Mtuache
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 260
- 707
Habari za wakati huu members wa JF
Mimi ni kijana, sina umri wa kutisha na sijaishi maisha marefu ila nashukuru kwa miaka yote niliyoishi mpaka leo kuandika haya.
Nitakoliongelea si jambo jipya, ni kukumbushana tu
Nimezika watu wengi sana. Ndugu, majirani, marafiki, mzazi, na wengine hata siwajui. Nina uhakika hata wewe pia umezika watu wengi pengine kuzidi mimi
Misiba imekuwa ikinifirisha sana, kwanini huyu kafa mimi bado nipo hai? Je, dhumuni la mimi kuwa duniani halijatimia? Dhumuni hilo ni lipi hasa? Huyu alielala hapa ni kweli hatusikii? Wala hajui lolote linaloendelea? Na mimi nitakuja kuwa hivi? Nitafanyiwa taratibu zote anazofanyiwa huyu? Sitaweza hata kutikisa kichwa? Nitafukiwa chini na nitaachwa hapo? Je ni kweli sitomuona tena huyu mtu?
Nimekuja kugundua Maisha ya mwanadamu ni hadithi tu
Maisha anayoishi binadamu hapa ulimwenguni ni hadithi tu itakayokuja kusimuliwa na hao hao binadamu kwa binadamu wengine.
Hivyo basi ndugu yangu/Rafiki yangu/Kaka yangu/Baba yangu/Dada yangu/Mama yangu unayoyafanya leo yatakuja kusimuliwa kwa wanao/majirani/huenda hata vizazi na vizazi.
Jitahidi hadithi yako iwe nzuri masikioni mwa wasikilizaji. Kila ukitaka kulala fikiria siku ukifa watu watakuhadithia kwa lipi? Kuwa "alikuwa mlevi sana bwana, kreti ana maliza mwenyewe" au "jamaa alikuwa malaya sana, hakuna mwanamke aliyemuacha hapa mtaani"
Ulikuja duniani kulewa tu kisha ufe au ulikuja ili uwe msaada na nuru kwa wanadamu wenzio? Wanao unawaachaje? Rafiki zako unawaachia masimulizi gani? Dunia itakuwa imefaidika kwa lipi kutoka kwako? Ni kweli pengo uliloacha halitazibika? Au kifo chako kimeleta afadhali kwa kero ulizokuwa nazo?
Utaadithiwa kwa mema au kwa mabaya? Uliyoyafanya yatahadithiwa kama mafunzo mema yanayopaswa kuigwa au makatazo na maonyo makali. Utahadithiwa kama mfano mema au mbaya?
ISHI VYEMA