OCC Doctors
Senior Member
- Jul 20, 2018
- 104
- 151
Historia ya kina na uchunguzi kamili unapaswa kufanywa ili kubaini sababu inayowezekana zaidi na njia ya utatuzi. Ikiwa kuna upungufu wa mtiririko wa damu kwenye moyo hali inayopelekea kuzuia misuli ya moyo kupokea oksijeni ya kutosha (myocardial ischaemia) mara nyingi maumivu yake huwa ni makali nyuma ya mfupa wa wima wa kifua (Retrosternal), hutambaa kuelekea kwenye taya na mikono, maumivu huongezeka mtu akifanya harakati za mwili na hupungua akipumzika.