a sinner saved by Christ
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 3,283
- 3,739
wakati mwingine vita unayoipitia inatokana na kile ulichokibeba..mti wenye matunda ndio unapigwa mawe.NYOTA
Nyota ni hatma ya maisha yako duniani ambayo hii Roho ambayo unapewa kabla hujazaliwa duniani na unaishi nayo hapa duniani.
Mfano nyota ya Yesu ilionekana kabla hata hajazaliwa mchawi anaitwa BALAMU aliwaona wanaisraeli lakini akaona katika hao waisrael kuna mkombozi wa ulimwengu atakuja kuzaliwa,lakini hata manabii walitabiri atazaliwa.
Hata mtoto akiwa kiunononi mwa baba yake kabla hajazaliwa au akiwa tumboni mwa mama yake kabla hajazaliwa ,nyota yake inaonekana.
Ibrahimu uzao wake ulionekana kabla.
Anapozaliwa nyota yake pia inaonekana ,mfano nabii Musa na Yesu Kristo walipozaliwa nyota zao zikionekana ziki angaza nuru sana na tayari ika amuriwa amri za wafalme watoto wote wakiume wauwawe...mana walikuwa na nyota za kifalme na nguvu zaidi.
nyota ina pande tano
kama ishara ya vidole vya mikono
dole gumba-kumililiki mali
shahada pointing finger-Mamlaka uongozi
Ring finger-Ndoa na uzao
midle finger-Heshima na kibali
kidole kidogo-nimesaha kidogo ? sijui ni afya ama bahati(nitarejea )
ila ni the way mambo yako yanavyokunyokea kwa urahisi na kufanikiwa mafaniki yako kibali kukubalika ,heshima mali,utawala.
nyota ni kama natural GIFT from God inherent,
mfano unakuta kama kiongozi ukiongea unasikilizwa na watu wanakufuata una ile KIPAJI ama karama na unajikuta pia unamsukumo wa ndani na mamlaka ya kufanya na ukifanya mwitikio na watu wanatii bila kuhoji na wanakufuata.
Nyota ya biashara na mali--unaokuta kila biashara akifanya anatoboa kiurahisi
Pia nyota ya MVUTO watu wanavutiwa na wewe kama ni biashara wateja wanajazana kukufuata mvuto wako kama sumaku
mifano ni mingi..nitaweka na videos hapa chini
NGUVU YA ROHO
Hii energy unaipata kutoka kwa Mungu,ndiyo hiyo wale waliomuamini YESU kristo anawapa nguvu ya ROHO mtakatifu..hii energy wako nayo inawafanya wale wenye nguvu za giza kuwachukia kwa sababu wanaona mambo ya rohoni,pia maombi yao na nguvu zao na hata uwepo wao unaharibu nguvu zao za giza na wakijaribu kuwaloga wanashindwa wanaungua moto..kwa hiyo wanawachukia sana ROHONI japo kimwili wanaweza wakawa wanajifanya marafiki ila katika ulimwengu wa Roho ni vita inapigwa kato ya nguvu za giza ma nguvu za nuru,na siku zote nuru hufukuza giza.
Unaweza ukapendwa au ukachukiwa kwa sababu ya nyota yako.
mifano itajielezea na video nitakayoweka hap chinihttps://youtu.be/wNS5PcU9PHE?si=EJoSgspVYz_EsS5S
View: https://youtu.be/1B0OU_NOHdM?si=l7CKKDjMhXLxS4Px
wanaweza kukuchukua kabisa uwe msukule wakuweke dukani kwao uwe unavuta wateja.(Kama una nyota ya mvuto wa biashara)Umesema watu wanaweza kukuchukia kwa sababu ya nyota yako, ila nataka kufahamu vizuri zaidi nyota ni nini hasa? Ni kitu gani kwa uhalisia wake?
Also, watu wenye positive energy unawatambua vipi? Like, what really defines someone as having positive energy?
Na pia umetolea mfano wa walokole je, kuwa na nguvu kubwa kiroho mpaka ikapelekea watu kukuchukia, hiyo nguvu lazima iwe connected na kuwa mlokole? Au mtu anaweza kuwa na hiyo spiritual power bila kuwa hivyo?
