Chuo cha Bahari (DMI) chaingia mkataba wa kubadilishana uzoefu na chuo cha Italy

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Chuo cha Italian Shipping Academy Kilichopo nchini Italy ya kubadilishana uzoefu katika mafunzo ya ubaharia na kushirikiana katika tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu

MOU hiyo imesainiwa nchini Italy na Dkt.Tumaini Gurumo wa Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy(FAIMM) Eugenio Massolo.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha DMI Dkt. Tumaini Gurumo amesema kuwa makubalino hayo ya Miaka mitano yatasaidia kuongeza ujuzi kati ya Wanafunzi na Wahadhiri kwa pande zote mbili.

“Nimefurahi sana kuingia Makubaliano haya kwakua wenzetu wapo tayari kushirikiana nasi katika miradi mbalimbali, ninaona ndoto ya kufikia viwango vinavyokubalika na EU inakwenda kutimia” Alisema Dkt. Tumaini.

Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Balozi Tanzania Balozi nchini Italy Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Italy nchini Tanzania Mhe. Marco Lombardi.

Kwa upande wake Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema kuwa Italy imepiga hatua katika teknolojia hivyo utayari wao wa kushirikiana na DMI utaiwezesha zaidi Tanzania kukua katika eneo hilo. Vilele Balozi Kombo ametoa wito kwa upande wa Tanzania kuteleza ipasavyo makubalivyo MOU hiyo ili izae matunda.

Naye Mkuu wa Chuo cha Italian Shipping Academy Foundation (FAIMM) Eugenio Massolo amesema kuwa makubaliano hayo yatasidia kukuza ujuzi kwa pande zote mbili ili kuendana na uhitaji wa soko la Ajira.
 
Back
Top Bottom