Chuki na unafiki.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuki na unafiki....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Dec 6, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nadhani itakua wiki moja imepita sasa tangu niulize kwenye thread fulani kama inawezekana mtu akapata adui hapa JF kwasababu binafsi bado sijaona uwezekano wa kumchukia mtu ambae sijui yukoje in reality na wala hajanifanyia lolote baya hapa mtandaoni.

  Naelewa kwamba huku mitaani hua inatokea mtu , hata ndugu yako au rafiki akawa anakuchukia bila sababu maalum.Yani unakuwa hujamfanyia lolote baya, tena inawezekana ukawa mtu wa kumsupport na kumsaidia sana.Chuki ya namna hii naamini mara nyingi hua inasababishwa na wivu,yani yule mwenye chuki anatamani alichonacho mwenzake kingekua chake (pesa,mpenzi mzuri, familia inayompenda, marafiki wanaomjali, kazi nzuri n.k). Na mara nyingi hali hii hua inapelekea hao wenye wivu kutafuta namna ya kumvurugia huyo mwingine hata kwa kusambaza maneno yasiyo na ukweli.Ila sasa naomba kuuliza, sehemu kama hapa JF, sehenu ambayo wengi hatufahamiani inakuaje mtu anakua na chuki tena kali na mwenzake? Tatizo ni nini? LIKE anazopokea? Thread anazoandika? Watu anaointeract nao jamvini? Muda anaospend online? Namna anayoandika? Mambo anayoonekana kujua? Kama jibu ni moja ya hayo hapo juu nini kinakusumbua wakati hatujuani hivyo na wewe unaweza ukatumia hata google kuandika kitu kizuri kikakubalika bila yeyote kujua hazikua juhudi zako mwenyewe?

  Nimeona niandike hii mada baada ya ile incident ya Ashadii, taarifa zinazonihusu mwenyewe na wengine ambao hata hawafahamu kwamba wana maadui wasiowahitaji humu.

  Wewe kama ni mmoja wa hawa watu wenye chuki na watu usiowafahamu embu chunguza tatizo lako lilipo. Na kama tatizo liko kwao (inawezekana kuna namna wamekuboa) wasiliana nao uwajulishe badala ya kuwachekea kinafiki huku roho yako ikilika taratibu kwa chuki na kujiabisha kwa kujipeleka kwa marafiki zao (watu wanaofahamu kiukweli) na kujifanya wewe unawajua wakati huwajui.

  Wote tumekuja hapa kwa mapenzi binafsi, sio kufurahisha watu wengine bali kujifurahisha wenyewe.Ukiona unakosa hiyo furaha uliyofuata pumzika badala ya kuwatolea hasira watu wasiohusika na hasira yako. Usimchukie mtu usiye mfahamu, kwa sababu zisizo na kichwa wala vidole maana huwezi jua mtajakutana katika mazingira gani. Hii ni sehemu ya kupunguza stress na sio kuongeza, usijinyanyase kwa kutoitumia vizuri.

  Jumanne njema.
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nina chuki sana na wewe..Hunijui Sikujui achana na mimi....:eyebrows:

  Mimi huwa najiuliza mtu ana chuki na wewe hakujui wala humjui, je ikitokea bahati mbaya/nzuri akakutana na wewe atajifanya anakuchekea kinafiki, mara nyingi watu wa namna hii wanakuwa na low self esteem na kutokujiamini wao kama wao, imagine hapa JF mtu anatoka povu kweli anakusemea mbovu kweli but in real sense hakujui wala hajawahi kukuona but anajaribu ku-assume kuwa anakujua sanaaa...ohooo mara fulani hivi mara vile anavyoongea utafikiri labda ni mama yako aliyekuzaa... snitches get stitches
   
 3. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mimi nimepita tu....
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Suck it up maana Nakujua, Unanijua , siachani na wewe.

  Inashangaza kwakweli. Watu wa huku mtaani naweza jaribu kuwaelewa ila huku mtandaoni ambapo kila mtu anaingia kutokana na uwezo wa bandwith yake,sielewi kabisa.
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Hamnijui siwajui acheneni na mimi - Source Lizzy, Finest & Kongosho(promotion)

  Ha ha ha, duh jf kuna mambo

   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hahahaha!! Sasa sisi wengine kama bandwidth zetu za kungaunga mara modem ya Tigo inachukua muda mrefu ku-load kwanini tusi-mind au wewe mwenzetu unachimba bandwidth
   
 7. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wenye chuki ni wanafiki na wasiowawazi. Mimi nikichukizwa na jambo lolote nakupa laivu kitu ambacho watu wengi huchukizwa nacho. Mimi nachukia matendo na maneno tu na wala siyo mtu.
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Naomba unifupishie nimeshindwa kusoma ndefu mno nipo kwenye tuktuk.
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Unakuwa na chuki na key board hiyo ni hatari
  Hayo uliyoyasema yapo na mtu anakuwa na chuki tuu na wewe kisa may be unachangia sana post za watu au thread yako inapata wachangiaji wengi kwa wakatii ilhali yeye ya kwake haipati wachangiaji
  So mtu kama huyo anatengeneza chuki tuu na wewe
  Na watu hao wapo hata mtaani na sio hapa kwenye mtandao tuu yaani mtu anakuchukia bila sababu za maana
  Hata umuulize kisa cha kunichukia anakuwa hana sababu ilimradi tuu amekuchukia
  Maisha ni safari ignore watu kama hawa na endelea na mambo yako maana sometime unaweza kujiumiza kwa kuwafikiria
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  :lol:Fidel bana sasa kama hauwezi kusoma umejuaje kama ndefu
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hatuachani na wewe wala nini, mpaka uache kutumia slogan yetu.
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hahahhaha, kumbe hapo ndo shida ilipo.Njoo basi utumie haka kabroadband kangu ka 100mb/s ili usinichukie tena.
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Jana wewe na TF mliishia nyumba gani maana nimezunguka kwa ndugu zenu wote sikuwaona
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Yeahhh ni bora umweleze mtu ili kama kweli kakutenda vibaya ajirekebishe badala ya kujitesa mwenyewe.
   
 15. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #15
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Pole dada Lizy... I have always admired you....... Threats zako zinatia fola.....
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Njoo nikusomeee.

  @ Mr Rocky. . . . TUKO PAMOJA.
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Heheheheh. . . . sipendi umbea.
   
 18. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #18
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Asante sana
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Threat tena mpendwa?Au umemaanisha thread?
  Kama ni thread niambie zimetiaje fora ili nipunguze.

  Ohh and ahhh Ahsante, na wewe nakukubali.
   
 20. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280

  Huu sio umbea bana nina haki ya kujua
  Au nimuumbue TF hapa na mambo yake namna alivyotoroka jana na kwenda mitaa ya kati
  :focus:
   
Loading...