Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustine chamwita Profesa Baregu


BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
82,021
Likes
121,389
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
82,021 121,389 280
  • UDASA YAANDAA TAMKO
Na Boniface Meena
Mwananchi
16/Jan/2010

WAKATI wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), wakajiandaa kutoa tamko lao kuhusu ajira ya Profesa Mwesiga Baregu, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine (SAUT), kipo tayari kumwajiri mwanazuoni huyo.

Makamu mkuu wa chuo hicho, Dk Charles Kitima aliliambia gazeti hili jana kuwa Profesa Baregu, ambaye amejikita kwenye sayansi ya jamii na uhusiano wa kimataifa, ni msomi anayekubalika na kwamba chuo chake kinamhitaji hata leo kama atakuwa tayari kuajiriwa.

"Aje hata kesho (leo) kwa kuwa tunamhitaji na taaluma yake tunaihitaji. Kujiunga na chama cha siasa si uasi kwa kuwa kila mtu ni mwanachama wa chama cha siasa lakini, kinachotakiwa ni kutoingiza siasa kwenye kazi," alisema Dk Kitima.

Alisema SAUT ingependa kuwa na mwanazuoni huyo kwa kuwa inaamini kuwa hawezi kuingiza siasa darasani.

Alisema kutokana na suala la Baregu kuisumbua serikali ni muhimu sasa ikaamua kujiondoa katika ajira za waalimu wa vyuo vikuu kwa kuwa vyuo hivyo ni mali ya wananchi.

Alisema kuwa hilo ni muhimu kwa kuwa wanasiasa wanapenda wawe wanasikilizwa zaidi kuliko watu wengine na kuacha wenye taaluma wakififia na taaluma ambazo zinahitajika.

Serikali ilitangaza kuwa imeamua kutomuongezea mkataba Prof Baregu kwa mara ya nne kwa sababu hahitajiki tena baada ya kustaafu na kupewa mikataba ya ziada mitatu na pia kwa sababu sasa anashikilia wadhifa wa juu kwenye chama cha siasa, kitu ambacho ni kinyume na sheria za ajira za utumishi wa umma.

Katika hatua nyingine Chama cha Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udassa) wamesema kitendo cha serikali kutoa tamko linalohusu ajira ya Profesa Mwesiga Baregu tu ni kumtisha, hivyo watatoa tamko lao Januari 22 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Udassa, Dk Dalmas Nyaoro alisema kuwa inashangaza kuona jinsi serikali ilivyomkamia Prof Baregu hadi kuamua kutoa tamko hadharani.

"Tamko la serikali linamtaja Baregu tu, huko ni kumtisha tunataka serikali itueleze inataka aende wapi wakati kuna upungufu wa wanataaluma hapa," alisema Dk Nyaoro.

Dk Nyaoro alisema idara ina upungufu na ndiyo maana Baregu anahitajika na upungufu huo usipofanyiwa kazi, wanafunzi wanapata wakati mgumu.

Katika tamko la serikali lililosomwa na Waziri wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia ajira ya mwanazuoni huyo maarufu nchini ilikoma alipostaafu kwa mujibu wa sheria mwaka 1999.

Waziri Ghasia alisema ameamua kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo, kutokana na taarifa nyingi kuhoji kwa nini Baregu hakupewa mkataba mpya wa ajira kama ilivyokuwa kwa wahadhiri wengine waliostaafu kama yeye.

Alisema kuwa pamoja kuwa si sera ya serikali kuajiri wastaafu katika utumishi wa umma, serikali imekuwa ikitoa ajira kwa mikataba ili wasaidie kutoa huduma wakati serikali ikifanya jitihada za kujaza nafasi zilizoachwa wazi.

Ghasia alisema uamuzi wa serikali kuajiri wastaafu si endelevu, kwa kuwa nafasi wanazotumikia kwa mikataba zinatakiwa zijazwe na wataalam wapya ili waendeleze utumishi wa umma hapo baadaye.