Ningependa kuelewa hii kwa undani zaidi Mkuu karibu
#Happy Sunday
Imebidi nicheke πππwanaweza kukuchukua kabisa uwe msukule wakuweke dukani kwao uwe unavuta wateja.(Kama una nyota ya mvuto wa biashara)
Hapa sitakijibu saivi nataka kutulia kwaza nitarudi mkuuwakati mwingine vita unayoipitia inatokana na kile ulichokibeba..mti wenye matunda ndio unapigwa mawe.
waliobeba hatma kubwa ndio wanapitia vita kubwa zaidi,shetani anapambana zaidi na mtu mwenye kitu ndani yake.
ndio maana unaona nabii MUSA alipitia vita kubwa kabla hajazaliwa (iliamuriwa amri ya mfalme watoto wote wa kiume wauwawe) hata baada ya kufa shetani alikuja kujaribu kuiba mwili wa Musa /maiti ya Musa malaika michael akaja kupambana naye.
Nyota yako inaonekana kabla hujazaliwa ukiwa tumboni inasoma ni kama user manual au road map plan blue print kuwa wewe ni nani na umebeba kusudi gani la kuja hapa duniani na utakuwa nani na utafanya jambo gani hapa duniani na utakuwa na madhara gani katika ulimwengu wa roho ..utaharibu nguvu za giza na kuwavuta watu wengi mbinguni.
utakuwa kiongozi
tajiri mafanikio n.k
nyota yako inaweza kuzimwa kubadilishwa ,pia hatma yako inaweza kuibwa sehemu inaweza kumegwa kwa njia mbali mbali na nguvu za giza ikiwemo kupitia kuzini
kuna watu wanapewa masharti ya kulala na watu mbali mbali hata wanne au sita kwa siku na kila anayelala naye anamwibia sehemu ya nafsi yake nyota yake.
unakuta kwa mwaka amejikusanyia sehemu ya nyota za watu wengi.
View: https://youtu.be/3hVImKP4SqI?si=Ot5g50MHnaM78_jD
Asantee hii mada ishakua ngumu subiri nitarudi acha nisome kwanza kwa utulivuwakati mwingine vita unayoipitia inatokana na kile ulichokibeba..mti wenye matunda ndio unapigwa mawe.
waliobeba hatma kubwa ndio wanapitia vita kubwa zaidi,shetani anapambana zaidi na mtu mwenye kitu ndani yake.
ndio maana unaona nabii MUSA alipitia vita kubwa kabla hajazaliwa (iliamuriwa amri ya mfalme watoto wote wa kiume wauwawe) hata baada ya kufa shetani alikuja kujaribu kuiba mwili wa Musa /maiti ya Musa malaika michael akaja kupambana naye.
Nyota yako inaonekana kabla hujazaliwa ukiwa tumboni inasoma ni kama user manual au road map plan blue print kuwa wewe ni nani na umebeba kusudi gani la kuja hapa duniani na utakuwa nani na utafanya jambo gani hapa duniani na utakuwa na madhara gani katika ulimwengu wa roho ..utaharibu nguvu za giza na kuwavuta watu wengi mbinguni.
utakuwa kiongozi
tajiri mafanikio n.k
nyota yako inaweza kuzimwa kubadilishwa ,pia hatma yako inaweza kuibwa sehemu inaweza kumegwa kwa njia mbali mbali na nguvu za giza ikiwemo kupitia kuzini
kuna watu wanapewa masharti ya kulala na watu mbali mbali hata wanne au sita kwa siku na kila anayelala naye anamwibia sehemu ya nafsi yake nyota yake.
unakuta kwa mwaka amejikusanyia sehemu ya nyota za watu wengi.
View: https://youtu.be/3hVImKP4SqI?si=Ot5g50MHnaM78_jD
msukule ni mtu anachukuliwa kimazingara anafichwa hapa hapa duniani ,ndugu wanaenda kuzika mgomba ,au mti,au mnyama wakiamini wanamzika mtu.Imebidi nicheke πππ
Kwanini msukule lakini π
HOFU/UKIWA NA WOGA ni kufungulia mlango wa kuvamiwa na maroho ya nguvu za giza.NDOTO ni mlango unaoweza kutumiwa na wachawi kukushambulia .
