Chuo Kikuu Muhimbili nao wasimamisha wanafunzi 66

2mbaku

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
316
67
SIKU moja baada ya Chuo Kikuu cha Dares Salaam kuwafukuza wanafunzi 43 , Uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), umewasimamisha masomo wanafunzi 66 kwa tuhuma za kuwa vinara wa vurugu chuoni hapo.Mbali na hatua hiyo, uongozi wa chuo hicho umeeleza kuwa mipango ya vitisho na uvunjifu wa amani chuoni hapo, bado ipo na inaleta hofu kwa walimu na wanafunzi wengine wanaoendelea na masomo.
Pallangyo alisema pia vurugu hizo zinaweza kuwa na athari kubwa hasa kwa wafadhili wao wakubwa ambao ni serikali ya Sweden, ambao walikuwepo Desemba 8, wakati wa sherehe ya utafiti chuoni hapo.
Source:Mwananchi
 
Ilikuwa siasa kwa sana hapo last month na sasa kwenye elim wakaanza kuwatimua Ud wamewafutia std 7 matokeo kwa uzembe wao wakutoweka wasimamizi imara na sasa Muhimbili. Je hii ndo Tz yetu tunayoitaka?
 
Ni ukosefu wa busara kuwaogopa wa Sweden hali unaendelea kuwakandamiza watoto wa wakulima. Palangyo amejituma kwa kiwango gani kutatua mgogoro uliopo? Kwanini aliwakimbia waandishi wa habari tar 8 na 10.12.2011?
Tatua mgogoro acha kuuahirisha.
 
Ninachoomba ni wanafunzi woooote walosimamishwa masomo kibabe waundiwe forum yao wakutane wajadili mustakabali wao, watoke na maamuzi na sisi wananchi tuwasaidie kuya-facilitate ili kuliokoa Taifa letu.
 
nakwambia mkuu kuwafukuza wanafunzi na kuwasimamisha masomo sio suluhisho la matatizo ndo kwanza wanawasha moto kwa kutumia petrol.
 
Ilikuwa siasa kwa sana hapo last month na sasa kwenye elim wakaanza kuwatimua Ud wamewafutia std 7 matokeo kwa uzembe wao wakutoweka wasimamizi imara na sasa Muhimbili. Je hii ndo Tz yetu tunayoitaka?

Mmethubutu, mmeweza mnasonga mbele na migomo. Hizo ni changamoto tu na si matatizo?
Miaka 50 ya uhuru!!!!! tafakari chukua hatua................
 
Back
Top Bottom