Chupi za Mitumba Marufuku Ghana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chupi za Mitumba Marufuku Ghana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 22, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nguo za ndani za mitumba zitapigwa marufuku nchini Ghana kuanzia mwezi februari mwakani.
  Wapenzi wa viwalo vya ndani vilivyotumika majuu nchini Ghana wana miezi michache ya kununua viwalo vyao baada ya nguo hizo za mitumba kupigwa marufuku nchini humo.

  Bodi ya viwango ya Ghana imetangaza kuwa kuanzia mwezi februari mwakani, itakuwa ni kinyume cha sheria kuuza chupi na sidiria zilizotumika ambazo huingizwa nchini humo kama mitumba kutoka nchi za ulaya.

  Ghana ilipitisha sheria ya kupiga marufuku mitumba ya nguo za ndani mwaka 1994 lakini ilishindwa kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo.

  Lakini hivi sasa bodi ya viwango ya Ghana imetangaza kuwa itasimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria hiyo kuanzia mwezi februari mwakani.

  Wafanyabiashara wa mitumba wamelalamika kuwa ajira zao zitapotea sheria hiyo itakapoanza kutekelezwa mwakani.

  Serikali ya Ghana imesema kuwa sheria hiyo ni kwaajili ya kulinda afya za wananchi wake.
   
Loading...