Chukua hatua mapema


Nani James

Nani James

Member
Joined
May 25, 2016
Messages
90
Likes
24
Points
15
Nani James

Nani James

Member
Joined May 25, 2016
90 24 15
MASOMO MATATU

SOMO LA KWANZA.

Nilikuwa kanisani nikimsikiliza muhubiri mmoja maarufu, muhibiri alitoa mfukoni noti za shilingi elfu kumi kumi zilizokuwa na jumla ya Tsh laki moja, akauliza, "ni nani miongoni mwenu anataka nimpe hii laki moja?"

Watu wengi waliokuwa mle kanisani walinyosha mikono, kila mmoja alikuwa akishauti mimi! Mimi!. Nikaanza kushangaa ni nani atakuwa na bahati ya kupewa ile pesa kati ya mamia ya watu waliohudhuria ile ibada.

Pia nikajiuliza kwa nini (ambapo bila shaka na baadhi ya wahudhuriaji wengine nao walijiuliza) atoe kitita cha shilingi laki moja kirahisi rahisi hivyo.

Wakati watu wakiendelea kupiga kelele kusema nipe mimi, nipe mimi huku wamenyosha vidole vyao, kutokea nyuma akaibuka msichana mdogo mwenye umri kama miaka 18 hivi, akaenda mbele kule aliko yule muhubiri akafika mbele na kuchukua ile laki moja kutoka mkononi mwa yule muhubiri.

"Safi sana, msichana! Umefanya vema," alisema yule muhubiri.
"Wengi wetu tunapenda kukaa tu na kusubiri mambo mazuri yaje yenyewe. Hii haitaweza kuwasaidia hata kidogo, unatakiwa kuinuka na kutafuta mafanikio. Mafanikio hayawezi kuja kama umekaa tu.

Na maisha yetu ndivyo yalivyo, tunaziona fursa nyingi sana zikiwa zimetuzunguka, kila mtu anahitaji mambo mazuri. Ila tatizo hatutaki kusimama na kuzifuata hzo fursa. Simama sasa na ufanye kitu, usisubiri mafanikio huku umekaa, kamwe hayatakuja. Usijali kuhusu watu watasema nini. Chukua hatua.

SOMO LA PILI.

Baadae yule muhubiri akatoa tena noti ya shilingi 10000 na akainyanyua ili wote tuione. Nikafikiri anarudia kama mwanzo tena. Lakini akauliza swali jepesi. "Noti hii inathamani gani?" Waumini wakajibu "shilingi elfu kumi". "Mko sahihi" akawajibu.

Akaichukua ile noti akaifinyanga finyanga na kuwauliza tena noti ile inathamani ya shilingi ngapi!? "shilingi elfu kumi" wakajibu wale wauminii!

Akaitupa chini ipe noti, akaikanyaga kanyaga sana, akaichukua na kuuluza tena noti hii ina thamani ya kiasi gani? "Shilingi elfu kumi" waumini walijibu vilevile.

Muhubiri akawaambia nataka muweka katika akili yenu hili, "mtu hata aichakaze, aikunje kunje na kuikanyaga noti ya fedha, thamani ya noti itabaki pale pale."

"Maisha yetu ndivyo yalivyo, tunatakiwa tuwe kama noti ya shilingi elfu kumi. Ktk maisha kuna kipindi tutasalitiwa, tutakanyagwa, tutaonewa na kupigwa. Ila usiache thamani yako ipotee, kwa sababu mtu amekuumiza tu, hiyo haimaanishi ndio thamani yako imepotea. Wewe ni wa thamani mno jinsi ulivyo. Usiache thamani yako ipotee kwa sababu ya wachache!

SOMO LA MWISHO.

Njia tofauti, jibu moja.
2+5=7
6+1=7
3+4=7
7-0=7
7+0=7
9-2=7
8-1=7

Pointi yangu iko wapi?

Pointi yangu ni kwamba kuna njia nyingi za kufikia mafanikio yako. Mungu hawezi kukufikisha katika mafanikio yako labda kama mama yako, baba yako, marafiki au ndugu walivyofanikiwa, kila mmoja hua na njia ya mafanikio tofauti Mungu aliyompangia.

Unaweza fikia mafanikio yako aitha kwa kuongeza watu katika maisha yako au kupunguza watu. "kujumlisha na kutoa" marafiki na baadhi ya vitu katika maisha yako kunaweza kusiwe kwa furaha kwa upande wako, ila Mungu ana makusudi yake.

Katika safari yako unaweza ukakumbana na kusalitiwa, kuumizwa kihisia, kuchekwa na kusimangwa! Acha kulia na futa machozi yako kila hali unayopitia ina makusudi yake. Mungu anakutengeneza uwe bora zaidi ya hivyo ulivyo.

Jibu langu ni jepesi tu

TUTAKUA KAMA VILE MUNGU ALIVYOTUPANGIA TUWE!
Mwenyezi Mungu awabariki.....n.usisahau kulike page yetu ya *James Nyondo stories* au fuata link hiyo https://mobile.facebook.com/James-Nyondo-stories-219395341729139/
 
Econometrician

Econometrician

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2013
Messages
9,202
Likes
9,072
Points
280
Econometrician

Econometrician

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2013
9,202 9,072 280
Mungu muweza wa yote ,mwenye huruma na upendo wote kwa nini aweke matabaka ya mafanikio kati ya mtu moja na mwingine
 
Victor wa happy

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2013
Messages
9,932
Likes
7,510
Points
280
Age
31
Victor wa happy

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2013
9,932 7,510 280
Nukuu nzuri sana

It brings courage
 
tozi25

tozi25

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2015
Messages
4,860
Likes
6,107
Points
280
tozi25

tozi25

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2015
4,860 6,107 280
Maneno mazima lakini kuna watu wataleta lawama hawa wale waliokwisha kata tamaa.
 

Forum statistics

Threads 1,236,436
Members 475,125
Posts 29,257,816