Uswisi ipi kubwa na inayohitaji uwajibikaji wa mara moja au kufukuzwa kazi?

Uwajibikaji ni ukomavu wa kiutendaji na kujitambua.
 
Kweli hayo ni kwa nchi za wenzetu, nimesikia pia Putin amemfukuza kazi mnadhimu wa jeshi na maofisa wengine wa jeshi kwa tuhuma za rushwa
 
ndomana Nchi zao zinaendelea ati sisi maskani mpaka tunakufa hivi hivi
 
Mkuu ZM,sasa hapa kwetu si kila mtu anapaswa kujiuzulu kuanzia mkulu mwenyewe hadi mwalimu wa shule ya msingi,hii sio sahihi kwetu kwani tutapoteza karibu nusu ya viongozi wetu!
 
Kigezo hicho kikitumika bongo mbona patachimbika!!!
 
Mkuu ZM,sasa hapa kwetu si kila mtu anapaswa kujiuzulu kuanzia mkulu mwenyewe hadi mwalimu wa shule ya msingi,hii sio sahihi kwetu kwani tutapoteza karibu nusu ya viongozi wetu!

Hata wakibaki wa 5 lakini waadilifu tutasonga tu.
 
Mchuzi umeleta topic nzuri sana wenzetu majuu uwajibikaji ni must kwani huwana heshimu na kutii maadili kwa hapa mjni ni maumivu kwani mashirka mengi tanzania yaani kitu cha uznzi na ngono nzembe, uonevu, na dhuluma kwa watumishi wanao waongoza mfano mashirika ya hifadhi ya jamii.
 
Wenzetu wako mbali sana,bongo cfa mojawapo ya kiongozi ni kuwa na nyumba ndogo kibwena !!

ni kweli lakini punguzeni kuwavalia kimtego mtego.... mavazi yunu siku hizi ni full mitego labda ******* ndio hatanasa.. ila kwa wenzetu wako smart kosa kidogo kwaheri..amaaaaa taifa mbele kei nyuma
 
Lakini wakifanya ushoga hawawajibiki!mi nadhani hatuna cha kuwaiga,wakizinzika gogoro,wakipigwa nao mwake mwake!
 
Kuwa na mahusiano na Mke wa mtu kabla mke huyo hajaachwa rasmi na mumewe hapa inakuwaje. Au kutelekeza watoto nayo pia sifa hii haimlazimishi mtu kulazimika kujiuzulu?
 
Kwa uzinzi, wakuu wa PPF wangejiuzuru mara ngapi?





Rais Barack Obama amemkubalia Jemedari David Petraeus kujiudhuru kwa kashfa ya kuwa na mpenzi mwingine.

Amesema alifanya kosa kuwa na kidumu huku akiwa na Mke anaempenda na ambae amedumu nae kwa miaka 30,Kwa kitendo hiki amesema hakifai kwa mtumishi anaefanya kazi kwenye Taasisi inayoshughulia Maswala Nyeti ya Nchi.
 
Hii tukii2mia wabongo, moboss wengi watajiuzuru maana wapo wanaoalikwa kwenye shughuli nyeti, wanaenda na nyumba ndogo!na hatakama anakosa atasingizia siasa eti wabaya wake wanamchafua! Hatoki atatafuta kila sababu alafu ndo anabebwa. Hii nchi we acha tu.
 
Jamaa anpenda kuvaa skafu ya bendera ya taifa la tanzania kila mahali ambaye pia aliongoza kampeni za Magamba Igunga,Si alikutwa na Mke wa mtu,hakuna kemeo lolote lilitoka kwa viongozi wake! Unategemea Nini? Kuna jamaa mmmoja humu JF ankamsemo kake huwa nakatafakari sana kanasema " kama kila unapozini mtu unatoka tundu watu wangekuwa na matundu Mengi sana"
 
Dr. Petraeus alikuwa ni mmoja wa watu wachache sana ambao akiingia kwenye stadium yoyote marekani anapokewa kwa standing ovation; Ni bahati mbaya tu marekani imepoteza mtu muhimu sana katika upande sahihi wa historia ya taifa lake; Republicans kumsimamisha mtu huyu urais 2016 wangekuwa na a good shot at it;
 
The pillar of modern generals and soldiers has fallen down...what a world! I really respect this retired Gen.
 
Back
Top Bottom