"Kwa kutumia utaratibu huu, Baregu alistaafu kazi kwa mujibu wa sheria Februari 24 mwaka 1999 akiwa na umri wa miaka 55 na baada ya kustaafu, aliajiriwa kwa mkataba na UDSM mara tatu na mkataba wa mwisho ulimalizika Januari mwaka 2008," alisema Ghasia.
 
saitama_kein

saitama_kein

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2009
Messages
982
Likes
3
Points
33
saitama_kein

saitama_kein

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2009
982 3 33
Jamani nifahamishwe elimu ya Hawa Ghasia? Kweli ktk Karne ya 21 unafukuza mwanataaluma? Hajui profesa ni km mvinyo...unavyokaa zaidi ndo thamani yake yapanda??? Hizi Siasa zetu za bongo zisiso na mipaka nachanganyikiwa zinapoingizwa kwenye taalum....sote ni mashuhuda wa shule za sekondari za vodafasta (kata) zinavyozalisha aina mpya kabisa ya wasomi ulimwenguni.... Japan, Profesa ni zaidi ya waziri....kwa wenzangu na mie wanaotafuta mombusho scholarship pale ubalozini watakubaliana nami once akapata acceptance letter ya professor ....mchezo umekwisha interview itakuwa bye way...........Nyumbani kwetu bongo??????
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
82,021
Likes
121,389
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
82,021 121,389 280
2010-01-16 11:00:00
General assembly to act on Baregu's contract saga


The University of Dar es Salaam Academic Staff Assembly (Udasa) Chairman, Dr Dalmas Nyahoro,briefs journalists in the city yesterday on Prof Mwesiga Baregu's contract. Right is Udasa Deputy Chairman Mushtaq Osman.By Bernard Lugongo
THE CITIZEN

The lecturers of the University of Dar es Salaam (UDSM) are going to meet next week to deliberate on what action to take after the government refused to extend Prof Mwesiga Baregu's work contract.

The UDSM Academic Staff Association (Udasa) executive committee met yesterday and scrutinised a circular which the government used to block Prof Baregu from a lecturing job at university.

The executive committee declined to reveal what was discussed during the closed door meeting but said they are going to table their report when the lecturers met next week.

One of the executive committee members confided to The Citizen after the meeting that their scrutiny of the circular which was used to block Prof Baregu has found some weaknesses in the document.

"We are going to present our findings to the meeting which will be attended by all Udasa members next week and make a decision over the matter," said Udasa Chairman, Dr Dalmas Nyaoro.

Though he declined to go into the details, he said what they have found calls for immediate redress as it affects welfare of all lecturers in the country.

He said basically, the circular seek to 'gag' lecturers. He wondered: "How can intellectuals who are expected to give their views for the national development are to be muted?"

He also said that the action taken against Prof Baregu was not fair because the Government has singled out one person while there are several other lecturers who practice politics.

Prof Cuthbert Mhilu, a member of Udasa Executive Committee, said it was important for Baregu's contract be extended considering the shortage of lecturers at the University.

"In the next five years the University will suffer from the shortage of 70 per cent of lecturers because many are nearing their retirement age," he cautioned.
 
Facts1

Facts1

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2009
Messages
308
Likes
5
Points
0
Facts1

Facts1

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2009
308 5 0
Baregu for President 2010

Baregu for Presida hata mtoe thread yake,

kuhusu kwenda SAUT mimi naona asihangaike sana nafikiri hana haja ya kuajiriwa yeye aendelee tu na mambo yake ya consultancy hasa katika politics na political science.
 
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2008
Messages
7,369
Likes
1,615
Points
280
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined May 14, 2008
7,369 1,615 280
Baregu for Presida hata mtoe thread yake,

kuhusu kwenda SAUT mimi naona asihangaike sana nafikiri hana haja ya kuajiriwa yeye aendelee tu na mambo yake ya consultancy hasa katika politics na political science.
Baregu anaweza kufanya hizo consultancy zake hata akiwa anafundisha SAUT!!!
 
R

Rafikikabisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2009
Messages
252
Likes
36
Points
45
R

Rafikikabisa

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2009
252 36 45
Hapa siyo pazuri maana wengi wa wahadhiri katika chuo kikuu cha Dar es salaaam wanaelekea kwenye age ya 60 hivyo kitendo cha kutoongeza mkataba wa Baregu wengi wanaweza kukichukulia kwamba wako hatarini.

Serikali haina budi kufikiria mara mbili kuhakisha huu mkataba unakuwa renewed mara moja otherwise ikae mkao wa kura katika kuelekea uchaguzi mkuu.

Serikali haina haja ya kujiingiza katika politics zisizo na tija katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.

Achana na Baregu muongezee muda haina maana yoyote kutomuongezea muda. Kuna mambo mengi yanayotakiwa kushughulikiwa na serikali kuliko hili la Baregu.
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
82,021
Likes
121,389
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
82,021 121,389 280
Hapa siyo pazuri maana wengi wa wahadhiri katika chuo kikuu cha Dar es salaaam wanaelekea kwenye age ya 60 hivyo kitendo cha kutoongeza mkataba wa Baregu wengi wanaweza kukichukulia kwamba wako hatarini.

