Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,657
- 729,766
Waliokuwa na wazo la kuwa na chumba cha wagonjwa waliozidiwa/mahututi ilikuwa ni kwa ajili ya kuokoa maisha ya wapendwa wetu...japo pamoja na kuboreshwa sana lakini mtu akipelekwa mule ndani taharuki fadhaa woga na wasiwasi hutawala ndugu jamaa na marafiki wakijiuliza kama atatoka salama!
Hii haina tofauti na chumba cha mahututi kifikra kimaono kimtazamo na hata kiutendaji, baba ndani ya familia anapotamani kuwa mlinzi ama housegirl
Hakuna kitu kibaya kama afya kukongoroka mpaka kufikia hatua ya kupelekwa hospital na ambulance kisha upelekwe ICU lakini hakuna zaidi kama kuwa na mahututi ya medulla, hapo ujue kila kitakachotoka humo ni maamuzi single phase wakati kiuhalisia ilitakiwa three phase
Chumba cha mahututi ya medulla husababisha maamuzi na utekelezaji usiotimia kwenye lolote! Huku binafsi ukijiaminisha kuwa wewe ndio wewe na unatenda katika ubora wa kiwango cha juu kabisa
Maagizo ya familia hayatolewi kwenye magenge ya kupiga stories na vijiwe vya kahawa
Teja hakamatwi na kupelekwa korokoroni bali anatakiwa tiba
Ushoga ni tatizo la kijamii zaidi kuliko la kihalifu!unamkamata shoga kisha unampeleka selo unategemea nini? Mahututi ya akili hii
Kujiapizaapiza kila wakati kujisifia weledi nk si dalili njema sana....cha kuogofya sana ni kwamba mahututi ya akili inaambukiza, ni jela ya fikra finyu inayoumiza kaya nzima na mustakabali wake
Tuitafutie tiba haraka sana