Chumvi na mila zetu...

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2010
Posts
8,084
Reaction score
15,069
Habari wana jukwaa!!
Kuna swali huwa linanitatiza mara nyingi sasa sijui kama nipo jukwaa sahihi kUuliza....
Zamani kidogo kulikua na mila au tuseme desturi kwamba unapoenda kununua chumvi nyakati za jioni na usiku hutakiwi kusema naomba chumvi na ukisema chumvi unaweza usipewe huduma kabsa...kwa nyakati hzo ulitakiwa kusema naomba MUNYU au dawa ya mboga ila si chumvi....siku hz hakuna hii mambo..
Je ni sababu gani tulikatazwa kutamka chumvi usiku
 
Walikuwa wanasema eti inageuka kuwa maji!! Miezi kadhaa iliyopita nilikuwa Mtwara vijijini kabisa huko nilikataliwa kupewa chumvi dukani kwa kutamka chumvi badala ya dawa ya mboga usiku.

Na jamaa walikuwa serious wamegoma kunipa kabisa mpaka nikahama duka na nkabadilisha usemi wangu, sikujua kama wao bado wanalitilia maanani sababu
 
Je ni kweli inageuka maji??

Nini reason behind ya hii kitu??

Lazma kutakua na mafundisho yake
 

Ni imani za kale zisizokuwa na maana yoyote.
 
Jaribu kuita chumvi usiku afu uwe na bibi karibu kitakachokushtua ni mate usoni pwaaaaaaaaaaaa.
 
Dada zangu kuna kipindi walikuwa hawaruhusiwi kuweka chumvi kwenye chakula then baada ya siku 3-5 wanaruhusiwa tena kuweka chumvi!Issue ilikuwa nn?Kuna yyt anaweza akaniambia hapa? mdida DEMBA kat.ph MankaM
 
Last edited by a moderator:
Nadhani hayo ni mambo yanayowatokea huko kwenye vinchi uchwara lakini huku majuu hatunaga ushamba-ushamba wa aina hiyo kila kitu kinaitwa kwa jina lake halisi, iwe usiku ama mchana.
 
Nadhani hayo ni mambo
yanayowatokea huko kwenye vinchi uchwara lakini huku majuu hatunaga
ushamba-ushamba wa aina hiyo kila kitu kinaitwa kwa jina lake halisi,
iwe usiku ama mchana.

umeongea pumba
 
Nadhani hayo ni mambo yanayowatokea huko kwenye vinchi uchwara lakini huku majuu hatunaga ushamba-ushamba wa aina hiyo kila kitu kinaitwa kwa jina lake halisi, iwe usiku ama mchana.

Wapi huko mkuu......
Huku uchwarani lazima useme dawa ya mboga jioni...
 
Yalikuwa na maana yake japo nami cjui huruhusiwi kusema chumvi au kununua sindano pindi ifikapo jioni dukani

Wazee walikuwa na maana
 
Aisee!
Kumbe ndo maana kuna duka moja pale kinondoni shamba nilienda kununua chumvi saa mbili usiku nikanyimwa wakati naziona kabisa! Eti ananiambia hawauzi chumvi usiku!
Nilijiuliza maswali Mengi sana!
 
Duh... Sidhan kama kuna ukweli katika hili. Make mie mwenyewe nimewahi kuuza chumvi nyakati za jioni na hata usiku na wala hakukuwahi kutokea kitu chochote kwa mteja kutamka chumvi....

Ni imani tu ambayo haina maana....
 
Duh... Sidhan kama kuna ukweli katika hili. Make mie mwenyewe nimewahi kuuza chumvi nyakati za jioni na hata usiku na wala hakukuwahi kutokea kitu chochote kwa mteja kutamka chumvi....

Ni imani tu ambayo haina maana....

Kwa hiyo hawa wazee waliweka masharti tu bila kuwa na maana yeyote??!!!
 
Nafikiri ilkuwa aina ya mafunzo fulani, kama mifano inavyojieleza hapo chini

Mfano unaambiwa usishone usiku - unafundishwa usalama wako unaweza kujitoboa/kujidunga na sindano

Usifagie usiku - usiku kuna giza kwahiyo hutoweza kufagia kama inavyotakiwa

Usimruke mtu utakuwa mfupi - unafundishwa nidhamu unapotaka kupita muombe mtu akupishe sio unaruka ruka
 

Kwa wahaya inabidi useme okashenye ikishakuwa usuku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…