Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Chalipuliwa Bungeni

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Chalipuliwa Bungeni

tatanyengo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2011
Posts
1,133
Reaction score
282
Mbunge wa CHADEMA Halima Mdee alisema bungeni jana kuwa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) kimekithiri kwa ubadhilifu wa fedha za serikali.

Akitoa mifano ya ubadhilifu huo alisema tangu chuo hicho kianzishwe mwaka 2007 kuna wafanyakazi takribani 250 wameisha acha kazi lakini mishahara ya baadhi yao bado inapelekwa chuoni hapo na kutafunwa na wajanja.

Pia alisema kuna baadhi ya watumishi wa chuo hicho wana mishahara miwili kinyume cha kanuni za utumishi wa umma. Na mbaya zaidi ni mishahara ya watumishi ambao ni marehemu mishahara yao kuendelea kupelekwa chuoni hapo.

Mdee aliendelea kusema kuwa mwaka 2010 uongozi wa chuo ulipopata fununu kuwa ukaguzi wa CAG ungefanyika chuoni hapo, uongozi wa chuo ukaandika barua serikalini kuomba mwongozo wa namna ya kutumia fedha zilizokuwa zimebaki.

My take:
Vyuo vikuu vinapaswa kuwa mfano wa kuigwa na taasisi nyingine nchini. Tunaomba pia wahusika kuimulika taasisi hiyo muhimu ili kusafisha uozo uliopo.
 
Mlacha huyo! Hata pesa za wanafunzi za field zimekatwa elf 20! Thieves
 
tatanyengoNi kweli tumisikia hiki chuo kinamabo ya udini pia.
Prof.Mlacha na Prof.Kikula wote ni sumu kwa maendeleo ya chuo.
Ni wasomi sawa ila sio viongozi ni vema serikali mkatofautisha uongozi na usomi

LWLNLW
 
Last edited by a moderator:
duh ile ya kuwalazimisha wafanyakazi wake wachukue mikopo CRDB tu inawezekana kuna kafungu nini....
 
ni vyema ushahidi uwekwe hapa ikiwa ni pamoja na majina ya wallioacha kazi lakini bado wanalipwa mishahara na wanaopokea
 
Kwani mshahara yote inakuja kama fungu moja chuoni halafu ndio inakuwa distributed kwenye akaunti zao au inalipwa vipi? maana kama inaingizwa kwenye akaunti za marehemu hamna atakayeweza kuzigusa.
 
Ha ha haa, hii nchi bana, kila kona ulaji tu!
 
Serikali sikivu sijui kama na hili imelisikia.:spy:
 
ni vyema ushahidi uwekwe hapa ikiwa ni pamoja na majina ya wallioacha kazi lakini bado wanalipwa mishahara na wanaopokea

Jamii forum ni mahali ambapo watu wanaofikiri vema hutoa issues ambazo pamoja na mambo mengine, hupelekea wahusika kujitizama upya na kujirekebisha! suala kama hili kwa kweli linahitaji ushahidi wa kutosha tena hata hapahapa jamii forum kama ifanyikavyo kwa mambo mengine ili wahusika wajirekebishe haraka kabla hawajasababisha majanga! tuwekeeni evidence za mishahara hewa, udini, n.k tuweze pia kuchangia kwa ufanisi zaidi!!! I like Jamii forum.
 
Hapa Bongo yote yanawezekana. Hapo haisikiki tena hiyo, na ikisikika itafunikwa haraka shetani apite. ONLY IN TANZANIA.
 
kazi sana hii nchi...... tunakulana tu kila angle... hatuna pa kupumulia...
 
Si wakamate tu waliokuwa wanachukua pesa wakati wahusika hawapo kazini. Hivi hii serikali mpaka mambo yaandikwe kwenye vyombo vya habari?.....mi nadhani kukamata na kuwashitaki watu km hao ni rahisi sn. Bora serikali kwa sababu haina meno kabisa iwe inaajiri watu special kwa ajili ya kushughulikia waharifu km hao
hii serikali sikivu jamani,
 
Chanzo ni Halima Mdee Bungeni, chanzo gani unachotaka kujua zaidi ya alivyoandika?
 
tatanyengoNi kweli tumisikia hiki chuo kinamabo ya udini pia.
Prof.Mlacha na Prof.Kikula wote ni sumu kwa maendeleo ya chuo.
Ni wasomi sawa ila sio viongozi ni vema serikali mkatofautisha uongozi na usomi

LWLNLW


Wa Tanganyika bwana.

Ukisikia udini pasi na shaka yoyote anakusudia Uislam.

Poleni sana , hili kovu mliloachiwa na ukoloni wa waingereza sasa ndio linakaribia kuwamaliza.
 
Back
Top Bottom