NDOTO zote zina maana hakuna ndoto unayo ota unapokuwa umelala isiyokuwa na maana.
Chochote unachoota kwenye ndoto ni tukio halisi.
1)USILALE usiku bila ya kusali.
2)usilale usiku ukiwa na hasira moyoni au kinyongo usiwe na chuki..
3)usilale usiku ukiwa na HOFU moyoni ..hofu wasisi wasi ni michezo ya mguvu za giza kukutisha ili uingie WOGA uwatatemgeneza kishindo cha mtu kutembea juu ya dari ,au kumwaga mchanga darini au kufanya upepo uvume na vishindo juu ya paa ya nyumba yako
au bundi kulia au mapaka manyau kulia lia kama watu nje ya dirisha lako..
USIOGOPE toka nje chukua jiwe piga hilo paka kwa jina la Yesu,..atadhurika yeye na wewe utakuwa salama kwa jina la YESU.
usiogope usihofu..WOGA ndio njia wanayotumia adui kukutengenezea woga ili ufungue mlango wa nafsi wapate kukudhuru..
Unapolala usitazame video kwenye simu au kusikiliza mambo yasiyompendeza Mungu kabla ya kulala..utaota ndoto mbaya adui atakuvamia.
Usilale ukiwa na hasira ..
soma neno laMungu sikiliza mahubiri,kwaya,SALI ..Mungu atasimama na wewe katika atakupigania
NENO LA LEO
Choose your language
Zaburi 91
SRUV
Zaburi 91 10-16
Hakikisho la ulinzi wa Mungu
1Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu
Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu nitakayemtumaini.
3Maana Yeye atakuokoa kutoka kwa mtego wa mwindaji,
Na katika maradhi mabaya.
4 Kwa manyoya yake atakufunika,
Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;
Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Hutaogopa hatari za usiku,
Wala mshale urukao mchana,
6Wala mapigo yajayo usiku,
Wala maafa yatokeayo adhuhuri,
7Hata watu elfu wakianguka ubavuni pako.
Naam, watu elfu kumi katika mkono wako wa kulia!
Wewe hutakaribiwa na maafa.
8 Ila kwa macho yako utatazama,
Na kuyaona malipo ya wasio haki.
9Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu;
Umemfanya Aliye Juu kuwa makao yako.
10 Mabaya hayatakupata wewe,
Wala tauni haitaikaribia hema yako.
11 Kwa kuwa atakuagizia malaika wake
Wakulinde katika njia zako zote.
12 Mikononi mwao watakuchukua,
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13 Utawakanyaga simba na nyoka,
Mwanasimba na joka utawakanyaga kwa miguu.
14Kwa kuwa amekaza kunipenda
Nitamwokoa; na kumweka palipo juu,
Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15 Ataniita nami nitamwitikia;
Nitakuwa pamoja naye taabuni,
Nitamwokoa na kumtukuza;
16Kwa siku nyingi nitamshibisha,
Nami nitamwonesha wokovu wangu
ISAYA 54:17
Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.
Mkuu mambo haya yakuibiwa nyota is illusion don't waste ur time kusambaza mambo ya kutunga
So Fu-ck ππMind ur shit CHUKI ni issue ya kiasili hauwezi ku-deal nayo
Uki-play fair utachukiwa na uki-play unfair you will be hated too.
So Fu-ck
Ukiona mtu anasambaza hizi habari sijui za nyota ujue ndio wale waliojikatia tamaa ya maisha na wamebaki kusubiri miujiza tu iwatokee.Mkuu mambo haya yakuibiwa nyota is illusion don't waste ur time kusambaza mambo ya kutunga
Inashangaza sana mkuu.Ukiona mtu anasambaza hizi habari sijui za nyota ujue ndio wale waliojikatia tamaa ya maisha na wamebaki kusubiri miujiza iwatokee tu!
ππInashangaza sana mkuu.
Hizo juhudi angeziweka ktk kupost biashara yake sifikirii kama angekosa wateja .
Utakuja kuambiwa usibitishe kua uchawi upoπ unaweza kuthibitisha?Chuki Hukaa ndani ya moyo wa mtu mwenye chembechembe za uchawi
Mm naona hapoWengine wanasema chuki huanzia kwenye majeraha ya moyo, wengine wanaona ni wivu, hasira au kukosa msamaha.