Serikali haina budi kufikiria mara mbili kuhakisha huu mkataba unakuwa renewed mara moja otherwise ikae mkao wa kura katika kuelekea uchaguzi mkuu.

Serikali haina haja ya kujiingiza katika politics zisizo na tija katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.

Achana na Baregu muongezee muda haina maana yoyote kutomuongezea muda. Kuna mambo mengi yanayotakiwa kushughulikiwa na serikali kuliko hili la Baregu.
Tatizo la Serikali hii ya kisanii haijaweka kabisa maslahi ya nchi mbele na badala yake wameweka maslahi yao binafsi mbele na yale ya CCM ndiyo maana wanafanya maamuzi mbali mbali kwa kurupuka bila kutafakari athari ya maamuzi yao kwa maslahi ya nchi.
 
P

PanguPakavu Amy

Senior Member
Joined
Jul 7, 2007
Messages
140
Likes
2
Points
0
P

PanguPakavu Amy

Senior Member
Joined Jul 7, 2007
140 2 0
Most accomplished academicians did get their most prized academic success at the twilight of their lives...,may be it has something to do with the utter clarity,settling old people.especially academicians.

Hapa haya politicians mmechemsha,academician hatakiwi kustaafu.just take a look at Nobel winners,most of them are way past 60!!

scientists and academicians have no Age limit.A brilliant mind has no limits,it will never have..,
 
Pengo

Pengo

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2009
Messages
579
Likes
3
Points
0
Pengo

Pengo

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2009
579 3 0
Kwani huyo Baregu ana PHD ya sayansi hadi nyie mnaojiita wana taaluma mumlilie?
Nakumbuka mwaka 1990 wakati nasoma pale UDSM, profesa M.Luhanga aliyekuwa VC alisema 'maprofesa wanaotambuliwa UDSM ni wale wenye chembechembe za sayansi tuu na hakusita kusema Luhanga,kadete,Mwandosya ndio profesa halisi sio hao wa Kiswahili,sayansi jamii,DS,na ukambala mwingine!
Huyo Baregu aende tu huyo anakohitajika kwani suala la ajira ni jinsi gani mwajiri anavyojisikia kukuajiri.Tatizo la watz wengi hawasomi kwa kujiajiri wanategemea sana kuajiriwa na ndio unaona profesa mzima analilia kuajiriwa serikalini kwanini asijiajiri mwenyewe au ndio wale maprofesa mkate kwa chai,majimarefu,simbaulanga,munufu,kajura n.k?
 
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2006
Messages
3,065
Likes
31
Points
135
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2006
3,065 31 135
Kwani huyo Baregu ana PHD ya sayansi hadi nyie mnaojiita wana taaluma mumlilie?
Nakumbuka mwaka 1990 wakati nasoma pale UDSM, profesa M.Luhanga aliyekuwa VC alisema 'maprofesa wanaotambuliwa UDSM ni wale wenye chembechembe za sayansi tuu na hakusita kusema Luhanga,kadete,Mwandosya ndio profesa halisi sio hao wa Kiswahili,sayansi jamii,DS,na ukambala mwingine!
Huyo Baregu aende tu huyo anakohitajika kwani suala la ajira ni jinsi gani mwajiri anavyojisikia kukuajiri.Tatizo la watz wengi hawasomi kwa kujiajiri wanategemea sana kuajiriwa na ndio unaona profesa mzima analilia kuajiriwa serikalini kwanini asijiajiri mwenyewe au ndio wale maprofesa mkate kwa chai,majimarefu,simbaulanga,munufu,kajura n.k?
Unapaswa kumwomba radhi Professa Baregu, kwa sababu kwanza yeye mwenyewe hajalilia, pili ujue ni watu wanaojua thamani ya Baregu kuwapo chuoni na sio mbumbumbu kama wewe japo unadai ulisoma hapo miaka ya 1990. Kauli zako ni kejeli kwa mapambano ya elimu ya watanzania. Hajashindwa kula Baregu, lakini watanzania wengi watashindwa kula kuoka kwa Baregu kwa sababu za wanasiasa uchwara ambao bahati mbaya na wewe nakuingiza huko.

Leka
 

Forum statistics

Threads 1,250,855
Members 481,494
Posts 29,748,008